Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Huwezi tenganisha makamasi na pua.
Wanaua na kusema dini imewatuma hivyo, kwanini wapagani wenzangu hawaui mtu, umeshaona mpagani anaua mtu na kulazimisha watu wawe wapagani?
Bado hayo ni makosa yao binafsi, wapo ambao wanatenda mazuri na kufuata sheria, tusiwachafue kwa makosa ya watu wengine.
 
Unazunguka mbuyu, bwana eeh , elewa dini ni ubatili mtupu, wewe amini Mungu yupo !
dini za waarabu na wazungu hazikufikishi mahali na ndio maan hizo dini zina majina ya nchi zao ama moji yao na ukislai inakubidi ujifanye unaongea kama wao waliokuletea.
 
Sawa mkuu, lakini bado hauna uhakika kama mimi ni mfuasi wa wazungu waarabu au wahindi na wachina, lengo la uzi lilikuwa ni kutafuta namna ya maisha yangelikuwaje pasipo na dini au sheria
 
Unazunguka mbuyu, bwana eeh , elewa dini ni ubatili mtupu, wewe amini Mungu yupo !
dini za waarabu na wazungu hazikufikishi mahali na ndio maan hizo dini zina majina ya nchi zao ama moji yao na ukislai inakubidi ujifanye unaongea kama wao waliokuletea.
Lugha mama kwako ni Kiswahili?
 
Watu wanajiwekea mifumo yao tu, hata hizo dini ni mifumo iliyowekwa na watu.

Na kama ulivyosema, dini zenyewe hazifuatwi.

Kipimo cha ubaya kinaweza kuwekwa kwa mifumo isiyo ya kidini kama sheria au haki za binadamu.
Hii reply inatosha kabisa kuhitimisha mjadala wa hii thread
 
What is the nature of moral law? Binadamu, kwa mfano, anajuaje kuwa kumuua binadamu mwenzake ni vibaya hata kama hakuna sheria au dini inayomkataza kuua?

Ukipata jibu la swali hili utakuwa umepata jibu la swali lako!
 
Lengo la swali langu ni kujua ulimwengu ungekuwa vipi pasipo sheria hususan za moral and responsibility.

Binadamu ana uwezo wa kutambua mazuri na mabaya lakini je ni muhimu kuwepo na sheria? Na je zisipo kuwepo mwanadamu ataweza kuishi bila kusababisha madhara kwa wengine?
 
Back
Top Bottom