UDENYE
JF-Expert Member
- Mar 17, 2016
- 318
- 201
Hao wanaume wote waliotawala takriban miaka khamsini wameleta maajabu gani? Heshimuni wanawake ni mama zenu waliowazaa, wana akili na maarifa sawa na wengine kuzidi wanaume. Mambo ya mila na tamaduni potofu za kumdharau na kumdodesha mwanamke zimepitwa na wakati. Kwa ushauri wangu Mama apindue katiba, atuongoze miaka myengine 25 mbele. Na kama itampendeza nnafasi zote nyeti atuwekee kina mama, mathalan mkuu wa majeshi, mkuu wa jeshi la polisi, mkuu wa jeshi la magereza, Jaji mkuu na majaji wa mahakama,waziri mkuu na makamu wa raisi. Pia atuwekee wakuu wa mikoa na wilaya akina mama, wakurugenzi wa mashirika na idara nyeti zote za serikali wawe akina mama.Nashauri Rais wetu mpendwa angepumzika by 2025 baada ya kumaliza utawala wa mpito aje Rais mwengine by 2025/2030.
Kulingana na ukweli kwamba Rais wetu ametoka katika jamii zinazokumbatia Sana mfumo dume hivyo amekuwa akisaidiwa na mawazo ya watu wengine ambao hasa ni wanaume hivyo kuonekana maamuzi mengi anayoyafanya yakiwa hasi analaumiwa yeye.
Urais ni taasisi kweli lakini Rais unatakiwa kuwa na maono yako binafsi mpaka sasa niseme ukweli sijaona falsafa yeyote mpya kutoka kwa Rais wetu zaidi ya kuona mchanganyiko wa utawala wa Kikwete na Magufuli ambao kifalsafa wote walikuwa na utofauti mkubwa.
Sizani Kama ni sahihi kuchukua falsafa za Magufuli na Kikwete kuzichanganya maana falsafa zao zinakinzana pakubwa na haziwezi kukaa katika chungu kimoja.
Unaruhusu Uhuru wa vyombo vya habari na uchaguzi huru uku bado hauna interijensia ya kukamata watekaji na wauaji wa Watanzania wenzetu?
Tanzania tulipofikia tunatakiwa kuwa na Rais ambaye ni game changer ambaye atakuja na falsafa zake zisizofungamana na upande wowote wa Rais asiye madarakani.
Rais ambaye anatengeneza makundi hawezi kufanyakazi na watu wanaomkosoa hatufai.
Rais ambaye bado haonekani kuleta suluhu ya kuwepo kwa katiba na uchaguzi huru na haki.
Nchi Haina future juu ya mambo mengi ya kitaifa Rais Bora ni yule mwenye falsafa inayoeleweka na watu wake.
Hivyo nashauri angepumzika mwakani atakuwa Rais mwenye heshima kubwa Sana kwenye Taifa letu.
Naamini huenda ikatusaidia kusonga mbele na uwizi , ubinafsi na ubadhirifu wa mali ya umma ukapungua kidogo. Nafikiri hata mambo ya ukatili wa kijinsia, ubakaji, na rushwa za ngono zitapungua pia.
Wanaume wameshindwa kuleta maendeleo kwa miaka zaidi ya 50 sasa ,tuwaachie wakinamama nao watuletee mawazo mbadala.