Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Ingekuwa vipi kama dini hazipo, ni wapi watu wangepata maarifa na taratibu za kuishi kwa hekima? Ni wapi tungepata sheria na kanuni za kutatua changamoto za kiroho?

Naelewa bado dini zipo lakini maovu yanaendelea, je ingekuwaje kama dini hazikuwepo kabisa? Inamaana maovu yangezidi na hakuna wa kukemea.

Dini zisinge kuwepo, kipimo cha uovu kingekuwa ni nini? Makatazo ya maovu yangetoka wapi?

Ingekuwa vipi?
Dini ni moja tu, Uislam.

Sema kusingekuwa na wapotoshaji, wanaozuka na misamiati na kuiita dini, ingekuwaje?
 
Scandinavia sijawahi kufika.
Ni kweli zipo jamii zisizo na dini, lakini bado wanaishi katika misingi na sheria ambazo zinafanana za zile za dini.

Kwa jamii ambazo zimebahatika kufikiwa na dini, ni vyema kuendelea kufwata na kutii sheria na kanuni za dini zao
Kufikiwa na dini sio kubahatika ni kuwa na hasara kabisa kwa sababu kwenye nchi zetu maskini dini inatumika kama kete ya serikali kutukandamiza kabisa , ndio maana ni rahisi serikali kufitinika dini ikikaa upande wa haki.
 
Dini ni moja tu, Uislam.

Sema kusingekuwa na wapotoshaji, wanaozuka na misamiati na kuiita dini, ingekuwaje?
Pia nimejiuliza hata Uislamu usingekuwepo je sheria muhimu za maisha zingetoka wapi?
 
Hoja kwamba maovu yanasababishwa na kukiuka na kutofata mafundisho ya dini ni upotovu kwasababu kabla ya uwepo wa dini tayari wema na uovu ulishakuwepo. Mwanzo 1:5 tunakutana na hadithi ya kaini na abeli. Na kaini alimuua abel kwasababu ya wivu. Tayari uovu unaanzia hapa na hapo ndio kwanza dunia kwa mujibu wa kitabu cha mwanzo ilikuwa na watu wa4 tu.

Baada ya hapo tunasikia sauti ya mungu anamwuliza kaini kuwa nduguyo yuko wapi anajitetetea yeye sio mlinzi wake. Kisha mungu anamwambia sauti ya habili inanililia kutoka kwenye ardhi umemwua. Bado mingu anamuhoji je kwani ww usingefanya vyema usingepata thawabu kama yeye..... Mpk hapo unagundua
1. Hakukuwa dini
2. Ustaarabu wa maisha ulikuwepo na uliongozwa zaidi na instincts. Ila pia tunagundua kuna consice moyoni inayomwambia mwanadamu hiki kibaya hiki kizuri.
Kwahyo dini ni utaratibu ulikuwepo tu ila kabla ya ujio wake tunaona tayari kulikuwa na mila, tamaduni, taratibu na mafundisho yalishakuwepo yanaendeshwa kwa watoto na watu waZima
 
Kufikiwa na dini sio kubahatika ni kuwa na hasara kabisa kwa sababu kwenye nchi zetu maskini dini inatumika kama kete ya serikali kutukandamiza kabisa , ndio maana ni rahisi serikali kufitinika dini ikikaa upande wa haki.
Vipi kuhusu nchi tajiri, nao wana dini au hawana?
 
Hoja kwamba maovu yanasababishwa na kukiuka na kutofata mafundisho ya dini ni upotovu kwasababu kabla ya uwepo wa dini tayari wema na uovu ulishakuwepo. Mwanzo 1:5 tunakutana na hadithi ya kaini na abeli. Na kaini alimuua abel kwasababu ya wivu. Tayari uovu unaanzia hapa na hapo ndio kwanza dunia kwa mujibu wa kitabu cha mwanzo ilikuwa na watu wa4 tu.

Baada ya hapo tunasikia sauti ya mungu anamwuliza kaini kuwa nduguyo yuko wapi anajitetetea yeye sio mlinzi wake. Kisha mungu anamwambia sauti ya habili inanililia kutoka kwenye ardhi umemwua. Bado mingu anamuhoji je kwani ww usingefanya vyema usingepata thawabu kama yeye..... Mpk hapo unagundua
1. Hakukuwa dini
2. Ustaarabu wa maisha ulikuwepo na uliongozwa zaidi na instincts. Ila pia tunagundua kuna consice moyoni inayomwambia mwanadamu hiki kibaya hiki kizuri.
Kwahyo dini ni utaratibu ulikuwepo tu ila kabla ya ujio wake tunaona tayari kulikuwa na mila, tamaduni, taratibu na mafundisho yalishakuwepo yanaendeshwa kwa watoto na watu waZima
Ni kweli binadamu ana uwezo wa kutambua mabaya na mazuri ndani ya moyo wake, lakini uwepo wa sheria ni kama ukumbusho kwake kwasababu mwanadamu ni msahaulifu na amejawa na tamaa.
 
Sisi marasta man tunaamini katika peace and love for all 😂, hao wengine kama wanabaguana mimi sijui kwakweli
Marasta ni wapagani, na ni watu wa amani, hawa wenye dini za kuletewa ndio shida.
Wanaua wenzao kuwalazimisha waamini wanachoamini wao!
 
Lakini mkuu mtu kuuwa na kufanya makosa haiondoi usahihi wa dini yake, anapaswa kubeba lawama yeye na sio dini yake
 
Nguvu kwa maana gani? Ushawishi au wingi wa waumini?
Nchi zilizoendelea jamii nyingi za watu wanajitambua japo wana dini hauwezi kuona matukio kama yale ya makenzie na serikali zipo macho mno kufuatilia mienendo ya dini
 
Inamaana nchi zilizo endelea wana maadili mazuri kuliko waafrika?
 
Africa maadili yetu yanaenda kuporomoka kwa kasi sana ya kuishi kama ndugu baina yetu na kupendana ,pia hizo dini zikiwa na mchango mkubwa sana katika kutugawa.

Leo hii binti wa kibantu ana shindwa kupendana na kijana wa kibantu kwa misimamo ya kidini .
 
Mkuu umesema vyema, lakini still Ni muhimu kuishi kwa kufuata sheria bila kujali ni dini au imani gani mtu anayo.
 
Back
Top Bottom