Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Anaandika GEREMY BENTHAM baba wa furaha ( UTILITARIAN)

🔹 WATU HAWATENDI MEMA AU MABAYA KWA SABABU YA UWEPO AU KUTOKUWEPO KWA MUNGU AU DINI

🔹 HATA KAMA MUNGU ASINGEKUWEPO AU YUPO ILA HAJIHUSISHI NA MASUALA YA BINAADAM BADO WANGEKUWEPO WATENDA MEMA NA WATENDA MABAYA KAMA ILIVYO KWA SASA

🔹KUNA BAADH YA JAMII ZA KICHINA HAWAJUI LOLOTE KUHUSU MUNGU ILA WAMETENDA MEMA DUNIANI KWA KUGUNDUA TECHNOLOJIA ZA KUMSAIDIA BINAADAM KULIKO WENYE DINI WANSOKESHA KILA SIKU NA MAPAMBIO AU WANAOFAFIRI MPAKA SAUDI ARABIA KUMRUSHIA MAWE SHETANI NA KUZUNGUKA KALE KADUDE
 
Kweli hao wote ni binadamu, lakini hakuna sehemu umethibitisha wao ndio watunzi wa sheria hizo
Kutaka uthibitisho kama Budha, yesu na Mohamed walitunga sheria za dini ya Ubudha, ukristo na uislamu respectively,

Ni sawa na kukubali kwa mfano, kwamba Bruce Lee na Tony Jaa ni waanzilishi wa Jet kan do na Muay thai respectively kisha kutoamini kuwa hao ndio watunzi wa sheria zinazoongoza michezo hiyo ya martial arts.

Ni kweli, kunaweza kuwa na vipengele walivyokopi mahali, lakini huko walikokopi nako vilitungwa na wanadamu.
 
Anaandika GEREMY BENTHAM baba wa furaha ( UTILITARIAN)

🔹 WATU HAWATENDI MEMA AU MABAYA KWA SABABU YA UWEPO AU KUTOKUWEPO KWA MUNGU AU DINI

🔹 HATA KAMA MUNGU ASINGEKUWEPO AU YUPO ILA HAJIHUSISHI NA MASUALA YA BINAADAM BADO WANGEKUWEPO WATENDA MEMA NA WATENDA MABAYA KAMA ILIVYO KWA SASA

🔹KUNA BAADH YA JAMII ZA KICHINA HAWAJUI LOLOTE KUHUSU MUNGU ILA WAMETENDA MEMA DUNIANI KWA KUGUNDUA TECHNOLOJIA ZA KUMSAIDIA BINAADAM KULIKO WENYE DINI WANSOKESHA KILA SIKU NA MAPAMBIO AU WANAOFAFIRI MPAKA SAUDI ARABIA KUMRUSHIA MAWE SHETANI NA KUZUNGUKA KALE KADUDE
SAWA MKUU NIMEKUPATA NA HUO NI MTAZAMO WAKO JUU YA MADA HII. LAKINI SHERIA NA TARATIBU NI MUHIMU KATIKA MAISHA YA MWANADAMU
 
Sheria zinazaliwa ndani ya utashi wa watu tu , na kukubaliana kama wamoja kuziishi katika misingi ipi kwa pamoja , ili kuwa na uwiano mzuri wa maisha.
Sawa mkuu, lakini uwepo wa sheria zote za dini na za kidunia, ni muhimu kuzingatiwa kwani pasipo hivyo, vurugu na matatizo yatazidi.
 
Sijui ingekuwaje, watu wanaoa watoto wa miaka 9.
Watu wangejilimbikizia wanawake 1000 na wengne kukosa.
Unafikiri hawaolewi hao watoto wa umri huo,,na unafikiri watu hawajilimbikizii hao Wanawake Kwa sasa?Umechelewa sana yapo ma na yanafanyika vizuri mnoo,,hakuna jipya chini ya jua
 
kweli, kunaweza kuwa na vipengele walivyokopi mahali, lakini huko walikokopi nako vilitungwa na wanadamu.
Kama walikopi kwa watu wa nyuma, je ni kina nani hao na ni nani muanzilishi wa kwanza kutunga sheria hizo
 
Waumini wengi wa dini hawajui na hawaelewi vyema sheria zao, ndymaana unaona ubaguzi na migogoro.

Sheria zao zipo perfect, lakini wao wanakosa elimu na uelewa na kusababisha kutokuwa perfect katika matendo yao.
Sio kwamba hawaelewi wanaelewa na wapo sahihi kabisa kubaguana na vitabu vya dini vyote vina wataka wafanye hivyo.
 
Sio kwamba hawaelewi wanaelewa na wapo sahihi kabisa kubaguana na vitabu vya dini vyote vina wataka wafanye hivyo.
Sisi marasta man tunaamini katika peace and love for all 😂, hao wengine kama wanabaguana mimi sijui kwakweli
 
Sawa mkuu, lakini uwepo wa sheria zote za dini na za kidunia, ni muhimu kuzingatiwa kwani pasipo hivyo, vurugu na matatizo yatazidi.
Dini imejijenga kwenye miimili mitatu AHADI + KIFO + ADHABU YA MILELE ila binadamu tunatakiwa tuvuke hiyo stage ya kutenda mema pasipo ahadi wala kitisho cha kifo na adhabu za milele.
 
Sodoma na Gomora nchi nzima walikuwa wanaf**, manefili walitaka kuwaF malaila, unataka kusema dini ndio iliwafundisha hao au unaandika tu kutokea sebuleni kwa shemeji yako bila kushirikisha ubongo?

Jenga hoja au jubu hoja kwa wazo fikirishi kama ambavyo nimeweka hoja fikirishi. Sasa hapo mkuu umeongelea hoja gani au umepiga wazo langu kwa hoja ipi. Ustaarabu basi kidogo toa hoja matusi ya kitu gani kama hajaenda shule
 
Hii Biblia tunayoitumia ni Roman Catholic church ndio walioamua tuitumie kwa kuficha vitabu vingine visivyopaswa watu wa chini kuzijua siri zingine za dunia.
Yapo makusanyo mengi sana nje ya hii Biblia pale Vatican
 
Vipi kuhusu sheria zilizopo katika dini, je hazina umuhimu katika maisha ya kawaida ya mwanadamu?
Sheria nyingi zilizopo katika dini zimekuwa zikilinda status quo wa wakati huo..., Kuna suala la Watwana (watumwa) na Mabwana lilikuwa ni jambo la kawaida na ruksa kwenye maandiko..., kwanini unaweza kujiuliza, Jibu ni kwamba wakati huo ambapo nguvu kazi zilihitajika zaidi ilibidi wengi wawe watumwa kuwatumikia wachache (hence story kwamba viongozi / watawala ni chagua la Mungu)

Wengi waliotoa maandiko haya walikuwa ni wanaume utaona kinachotokea sasa katika haya maandiko kuwa yanamyanyua sana mwanaume na kumkandamiza mwanamke (na hali hio iliendana na enzi hizo sababu hata mfumo ulikuwa mfumo dume) ingekuja imani ya vice versa au tofauti na hapo angejikuta mwenye imani yake pekee....

Kwahio kama wachache wanalamba asali hata lile neno (opium) lazima li justify uwepo wa wale wachache au liwape hope hawa wengi kwamba tomorrow maybe yes (au huenda hizi dua zangu mwisho wa siku zitampata mwewe)

In conclusion kama point yako inasema kwamba watu wanafanya mema sababu ya hofu ya Mungu na sio wema sababu wanahuruma na utu; basi watu hao ni wanafiki na wanatenda mema sababu ya kuogopa kuchomwa moto na in really sense sio wema....
 
Dini imejijenga kwenye miimili mitatu AHADI + KIFO + ADHABU YA MILELE ila binadamu tunatakiwa tuvuke hiyo stage ya kutenda mema pasipo ahadi wala kitisho cha kifo na adhabu za milele.
Hapo sasa umegusa maswala ya Kiimani na kuamini, kama mtu anaamini hayo ni haki yake kufanya hivyo, kama ilivyo uhuru wa kuchagua ni wapi au nani wa kuabudiwa
 
Ingekuwa vipi kama dini hazipo, ni wapi watu wangepata maarifa na taratibu za kuishi kwa hekima? Ni wapi tungepata sheria na kanuni za kutatua changamoto za kiroho?

Naelewa bado dini zipo lakini maovu yanaendelea, je ingekuwaje kama dini hazikuwepo kabisa? Inamaana maovu yangezidi na hakuna wa kukemea.

Dini zisinge kuwepo, kipimo cha uovu kingekuwa ni nini? Makatazo ya maovu yangetoka wapi?

Ingekuwa vipi?
Umewahi kufika nchi za Scandinavia? Watu siyo washika dini, hawaendi makanisani lakini huwezi kukuta wanafanya maovu kama huku kwetu. Vipimo vya uovu ni dhamira zao. Of course siyo wote lakini wengi ndiyo walivyo. Hata kama ana uwezo wa kuiba kitu bila kujulikana lakini atakuambia dhamira yangu inaniambia ni vibaya kuiba.
 
Hapo sasa umegusa maswala ya Kiimani na kuamini, kama mtu anaamini hayo ni haki yake kufanya hivyo, kama ilivyo uhuru wa kuchagua ni wapi au nani wa kuabudiwa
Kila mtu anayo haki ya kuamni chochote anachopenda ndio
 
Umewahi kufika nchi za Scandinavia? Watu siyo washika dini, hawaendi makanisani lakini huwezi kukuta wanafanya maovu kama huku kwetu. Vipimo vya hofu ni dhamira zao. Of course siyo wote lakini wengi ndiyo walivyo. Hata kama ana uwezo wa kuiba kitu bila kujulikana lakini atakuambia dhamira yangu inaniambia ni vibaya kuiba.
NAKAZIA
 
Hata mtoto mdogo kabisa asiye jua dini yoyote ukimchunguza anatambua mema na mabaya kwa kulinganisha mazingira , ndio maana katoto kachanga ukikachekea kanatabasamu ila ukikatisha na sura kanalia.
 
Scandinavia sijawahi kufika.
Ni kweli zipo jamii zisizo na dini, lakini bado wanaishi katika misingi na sheria ambazo zinafanana za zile za dini.

Kwa jamii ambazo zimebahatika kufikiwa na dini, ni vyema kuendelea kufwata na kutii sheria na kanuni za dini zao
 
Hata mtoto mdogo kabisa asiye jua dini yoyote ukimchunguza anatambua mema na mabaya kwa kulinganisha mazingira , ndio maana katoto kachanga ukikachekea kanatabasamu ila ukikatisha na sura kanalia.
Uko sahihi kabisa.
 
Hii Biblia tunayoitumia ni Roman Catholic church ndio walioamua tuitumie kwa kuficha vitabu vingine visivyopaswa watu wa chini kuzijua siri zingine za dunia.
Yapo makusanyo mengi sana nje ya hii Biblia pale Vatican
Inamaana Bibilia ya sasa inakosa baadhi ya vipande muhimu?
 
Back
Top Bottom