The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Mkuu ahsante sana kwa kuuliza maswali yenye tija, ila naomba tu niweke kumbukumbu sawa, huu mkataba wa Lugumi kuweka na kusambaza mitambo ya alama za vidole kwenye vituo vya polisi ulifanyika 2011, wakati huo waziri mwenye hiyo dhamana alikua ni mwingine. Hii haiondoi ukakasi wa uhusika wa huyu mheshimiwa ila itasaidia kujibu baadhi ya maswali yako.
Kubwa zaidi, ilikuwaje wakalipwa pesa karibia zote za mradi 99% wakati kazi hata nusu haijakamilika?
Mkubwa, hii ishu ya mkataba wa kampuni hii ni very complicated.
Kwani kumbe nje ya kampuni hii kulipwa 99% ya fedha ya makubaliano ya mkataba sawa na Tshs. 34bn kati ya 37bn, pia mshauri mwelekezi (consultant) wa mradi huu ambao ni kama haujafanyika naye amelipwa Tshs. 46bn nje ya zile zilizopo ktk mktaba!!
Si hivyo tu, bali kampuni hii ilitumia kiasi kingine cha Tshs. 5bn kwa mafunzo ya watu watano nje ya nchi na hizi pia zikiwa nje ya fedha za mkataba wenyewe!!
Kwa hiyo tunapoongelea fedha iliyolipwa kwa kampuni hii tayari na kupotea kifisadi tu ni jumla ya 34bn + 46bn + 5bn = Tshs. 85bn!!
Just imagine, 85bn zinapotea kwa njia ya "mkataba hewa" halafu kuna watu humu wanasema "vijana tuache kuendekeza siasa...", nadhani wakimaanisha tunyamaze kimya,tusihoji!!
Hili haliwezekani kamwe kwa sababu hizi ni fedha zetu kutokana na kodi tunayolipa..... lazima tuendelee kuhoji na tuhakikishe kila anayetajwa kuhusika kwa namna hii au ile awe Kitwanga au Lugumi au Ridhiwan Kikwete anaibuliwa popote alipo na hatua zichukuliwe!!
Kwa kweli tukatae "double standard" ya vita ya kupigana na ufisadi na kutumbua majipu. Popote jibu lilipo likamuliwe tu.
Inasikitisha sana, kwamba jana niliona taarifa ya habari ITV mhandisi wa maji wa wilaya ya Rorya - Mara pamoja kampuni iliyotekeleza mradi wakitiwa pingu (sema wakitumbuliwa) kwa amri ya RC Mulongo kwa kushindwa kusimamia mradi wa maji ktk kijiji kimoja huko wenye thamani kama Tshs 200 milioni na kitu hivi.
Hakukuwa na ushahidi wa kuliwa pesa wala nini wa moja kwa moja wa hawa watu, bali ni kile tu kinachoitwa "kuisaidia polisi" ktk uchunguzi wao.
Leo mkataba wa Polisi na Lugumi una siri gani eti hata tushuhudie sarakasi zenye kila dalili za kulindana!!??