Injinia Hersi Said: Bado tunamsubiri Fei Toto, tunaendelea kumlipa mshahara

Injinia Hersi Said: Bado tunamsubiri Fei Toto, tunaendelea kumlipa mshahara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amezungumza kuwa baada ya Kamati ya Hadhi na Haki za Wachezaji kumtaka Fei Toto kurejea Yanga, mchezaji huyo hajarejea klabuni licha ya kushindwa katika shauri la kuvunja mkataba wake na Yanga.

Amesema baada ya hapo wao wanaendelea kumlipa mshahara na stahiki zake kama kawaida mchezaji huyo licha ya kutokuwepo kamibini.

Amesema “Mchezaji aliomba marejeo (Review) ya maamuzi hayo ambayo yalimepangwa kusikilizwa Februari 27, 2023, tumeandika barua kwenda kwenye Kamati kuomba shauri hilo lisogezwe mbele kwa kuwa tunatarajia kuwa na mechi Februari 26 Nchini Mali.”

Kuhusu kama Yanga bado inamhitaji Fei?
“Hapo kuna mambo mawili, mkataba ni ishu ya taasisi na ni suala la mkataba, Fei ana mkataba na anatakiwa kurudi, kuhusu suala binafsi sisi Fei ni kijana wetu, kuna watu wanaongeza chumvi, ni mchezaji wetu na ataendelea kuwa kwetu hadi Mwaka 2024."

Kama Fei alishawishiwa je?
"Kama Feisal atakuwa ameshawishiwa na mtu, huyo mtu anatakiwa kupigwa vita, soka ina njia zake za kupita, kwa nini uanze kupitia njia ambazo si sahihi, siwezi kumlaumu Fei kama ivyo ndivyo, lakini tunatakiwa kufuata njia."

Chanzo: Clouds FM
 
Mkuu taarifa ya kufungiwa kwa account ya Feisal umepata kwa nani?
Nilisikia wapo Fm kuna kiongozi wa Yanga alikuwa anahojiwa kwa njia ya simu alidai kuwa mchezaji mwenyewe ndiye aliyefunga account
 
Back
Top Bottom