Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,160
- 9,151
Paul Rusesabina aliyecheza filamu maarufu inayoelezea mauwaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 ambapo yeye alikua Manager wa Hotel akiwaokoa Watutsi wasivamiwe na kuchinjwa na Interahamwe hatimaye amefikishwa mbele ya sheria kwa makosa ya kuhusika na njama za mauji hayo hayo!!
Baada ya Rusesabagina kucheza filamu ile wakati wote dunia ilimuona kama shujaa aliyesaidia kuokoa maisha ya makumi ya Watutsi wasio na hatia waliokimbilia Hotel Rwanda hadi pale uchunguzi ulipofanyika na kugundua naye alikua mmoja wa walioshiriki kutekeleza genocide ile. Suala kama ana hatia au la mahakama itaamua lakini kilichoacha watu midomo wazi ni namna alivyofikishwa Rwanda, maana alikua akiishi Ubelgiji na alishachukua urai wa huko.
Inasemekana alikua Dubai na alidanganywa kupanda ndege ambayo labda aliamini inaenda sehemu nyingine. Kuja kutahamaki anajikuta anashuka Kigali Airport na pingu zikimsubiri!!!. Kabda ya hapo kuna jamaa wa Kinyarwanda aliandika makala akisema alijipa jukumu la kufuatilia nyendo za Rusesabagina duniani kote na alifanya hivyo kwa miaka 15 na kwa kukamatwa kwa Paul Rusesabagina basi ametimiza kazi yake akiwa kama Mzalendo wa nchi yake! Maofisa wa Rwanda wanasema jamaa amerudi mwenyewe kwa hiyari yake jambo ambalo ndugu wanalikanusha wakidai kua ametekwa, na sababu ni kwamba alianza harakati za kumuondoa madarakani Rais Kagame kwa kuongoza kundi la FNL ambalo Kigali inasema ni lakigaidi
Serikali ya rais PK kama alivyo yeye mwenyewe ina mkono mrefu na wanamsemo wao kua "There is a price to pay in betraying Rwanda" na kwamba hicho ndio kilichomkuta mcheza filamu/mwanasiasa Paul Rusesabagina
Amewakosea nini mpaka mhangaike naye hivyo? Kila Lenye mwanzo lina mwisho. Poleni sana mnaohangaika na mambo ambayo hayana umuhimu wowote.