Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

Serikali ya Rwanda inadai kuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka ya kuhusika na genocide
Kwani mkuu hakunaga ushahidi na mashahidi wa kupikwa?

Miaka yote hadi anapewa 'tuzo ya ukombozi', hatujawahi sikia tuhuma ya mauaji dhidi yake.

Yamezushwa tu alipoonesha nia ya kugombea madaraka na kumpinga PK!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka Binti mmoja mfanyabiashara wa Kitutsi kijana sana (jina limenitoka) alitangaza nia ya kugombea Urais lakini ndoto yake haikutimia kwani alikamatwa yeye na mama yake kwa makosa ya ukwepaji kodi kwenye kiwanda chao walichoachiwa na marehemu baba yao

Pia kuna Mwanamama wa Kihutu anaitwa Victoire Ingambire naye alirudi Rwanda kutokea nje ya nchi hiyo kwa ajili ya kugombea Urais pia akashtakiwa kwa makosa ya uhaini. Aliachiwa baada ya kukaa jela miaka kadhaa

Je ni kweli inawezekana watu wanakua na makosa yao mengi ya jinai ndipo wanataka kujiingiza kwenye siasa washinde kiti cha Urais wafiche madhambi yao au kuna uonevu tu? Lakini kama ni uonevu ni kwa kila mwenye kuonesha nia ya kugombea Urais?
 
Mkuu uzi wako unachanganya sana,sababu hata hiyo hotel haikuitwa hotel Rwanda.Nadhan tatizo umechanganya mambo ya kwenye movie na facts.
 
Mkuu uzi wako unachanganya sana,sababu hata hiyo hotel haikuitwa hotel Rwanda.Nadhan tatizo umechanganya mambo ya kwenye movie na facts.
Ndio Mkuu, movie iliitwa Hotel Rwanda lakini kiuhalisia ni Hotel Des Mille Collines. Mambo mengi nimesahau maana masiku nayo yamekua mengi. Ila uhalisia ni kwamba Rusesabagina ambaye wote tukidhani ni shujaa aliyewaokoa watu wasiuwawe na Intrehamwe sasa na yeye anatuhumiwa kwa ugaidi na yupo Rwanda baada ya kurudi katika njia ya kutatanisha
 
Kwani mkuu hakunaga ushahidi na mashahidi wa kupikwa?

Miaka yote hadi anapewa 'tuzo ya ukombozi', hatujawahi sikia tuhuma ya mauaji dhidi yake.

Yamezushwa tu alipoonesha nia ya kugombea madaraka na kumpinga PK!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena ndugu zake wametoa taarifa kwamba wamegundua Wakili anayemuakilisha yupo kwenye jopo la waendesha mashtaka wanao prosecute case yake!
 
Ndiyo hasa niliotaka kuwaelezea, lakini nikawa sina details za majina yao, shukrani mkuu kwa kuweka kumbukumbu sawa.

Huyo rais ndiyo zake kuzushia mabalaa watu wanaompinga ama kutofautiana naye kimawazo.

Kuna mwanajeshi mwingine pia, kama sikosei alikuwa ni 'director' wa intelligency walipishana kauli akakimbilia SA, mbona alifuatwa kuchinjiwa huko huko?

Hao tunaowafahamu ni wachache, lakini wengi wanaoata misukosuko wanapoinesha nia za upinzani.

Kwa hiyo raia anayetofautiana na watawala, kuzushiwa kesi ni kawaidana ni rahisi sana hasa nchi zetu za kiAfrika.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila tukitoka nje ya mada wazee, huyo muigizaji Don C ni nguli ki noma.

Filamu ya Hotel Rwanda ukianza kuiangalia, ni lazima utaing'ang'ania bila ya kupepesa macho kwingine hadi mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa Mkuu, wenzetu wametuacha sana kwenye kila fani. Unajua hata ile 'This time in April' aliyocheza Idris Elba nayo ni kiwango na yenye kukuweka roho juu wakati wote
 

Jamaa pia ameishi Marekani na Afrika Kusini na aka-settle Ubelgiji.

Tatizo hakusoma alama za nyakati na zile safari zake za kutoa lecture kwenye mavyuo mbalimbali duniani.

Hizo lectures zake zilionekana kama vile zapindisha ukweli halisi.

Sasa hawa mazee wa RIB walikuwa na kazi moja tu, ya kusoma uzuri zile dots za kuunganisha pale Dubai.
 
Hii ime confuse watu wengi sana. Hata ndugu hawajui ilikuaje. Wanajua tu hakurudi kwa hiyari.

Kama "international transit hub", Dubai pana dawati kabisa kwa ajili ya vyombo kama Interpol.

Pia,kulikuwa na International Warrant ilotolewa na Rwanda ambayo inaruhusu kuingilia safari ya anaetafutwa.
 
Je, shutuma anazo shutumiwa ni za kweli au ni vile anampinga kiongozi aliyepo madarakani?
Waafrika tuna shida sana kwenye kubadilishana uongozi.

Baadhi ya alokuwa akiwahifadhi ndo wamekuwa wakipinga yale anayoyahubiri kwenye mihadhara na kwenye kitabu alichoandika.

Kuna madai mengine mengi tu ambayo itabidi yawasilishwe mahakamani.
 
All empires are built on blood (Pablo Escobar). But ushauri wangu kwa Rwanda na wanyaruanda tu waanze kufikiria the after Kagame, hatutaki kuona mauaji mengine au kupokea wakimbizi tena. A smooth transition inastahili kuanza kufirikiwa before it is too late. Power vacuum huwa ni mbaya especially when there are many power mongers. Mungu ibariki Africa
 
Hii ishu ina siri kubwa, Siku zote ukimpinga PK lazima akutafute popote ulipo ndicho kilichotokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…