Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Ingekuwa vipi kama dini hazipo, ni wapi watu wangepata maarifa na taratibu za kuishi kwa hekima? Ni wapi tungepata sheria na kanuni za kutatua changamoto za kiroho?

Naelewa bado dini zipo lakini maovu yanaendelea, je ingekuwaje kama dini hazikuwepo kabisa? Inamaana maovu yangezidi na hakuna wa kukemea.

Dini zisinge kuwepo, kipimo cha uovu kingekuwa ni nini? Makatazo ya maovu yangetoka wapi?

Ingekuwa vipi?

#BM
 
Kwani wazee wako huko kijijini miaka si mingi, fanya 90 tu nyuma walikuwa na dini? Dini ni scam.
Ni kweli hawakuwa na dini, lakini walikuwa wanakesha na kuchinja mbuzi makaburini, Nadhani Dini ni njia sahihi kuliko hayo.
 
Kabla ya mwaka 1 AD hakukuwa na dini duniani japo watu walikuwepo na dhambi pia ilikuwepo kwa sababu kila penye mwanadamu hapakosi dhambi vilevile.

Hakuna kinachoweza kumaliza dhambi duniani kwa sababu Mungu alishalaani binadamu kufuatia yaliyotokea kwenye bustani ya edeni.
Ni kweli zamani sana hapakuwa na dini, lakini nadhani dini zimeletwa kama suluhisho baada ya dhambi kuzidi katika nyakati hizo
 
Kabla ya mwaka 1 AD hakukuwa na dini duniani japo watu walikuwepo na dhambi pia ilikuwepo kwa sababu kila penye mwanadamu hapakosi dhambi vilevile.

Hakuna kinachoweza kumaliza dhambi duniani kwa sababu Mungu alishalaani binadamu kufuatia yaliyotokea kwenye bustani ya edeni.
Maajabu
 
Ni kweli hawakuwa na dini, lakini walikuwa wanakesha na kuchinja mbuzi makaburini, Nadhani Dini ni njia sahihi kuliko hayo.
Dini ni mfumo wa maisha ambao jamii yoyote lazima iwe nayo by default karne na karne, shida ni pale jamii nyingine inapotaka kuwa brainwash watu wa jamii nyingine kwa kutaka kuwaletea namna yao ya kuishi kwa kigezo cha kuwamobilize, hiyo ni scam.

Mathalani, nimekwenda miji kadhaa nchi za ulaya wao wenyewe dini zimewashinda wameamua kurudi kwenye mifumo yao ya asili, sasa hivi makanisa mengi yamebaki kuwa magofu ya kiutalii, sehemu za kufanyia matamasha mbalimbali n.k.

Ifike kipindi waafrika tuamke na turudi kwenye mifumo yetu ya kizamani kabla hatujaingiliwa na hawa waarabu na wazungu.
 
Ingekuwa vipi kama dini hazipo, ni wapi watu wangepata maarifa na taratibu za kuishi kwa hekima? Ni wapi tungepata sheria na kanuni za kutatua changamoto za kiroho?

Naelewa bado dini zipo lakini maovu yanaendelea, je ingekuwaje kama dini hazikuwepo kabisa? Inamaana maovu yangezidi na hakuna wa kukemea.

Dini zisinge kuwepo, kipimo cha uovu kingekuwa ni nini? Makatazo ya maovu yangetoka wapi?

Ingekuwa vipi?
Sijui ingekuwaje, watu wanaoa watoto wa miaka 9.
Watu wangejilimbikizia wanawake 1000 na wengne kukosa.
 
Ingekuwa vipi kama dini hazipo, ni wapi watu wangepata maarifa na taratibu za kuishi kwa hekima? Ni wapi tungepata sheria na kanuni za kutatua changamoto za kiroho?

Naelewa bado dini zipo lakini maovu yanaendelea, je ingekuwaje kama dini hazikuwepo kabisa? Inamaana maovu yangezidi na hakuna wa kukemea.

Dini zisinge kuwepo, kipimo cha uovu kingekuwa ni nini? Makatazo ya maovu yangetoka wapi?

Ingekuwa vipi?
Unaposema dini unamaanisha nini?

Kama ni uislamu na ukristo, kuna nchi nyingi tu hakuna.
 
Ni aibu kuona mtu anaacha na kudharau mila na desturi za kwao ambazo zimemkuza na zimekuwa zikifanyika enzi na enzi kwa kigezo cha hizi dini mpya.
 
Binaadam kwa kutumia utashi tu angeandaa namna nyingine ya kujisimamia.

Unaona kuna hizi sheria zimesimama ili kutoa haki,ingawa sio 100% ni zao la binaadam.
Inamaana binadamu angeweza kujisimamia mwenyewe bila muongozo kutoka kwa aliyemuweka hapa Duniani?
 
Unaposema dini unamaanisha nini?

Kama ni uislamu na ukristo, kuna nchi nyingi tu hakuna.
Dini ni mfumo wa kuabudu na kuishi kwa utaratibu maalum, zipo nyingi zaidi ya ukristo na uislamu
 
Ni aibu kuona mtu anaacha na kudharau mila na desturi za kwao ambazo zimemkuza na zimekuwa zikifanyika enzi na enzi kwa kigezo cha hizi dini mpya.
Mkuu unamaanisha watu waendelee na mila zao za zamani?
 
The fact that religion is a tool of peace does not fit the facts of its history.

Religion has done more harms than good.

Nchi zinazo jifanya washika dini ndio zina ongoza kwa uovu, mabaya, vita, umaskini na ukandamizaji wa haki za binadamu.

Mifano ni mingi, Israel wanaodaiwa taifa teule ndio hao mapigano kutwa kucha,

Afghanistan, Iraq, Syria, Yemen na nchi nyingi za dola ya kiislam ndizo zinaongoza kwa Vita zisizoisha na ukandamizaji wa haki za binadamu.

Afrika inayo jifanya kushika dini ndio inaongoza kwa umaskini na matukio ya ukatili kama mauaji ya wazee, watoto, albino na wanawake. Viongozi wengi wa dini wana tuhumiwa kwa ulawiti, ubakaji na unyonyaji wa mali za raia kupitia mahubiri uchwara.

Ukija kwenye mataifa yenye furaha na Amani duniani kama Finland, Switzerland, Netherland, Sweden, Norway, Denmark, Luxembourg n.k
Dini sio jambo la msingi sana kwao na wengi wa raia wa nchi hizi ni Atheists hawaamini uwepo wa Mungu.

Ila wana ongozwa kwa sheria na misingi imara inayotoa mchango mkubwa kuleta Amani ya nchi.

DINI HAINA MCHANGO WOWOTE KULETA AMANI YA DUNIA.

SANASANA DINI IMECHANGIA PAKUBWA MNO KUVURUGA AMANI YA DUNIA NA KULETA MATABAKA YA UTENGANO.
 
Ingekuwa vipi kama dini hazipo, ni wapi watu wangepata maarifa na taratibu za kuishi kwa hekima? Ni wapi tungepata sheria na kanuni za kutatua changamoto za kiroho?

Naelewa bado dini zipo lakini maovu yanaendelea, je ingekuwaje kama dini hazikuwepo kabisa? Inamaana maovu yangezidi na hakuna wa kukemea.

Dini zisinge kuwepo, kipimo cha uovu kingekuwa ni nini? Makatazo ya maovu yangetoka wapi?

Ingekuwa vipi?
Watu wanajiwekea mifumo yao tu, hata hizo dini ni mifumo iliyowekwa na watu.

Na kama ulivyosema, dini zenyewe hazifuatwi.

Kipimo cha ubaya kinaweza kuwekwa kwa mifumo isiyo ya kidini kama sheria au haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom