Wizara yake inachangia kwa kiasi kikubwa kusinyaa kwa sekta ya ujenzi (hasa wakandarasi wazawa) malalamiko ya wakandarasi kutolipwa toka mwaka jana ni mengi sana sasa kampuni zinajiendesha vipi kama hawalipwi na kodi watalipa vipi yeye kama waziri amekuwa kimya juu ya hili na hata halisemei. Wizara ikishirikiana na mamlaka za barabara kama Tanroads na Tarura (Tamisemi) mafungu ya mfuko wa barabara (Road fund) wameyapeleka wapi miaka yote pesa hizo huwa zinakuwepo iweje wakati huu wakandarasi walalamike malipo na wengi wamesimamishq miradi kwa kukosa fedha za kuendeshea miradi. Taasisi za fedha nao wanapiga mnada dhamana za wakandarasi waliochukua mikopo kutokana na kutolipa kwa wakati marejesho ya mikopo nafikiri waziri ana safari ndefu ya kujifunza kabla ya kumfikiria kwenye madaraka makubwa