Baada ya watu kuzoea kuona muvi kwa flashi, soko la uhakika la muvi limekuwa gumu kuingia na kupata faida,
Hii imefanya watu wenye fedha kuacha kuinvest kutengeneza muvi, hii inafanya wasanii wazuri, madirector wazuri na hata maproducer kuacha kufanya kazi kwasababu ya ukali wa maisha na kufanya ishu ingine hii ikafanya bongo movie kuwa low quality kuliko za enzi zile za kanumba kipindi watu wako tayari kununua m8kanda na deki walikuwa nazo
Sasa siku hizi kuna platform kama showmax na netflix, shida ya hizi hazifikiki kirahisi na maproducer wa kawaida wa kibongo wasio na pesa ni kama platform za kimagharibi mno na hazilengi maproducer wa Kiafrika na soko letu kwa ujumla, huku platform zetu kama swahiliflix zina changamoto kibao