INSYUKA ni movie bora sana kuwahi kuigizwa na wasanii wa Tanzania haina mpinzani

INSYUKA ni movie bora sana kuwahi kuigizwa na wasanii wa Tanzania haina mpinzani

Ubunifu hakuna kabisa huo ndio ukweli.
Huko kuiga ni sehemu ya kuhaha tu, ukweli ni kuwa bongo movie haina platform ya kuuzia kazi, huo ndio ukweli hakuna platform, toa hela yako tengeneza filamu ya kibongo, hutaona pesa ikirejea hasa pesa ya maana,

Wameishia kutengeneza muvi kwa elfu uamsini ama laki, sasa muvi ya laki moja muvi gani hiyo, star gani anayejua kuigiza atacheza muvi hiyo

Matokeo yake maproducer wanachezesha wasanii wasiojua kuigiza.

Mastaa wote wanaigiza tamthilia siku hizi na sio muvi
 
Girlfriend na Saladini sio za Musa Banzi,Saladini nadhan ni ya July Tax wa Mwanza,Girlfriend ni ya George Tyson ila imetayarishwa na Sultan Tamba.
Hivi yule July Tax aka domo alipoteleaga wapi?
 
Umeeleza vizuri Sana mkuu
Baada ya watu kuzoea kuona muvi kwa flashi, soko la uhakika la muvi limekuwa gumu kuingia na kupata faida,

Hii imefanya watu wenye fedha kuacha kuinvest kutengeneza muvi, hii inafanya wasanii wazuri, madirector wazuri na hata maproducer kuacha kufanya kazi kwasababu ya ukali wa maisha na kufanya ishu ingine hii ikafanya bongo movie kuwa low quality kuliko za enzi zile za kanumba kipindi watu wako tayari kununua m8kanda na deki walikuwa nazo


Sasa siku hizi kuna platform kama showmax na netflix, shida ya hizi hazifikiki kirahisi na maproducer wa kawaida wa kibongo wasio na pesa ni kama platform za kimagharibi mno na hazilengi maproducer wa Kiafrika na soko letu kwa ujumla, huku platform zetu kama swahiliflix zina changamoto kibao
 
iLifanya nisilale miaka ile. Girlfriend as well kina TID na AY.
 
Nakumbuka tuliangaalia hii movie jion, kufika usik kila mtu anaogopa kwenda chumban kulala..! Tulilala hatujazima taa mpk asubuh 😂😂
 
Back
Top Bottom