Inferior Complex
JF-Expert Member
- Oct 17, 2014
- 3,655
- 5,023
Suuh
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukweli upi ? Hapo hakuna ukweli wowote bali Uchakachuaji na Rushwa ndivyo vimetawala , hata mje na utetezi gani Safari hii Huyo boss wako lazima ajue kuwa Watanzania wa Sasa si wajinga kiasi hicho.Haya sasa ukweli umewekwa wazi kumbe ni juhudi za kumpiga vita Waziri Kitwanga na kutaka kuichafua serikali ya Magufuli.
Wapiga dili tafuteni kiki nyingine ukweli ndio huu.
1. Wewe ni waziri tena wa wizara ambayo kampuni uliyoianzisha wewe wana mahusiano ya kibiashara. Je huoni kwamba kuna mgongano wa kimaslahi?
2. Ikiwa wizara yako imetangaza tenda kampuni yangu ikatenda na Infosys uliyoianzisha wewe ikatenda, naweza kupewa mimi? Hata nikikosa kwa haki na ikapata Infosys nitaridhika?
3. Hivi ni sahihi kampuni zenye mahusiano na mawaziri kufanya kazi na serikali wanayoitumikia?
4. Kampuni yako imekanusha kuijua wala kushirikiana na Lugumi. Wewe binafsi unaijua Lugumi na wamiliki wake? Kama unaijua inawezekanaje watu wa kampuni uliyoianzisha hawaijui?
5. Kelele kubwa zinaendelea kuhusu wizara unayoiongoza, kimya chako kinasababishwa na nini? Mbona hujatoka hadharani kuzungumza lolote kuhusu kinachoendelae ofisini mwako?
6. Unasubiri kutimuliwa? kwa nini usimwombe bwana mkubwa akuweke pembeni ili uchunguzi uendelee vizuri ofisini kwako?
7. Ni kweli kwamba una uhusiano/rafiki wa karibu na bwana mkubwa?
8. Uhusiano huo kama upo ni wa kawaida au wa kibiashara?
9. Kama ni wa kibisahara anahusika kwenye Infosys?
10. Kama mna uhusiano kama inavyosemekana huoni kwamba unampa mtihani mkubwa sana rafiki yako?
Hii nimeipenda. Kumbe Jeshi la Police ndo iliwapa kazi Bio-Metrica LLC, na siyo Lugumu kama Meneja Msaidizi wa Infosys alivyosema. Kwa habari hiyo hapo juu Bio-Metrica LLC ndo waliokuwa main contractor! Mhh?
Mkuu, hakuna usanii, kuna nguvu kubwa inatumika kuhakikisha JPM anatengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, kutokana na sababu kadha wa kadha. Magufuri angeweza mpatia jamaa wake wizara nono, ila alijari ulinzi wake mwenyewe. Wajanja wanataka wamcontrol JPM kupitia wizara ya mambo ya ndani. Kitu ambacho sidhani kama JPM atakiridhia any soon, maana hakuna sababu nzito ya kumuondoa jamaa. Kampuni yake ishaweka wazi kuwa walipewa mkataba wa $74,000.00 tu na si vinginevyo, kazi wamefanya na wamemaliza. Ikumbukwe hiyo $74,000.00 ni installation ya vifaa/site 108. Sasa kwanini asikomaliwe Lugumi mwenye mkataba wa 37bilion na Kashalipwa 34bilion, aje akomaliwe Kitwanga??Fact kwamba Infosys imetajwa katika hilo deal na ni kweli wamekili kushiriki ni wazi kwamba yapo mengi tunayoweza kuyapata kuhusiana na ufedhuli huo. Ingekuwa hawajui chochote juu ya hilo deal, tungesema kuna haja ya kupunguza vidole na sauti kwa Infosys. Kitwanga hachomoki.
Ushauri: Acheni kufanya usanii kwani hamjui kuwa kila kitu kipo mikononi mwa vyombo vya uchunguzi kwa hatua Zaidi. Upuuzi wa kutuletea clip za kujaribu kupoteza ukweli haziwasaidii kwa sasa.
Mkuu huyo jamaa ameenda kubadili sura na atatoa mafuta kiasi tunboni pale alipoficha B zetu akirudi humjui,anaoa upya mkewe maisha yanakwenda!ni muhimu sasa kuwa na DNA profile ya watanzania wote.Kitwanga ni kweli amewabana wazee wa dili chafu.
Hii kashfa ya Lugumi inanichekesha sana, eti Lugumi kakimbia, kakimbilia wapi? Eti haijulikani......
Swali langu, is Lugumi Invisible person?
Kakamatwa gaidi àliyekimbia (mwenye kofia ya pama) kwenye tukio la ulipuzi wa wamja wa ndege Ubelgiji, huyu Lugumi asiyejua hata kusoma atajifichaje asikamatike?
Usiitie Chadema kwenye wizi wenu na wala usitafute pa kujifichia CDMUmeshaambiwa Kitwanga ni founder, ila kwa sasa sio Director, hivyo kibiashara anasubili gawio la faida mwisho wa mwaka.
Ok, hata kama Kitwanga angekuwa ni Director kwa sasa, bado wameweka mambo wazi kama infosys, ambayo yako crystal clear.
Watanzania wengi tunapelekwa na matakwa ya wanasiasa, Lowasa alivyokuwa CCM tuliambiwa ni fisadi, tukimuona tumzomee, ameingia CHADEMA amekuwa msafi kama malaika.
Vijana tuache kutumika katika siasa!
Duh, kuna kauhusiano!! Kazi ni moja inawahusu Lugumi, Biometric, Infosys kwa upande mmoja na Polisi kwa upande mwingine. Tusubiri tuoneKitaeleweka tu, mmefanya chini ya wamarekani ambao nao walikua wakifanya kazi chini ya Lugumi, bado kidogo tutapata ukweli
Waziri CK kakukosea nini ndugu?Kitwanga ndio anajaribu kujisafisha. Haya bana hata Yusuph manji hausiki kabisa na quality group kwa sasa. Hiyo infosy ni Mali ya kitwa ga
Duh vijana wengi na wachangiaji ni vilaza kwelikweli. Ukweli mmeambiwa kuwa Kitwanga is no longer in the mgt of infosys, yet hawakuingia mkataba na hiyo lugumi, zaidi na zaidi mkurugenzi wa nida siyo shareholder bado watu mnabisha tu! Je watanzania mmerogwa kuamini uongo??????? yaani ni sawa na kipindi kile watu mlimuamini lowasa kuliko magufuli ila baada ya wananchi kuamua mmeanza kujipendekeza kwa magu. In short Magufuli ni mpango wa Mungu, atafeli kila atakayeinuka kumpinga, na wengine mtakufa ili nchi yetu iende mbele, tumechoka kuishi na siasa za kudanganywa na kuamini. Sweki kamaliza kila kitu, na vita iko pale pale, waziri kitwanga ataendelea na nafasi yake, na wauza madawa mtakoma.