Pre GE2025 Innocent Bashungwa ana sifa zote za kumrithi Samia baada ya 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Acha wasi wasi. Samia 2025 Hana mpinzani lishapita hilo hapa tunamjadili mrithi wake ndugu Inno Bashungwa.
 
Wizara yake inachangia kwa kiasi kikubwa kusinyaa kwa sekta ya ujenzi (hasa wakandarasi wazawa) malalamiko ya wakandarasi kutolipwa toka mwaka jana ni mengi sana sasa kampuni zinajiendesha vipi kama hawalipwi na kodi watalipa vipi yeye kama waziri amekuwa kimya juu ya hili na hata halisemei. Wizara ikishirikiana na mamlaka za barabara kama Tanroads na Tarura (Tamisemi) mafungu ya mfuko wa barabara (Road fund) wameyapeleka wapi miaka yote pesa hizo huwa zinakuwepo iweje wakati huu wakandarasi walalamike malipo na wengi wamesimamishq miradi kwa kukosa fedha za kuendeshea miradi. Taasisi za fedha nao wanapiga mnada dhamana za wakandarasi waliochukua mikopo kutokana na kutolipa kwa wakati marejesho ya mikopo nafikiri waziri ana safari ndefu ya kujifunza kabla ya kumfikiria kwenye madaraka makubwa
 
Yaani sisi tuongozwe na Bijwajwa Munwa
 
hii inasababishwa na mwigulu. pesa wanazizuia zingine wanafanyia ujinga kwaajili ya kuandaa uchaguzi wa kulinda majimbo yao. hivyo ukimulaum unamuonea tangu waziri wa fedha huyu aingie pesa hazijawawi kua na utulivu.madeni yanaongezeka na bado hela zinazokopwa hazijulikani zinakoenda.
 
kwanini
kwaninii ni 2030 na sio 2025??????


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
CCM wao ni kifikiri Urais tu badala ya kuwaletea watu maendeleo.

Watu wanakula mlo mmoja hali ni mbaya wao wanaleta machungwa eti 2030.

Kwanza 2025 Samia mwenyewe tia maji tia maji unga umezidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…