Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Kwani wazee wako huko kijijini miaka si mingi, fanya 90 tu nyuma walikuwa na dini? Dini ni scam.
Ninadhani mleta mada pamoja na wachangiaji wengi hawajui hata wanachokijadili.

Miaka yote jamii karibu zote duniani zikiwemo jamii za kiafrika zimekuwa na dini.

Kabla ya kuletwa kwa imani za ukristo, uyahudi, uislamu, uhindu, ubudha, shinto nk, bado dini zilikuwepo.

Kabla ya kujadili chochote mnatakiwa mkubaliane mnaposema ''dini'' mnamaanisha nini?

Ndivyo ilivyokuwaga mijadala humu JF zamani.
 
The fact that religion is a tool of peace does not fit the facts of its history.

Religion has done more harms than good.

Nchi zinazo jifanya washika dini ndio zina ongoza kwa uovu, mabaya, vita, umaskini na ukandamizaji wa haki za binadamu.

Mifano ni mingi, Israel wanaodaiwa taifa teule ndio hao mapigano kutwa kucha,

Afghanistan, Iraq, Syria, Yemen na nchi nyingi za dola ya kiislam ndizo zinaongoza kwa Vita zisizoisha na ukandamizaji wa haki za binadamu.

Afrika inayo jifanya kushika dini ndio inaongoza kwa umaskini na matukio ya ukatili kama mauaji ya wazee, watoto, albino na wanawake. Viongozi wengi wa dini wana tuhumiwa kwa ulawiti, ubakaji na unyonyaji wa mali za raia kupitia mahubiri uchwara.

Ukija kwenye mataifa yenye furaha na Amani duniani kama Finland, Switzerland, Netherland, Sweden, Norway, Denmark, Luxembourg n.k
Dini sio jambo la msingi sana kwao na wengi wa raia wa nchi hizi ni Atheists hawaamini uwepo wa Mungu.

Ila wana ongozwa kwa sheria na misingi imara inayotoa mchango mkubwa kuleta Amani ya nchi.

DINI HAINA MCHANGO WOWOTE KULETA AMANI YA DUNIA.

SANASANA DINI IMECHANGIA PAKUBWA MNO KUVURUGA AMANI YA DUNIA NA KULETA MATABAKA YA UTENGANO.
Mkuu nimekuelewa vyema, dini kwa upande mwingine ni chanzo cha migogoro na hiyo inatokana na uelewa mdogo wa waumini katika sheria na taratibu za dini zao.
 
Mkuu nimekuelewa vyema, dini kwa upande mwingine ni chanzo cha migogoro na hiyo inatokana na uelewa mdogo wa waumini katika sheria na taratibu za dini zao.
SIYO UELEWA MDOGO, HAO WALIOANZOISHA HIZO DINI NDIO WAMEANDIKA VITABU VINAVYOBAGUA watu wasio wa dini husika.
 
Watu wanajiwekea mifumo yao tu, hata hizo dini ni mifumo iliyowekwa na watu.

Na kama ukivyosema, dini zenyewe hazifuatwi.

Kipimo cha ubaya kinaweza kuwekwa kwa mifumo isiyo ya kidini kama sheria au haki za binadamu.
Sheria za kibinadamu zina nafasi yake katika maisha, pia sheria za dini zina nafasi yake. Hata sheria za binadamu zime copy baadhi ya mambo kutoka kwa sheria za Dini
 
Ninadhani mleta mada pamoja na wachangiaji wengi hawajui hata wanachokijadili.

Miaka yote jamii karibu zote duniani zikiwemo jamii za kiafrika zimekuwa na dini.

Kabla ya kuletwa kwa imani za ukristo, uyahudi, uislamu, uhindu, ubudha, shinto nk, bado dini zilikuwepo.

Kabla ya kujadili chochote mnatakiwa mkubaliane mnaposema ''dini'' mnamaanisha nini?

Ndivyo ilivyokuwaga mijadala humu JF zamani.
Huenda ni kweli hatuelewi concept ya dini, kama yapo mengine naomba utujuze mkuu.
 
SIYO UELEWA MDOGO, HAO WALIOANZOISHA HIZO DINI NDIO WAMEANDIKA VITABU VINAVYOBAGUA watu wasio wa dini husika.
Kwa mfano hizi dini mbili kubwa, wewe unadhani nani alianzisha na kwa lengo gani hasa
 
Mnazoita dhambi ni moral values ambazo mtu yeyote mwenye common sense anafuata hata kama hana dini. Usiibe, usiue, usizini, usitamani, sambaza upendo nk. Hizi ni morals za kawaida tu huhitaji dini kujua au kufuata.
 
Watu wanajiwekea mifumo yao tu, hata hizo dini ni mifumo iliyowekwa na watu.

Na kama ukivyosema, dini zenyewe hazifuatwi.

Kipimo cha ubaya kinaweza kuwekwa kwa mifumo isiyo ya kidini kama sheria au haki za binadamu.
Karibu sana mkuu, nina siku mbili nawaza kukutafuta maana siku nyingi zimepita.
 
Inamaana binadamu angeweza kujisimamia mwenyewe bila muongozo kutoka kwa aliyemuweka hapa Duniani?
Hakuna aliyemweka binadamu hapa duniani.

Binadamu ameweza kujisimamia mwenyewe kwa kujitungia sheria ambazo huzitumia kumuongoza.
 
Ingekuwa vipi kama dini hazipo, ni wapi watu wangepata maarifa na taratibu za kuishi kwa hekima? Ni wapi tungepata sheria na kanuni za kutatua changamoto za kiroho?

Naelewa bado dini zipo lakini maovu yanaendelea, je ingekuwaje kama dini hazikuwepo kabisa? Inamaana maovu yangezidi na hakuna wa kukemea.

Dini zisinge kuwepo, kipimo cha uovu kingekuwa ni nini? Makatazo ya maovu yangetoka wapi?

Ingekuwa vipi?
Aknowledge muimbaji MWANA FALSAFA.
 
Mnazoita dhambi ni moral values ambazo mtu yeyote mwenye common sense anafuata hata kama hana dini. Usiibe, usiue, usizini, usitamani, sambaza upendo nk. Hizi ni morals za kawaida tu huhitaji dini kujua au kufuata.
Sawa mkuu, maoni mazuri hayo nimeyaelewa
 
Back
Top Bottom