Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #41
Kutwa nzima kabla ya giza kuanzaKila siku unabwabwaja humu, hiyo kilimo unafanya saa ngapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kutwa nzima kabla ya giza kuanzaKila siku unabwabwaja humu, hiyo kilimo unafanya saa ngapi?
..r you kidding, alipikwa kuwa Rais?Huyu alipikwa kuwa Rais lakini kwa hiyo Wizara waliyompa ndio Basi tena labda abadilishe Hali ya mambo ya wasiojulikana
Inawezekana Samia kanusa 2025 kaamua kumzika Bashungwa!!
Mara nyinyingi majina ya kwanza hasa ya utotoni unapozaliwa hubeba, (huwakilisha), picha nafsi, self-image, picha nafsi ni tabia ambayo binadamu anaijenga kwa muda mrefu na kuibadilisha huwa ni ngumuSababu ya jina lake la kwanza “Innocent” aliempa hakukosea
Hata mimi nimemuona ni Mzushi tu na mwenye kuleta uongo na umbeya..r you kidding, alipikwa kuwa Rais?
Nani akupe uteuzi Kilaza kama wewe???Mimi Sitafuti uteuzi
Mimi siyo kilaza ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa MawazoNani akupe uteuzi Kilaza kama wewe???
Haitatokea Muhaya/munyambo kuwa president wa nchi hii.Huyu alipikwa kuwa Rais lakini kwa hiyo Wizara waliyompa ndio Basi tena labda abadilishe Hali ya mambo ya wasiojulikana
Inawezekana Samia kanusa 2025 kaamua kumzika Bashungwa!!
Acha ukabilaHaitatokea Muhaya/munyambo kuwa president wa nchi hii.
Tatizo Muhaya /munyambo akipewa uongozi mkuu wa nchi hii ndani ya miaka miwili sekta zote muhimu za kiserikali zitashikwa na watu wa kabila lake na akiulizwa atasema wahaya/ wanyambo wamesoma sana na Wana akili sana sababu wanakula senene wana protin nyingi.Acha ukabila
Humuelewi nini.Huyu jamaa to be honest huwa simuelew
Wamegundua kuna wenye mapepo la kisifia na wameanza kukataa mapepo ya aina hiyoKwahiyo Lucas Mwashambwa kakosa tena teuzi?
Hatakuongea tu awezHumuelewi nini.
Yamkini kasomea uchawa.Ungekuwa umesoma na kupata elimu bora usingekuwa chawa wa kiwango hiki.
Bashungwa huyu awe Rais? Ikulu sio Bar plzNa atakuja kuwa Rais baadae
Kama unataka kuargue kizembe hivi, usingepost hata hiyo thread maana kinachomfanya ahudumu wizara nyingi ni kwa sababu ana sifa ya kuwa waziri, simple!Hana sifa kivipi? Kwani sifa ya uwaziri ni nini?
Kwa sababu mama mkwe anajua kifua cha mkwe wake kilivyo kipanaNdugu zangu Watanzania,
Katika mabadiliko ya kawaida ya Baraza la Mawaziri yameshuhudia Mheshimiwa Innocent Bashungwa akihamishwa kutoka wizara ya Ujenzi kwenda wizara ya mambo ya ndani.
Hii na hatua hiyo ya kupata uteuzi mpya imemfanya kujiwekea rekodi yake binafsi na kuwa kati ya mawaziri wachache waliopita na kuhudumu katika wizara nyingi zaidi kuliko mtu yeyote yule .
Amebakiza wizara chache sana kuweka rekodi ya Nchi ya kuhudumu kama waziri katika wizara zote hapa Nchini. Sasa anakwenda kuwa waziri katika wizara ambayo imekuwa na mambo mbalimbali ambayo walau ukisikiliza katika vyombo vya habari utaona ikiguswa kila siku.
Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais
Hii ni kwa kuwa wizara hiyo ya mambo ya ndani inagusa maisha ya watu kila siku katika masuala ya haki.huu ni mtihani mpya kwake na ambao anatakiwa aubebe kwa hekima,busara na utulivu wa hali ya juu sana.
Ni wizara ambayo inataka kabla ya kutamka au kutoa tamko hadharani ufikirie kwanza na kuwa na taarifa za kutosha na zote kiganjani pako.ni wizara ambayo inahitaji kujiridhisha kwa mambo mengi sana Kabla ya kuchukua hatua na maamuzi. Ni wizara inayohitaji sikio la usikivu muda wote pamoja na macho makali ya matukio mbalimbali.
Ni wizara inayohitaji matumizi ya akili nyingi sana kuliko nguvu.inahitaji umakini wa hali ya juu sana kwa kuwa ni wizara ambayo usipokaa sawa unaweza kujikuta unachafuka ,unachukiwa na watu na kuanza kuitwa kila aina ya majina mabaya .inahitaji ngozi ngumu, unyenyekevu na kuondoa kabisa jazba ,hasira na hata haraka ya Mambo.
Hii Ni wizara Mtambuka na inagusa watu moja kwa moja katika masuala mbalimbali.
Swali langu ni kuwa unafikiri ni kwanini Mheshimiwa Innocent Bashungwa amepata Neema ,bahati na kibali mbele ya mamlaka za uteuzi cha kuaminiwa kuhudumu katika wizara mbalimbali? Unafikiri ni kwanini anaendelea kuwekwa kwenye wizara tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti tofauti?
Ngoja niweke kalamu yangu chini mara moja . Lakini nawakumbusha kwa uchache tu kuwa miongoni mwa Wizara alizopita kama waziri kamili kati ya nyingi ni Wizara ya viwanda na Biashara,Wizara ya ulinzi,wizara ya habari , utamaduni michezo na sanaa,wizara ya ujenzi ,wizara ya TAMISEMI na sasa wizara ya mambo ya ndani.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.