Mkuu, hakuna usanii, kuna nguvu kubwa inatumika kuhakikisha JPM anatengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, kutokana na sababu kadha wa kadha. Magufuri angeweza mpatia jamaa wake wizara nono, ila alijari ulinzi wake mwenyewe. Wajanja wanataka wamcontrol JPM kupitia wizara ya mambo ya ndani. Kitu ambacho sidhani kama JPM atakiridhia any soon, maana hakuna sababu nzito ya kumuondoa jamaa. Kampuni yake ishaweka wazi kuwa walipewa mkataba wa $74,000.00 tu na si vinginevyo, kazi wamefanya na wamemaliza. Ikumbukwe hiyo $74,000.00 ni installation ya vifaa/site 108. Sasa kwanini asikomaliwe Lugumi mwenye mkataba wa 37bilion na Kashalipwa 34bilion, aje akomaliwe Kitwanga??
Je kuna mtu toka Biometrica Marekani aliyelalamikia poor installation services za infosys? Ushaambiwa infosys haina mkataba na Lugumi, ina mkataba wa kufunga vifaa vya Biometrica ambayo ilipewa kazi na Lugumi. Kwa namna hiyo muulizeni Biometrica kama hamuamini details zilizotolewa na Infosys.
Kwa kuwa swali hili lina involve US based company ni rahisi sana kupata ukweli, haya makampuni yakibanwa na mashirika yao ya kijasusi hayanaga namna, hata kama chenji watarudisha tu.
Inthemeantime kelele zote zingeelekezwa kwa Lugumi, aseme yeye basi kama kashirikiana na Infosys au Biometrica!