Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,133
- 12,361
Umeenda vizuri, ila naomba nikuongezee kipengele kidogo.Nani huyo alisahau kukwambia haiwezekani kabisa kutenganisha maisha ya mwanadamu na dini?
Mwanadamu kihulka ni mtu wa dini. DNA yake yenyewe imekodiwa misimbo ya dini. Si ajabu vyote viwili huanza kwa herufi D! 🙂
Labda kama hujui maana ya dini, hapo unaweza kueleweka.
Hakuna kipengele cha maisha ambapo dini inaweza kukwepeka.
Mungu ana dini ya watu safi. Sheitwani Ibilisi naye ana dini yake chafu ya kuzimu.
Hapo upo?
Mwanadamu ajihadhari sana sana asije akawa anaikimbilia baharini akidhamiria kuikwepa mvua.
Siku binadamu akitambua kwamba hana amri mkataa kuhusu maisha yake, basi huo utakuwa uvumbuzi mkuu mno kuliko nadharia na mavumbuzi yote ya wanasayansi kwa pamoja.
Dini siyo lazima ihusishe mungu ama shetani.