Innocent Bashungwa amejiwekea rekodi ya kupita na kufanya kazi Wizara nyingi sana.Unafikiri sababu ni nini?

Innocent Bashungwa amejiwekea rekodi ya kupita na kufanya kazi Wizara nyingi sana.Unafikiri sababu ni nini?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Katika mabadiliko ya kawaida ya Baraza la Mawaziri yameshuhudia Mheshimiwa Innocent Bashungwa akihamishwa kutoka wizara ya Ujenzi kwenda wizara ya mambo ya ndani.

Hii na hatua hiyo ya kupata uteuzi mpya imemfanya kujiwekea rekodi yake binafsi na kuwa kati ya mawaziri wachache waliopita na kuhudumu katika wizara nyingi zaidi kuliko mtu yeyote yule .

Amebakiza wizara chache sana kuweka rekodi ya Nchi ya kuhudumu kama waziri katika wizara zote hapa Nchini. Sasa anakwenda kuwa waziri katika wizara ambayo imekuwa na mambo mbalimbali ambayo walau ukisikiliza katika vyombo vya habari utaona ikiguswa kila siku.

Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Hii ni kwa kuwa wizara hiyo ya mambo ya ndani inagusa maisha ya watu kila siku katika masuala ya haki.huu ni mtihani mpya kwake na ambao anatakiwa aubebe kwa hekima,busara na utulivu wa hali ya juu sana.

Ni wizara ambayo inataka kabla ya kutamka au kutoa tamko hadharani ufikirie kwanza na kuwa na taarifa za kutosha na zote kiganjani pako.ni wizara ambayo inahitaji kujiridhisha kwa mambo mengi sana Kabla ya kuchukua hatua na maamuzi. Ni wizara inayohitaji sikio la usikivu muda wote pamoja na macho makali ya matukio mbalimbali.

Ni wizara inayohitaji matumizi ya akili nyingi sana kuliko nguvu.inahitaji umakini wa hali ya juu sana kwa kuwa ni wizara ambayo usipokaa sawa unaweza kujikuta unachafuka ,unachukiwa na watu na kuanza kuitwa kila aina ya majina mabaya .inahitaji ngozi ngumu, unyenyekevu na kuondoa kabisa jazba ,hasira na hata haraka ya Mambo.

Hii Ni wizara Mtambuka na inagusa watu moja kwa moja katika masuala mbalimbali.

Swali langu ni kuwa unafikiri ni kwanini Mheshimiwa Innocent Bashungwa amepata Neema ,bahati na kibali mbele ya mamlaka za uteuzi cha kuaminiwa kuhudumu katika wizara mbalimbali? Unafikiri ni kwanini anaendelea kuwekwa kwenye wizara tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti tofauti?

Ngoja niweke kalamu yangu chini mara moja . Lakini nawakumbusha kwa uchache tu kuwa miongoni mwa Wizara alizopita kama waziri kamili kati ya nyingi ni Wizara ya viwanda na Biashara,Wizara ya ulinzi,wizara ya habari , utamaduni michezo na sanaa,wizara ya ujenzi ,wizara ya TAMISEMI na sasa wizara ya mambo ya ndani.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katika mabadiliko ya kawaida ya Baraza la Mawaziri yameshuhudia Mheshimiwa Innocent Bashungwa akihamishwa kutoka wizara ya Ujenzi kwenda wizara ya mambo ya ndani.

Hii na hatua hiyo ya kupata uteuzi mpya imemfanya kujiwekea rekodi yake binafsi na kati ya mawaziri wachache waliopita na kuhudumu katika wizara nyingi zaidi kuliko mtu yeyote yule .

Amebakiza wizara chache sana kuweka rekodi ya Nchi ya kuhudumu kama waziri katika wizara zote hapa Nchini. Sasa anakwenda kubwa waziri katika wizara ambayo imekuwa na mambo mbalimbali ambayo walau ukisikiliza katika vyombo vya habari utaona ikiguswa kila siku.

Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Hii ni kwa kuwa wizara hiyo ya mambo ya ndani inagusa maisha ya watu kila siku katika masuala ya haki.huu ni mtihani mpya kwake na ambao anatakiwa aubebe kwa hekima,busara na utulivu wa hali ya juu sana.

Ni wizara ambayo inataka kabla ya kutamka au kutoa tamko hadharani ufikirie kwanza na kuwa na taarifa za kutosha na zote kiganjani pako.ni wizara ambayo inahitaji kujiridhisha kwa mambo mengi sana Kabla ya kuchukua hatua na maamuzi. Ni wizara inayohitaji sikio la usikivu muda wote pamoja na macho makali ya matukio mbalimbali.

Ni wizara inayohitaji matumizi ya akili nyingi sana kuliko nguvu.inahitaji umakini wa hali ya juu sana kwa kuwa ni wizara ambayo usipokaa sawa unaweza kujikuta unachukuwa na watu na kuanza kuitwa kila aina ya majina.inahitaji ngozi ngumu, unyenyekevu na kuondoa kabisa jazba ,hasira na hata haraka .

Hii Ni wizara Mtambuka na ndio maana inagusa watu moja kwa moja katika masuala mbalimbali.

Swali langu ni kuwa unafikiri ni kwanini Mheshimiwa Innocent Bashungwa amepata Neema ,bahati na kubali mbele ya wateule cha kuaminiwa kuhudumu katika wizara mbalimbali? Unafikiri ni kwanini anaendelea kuwekwa kwenye wizara tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti tofauti?

Ngoja niweke kalamu yangu chini mara moja . Lakini nawakumbusha kwa uchache tu kuwa miongoni mwa Wizara alizopita kama waziri kamili kati ya nyingi ni Wizara ya viwanda na Biashara,Wizara ya ulinzi,wizara ya habari , utamaduni michezo na sanaa,wizara ya ujenzi ,wizara ya TAMISEMI na sasa wizara ya mambo ya ndani.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kila Wizara anayokwenda anaharibu.
 
Back
Top Bottom