mr gentleman
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,222
- 4,689
Ndio awa tunasema wanacheza muziki wasoujua ilimradi mmeambiwa mcheze basi mnacheza tu. Kampuni imefanya kazi hii miaka minne nyuma sasa hapo Kitwanga alikuwaje Waziri!1. Wewe ni waziri tena wa wizara ambayo kampuni uliyoianzisha wewe wana mahusiano ya kibiashara. Je huoni kwamba kuna mgongano wa kimaslahi?
2. Ikiwa wizara yako imetangaza tenda kampuni yangu ikatenda na Infosys uliyoianzisha wewe ikatenda, naweza kupewa mimi? Hata nikikosa kwa haki na ikapata Infosys nitaridhika?
3. Hivi ni sahihi kampuni zenye mahusiano na mawaziri kufanya kazi na serikali wanayoitumikia?
4. Kampuni yako imekanusha kuijua wala kushirikiana na Lugumi. Wewe binafsi unaijua Lugumi na wamiliki wake? Kama unaijua inawezekanaje watu wa kampuni uliyoianzisha hawaijui?
5. Kelele kubwa zinaendelea kuhusu wizara unayoiongoza, kimya chako kinasababishwa na nini? Mbona hujatoka hadharani kuzungumza lolote kuhusu kinachoendelae ofisini mwako?
6. Unasubiri kutimuliwa? kwa nini usimwombe bwana mkubwa akuweke pembeni ili uchunguzi uendelee vizuri ofisini kwako?
7. Ni kweli kwamba una uhusiano/rafiki wa karibu na bwana mkubwa?
8. Uhusiano huo kama upo ni wa kawaida au wa kibiashara?
9. Kama ni wa kibisahara anahusika kwenye Infosys?
10. Kama mna uhusiano kama inavyosemekana huoni kwamba unampa mtihani mkubwa sana rafiki yako?