Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

Umaru Diko,alikua waziri wa mafuta na usafirishaji,aliiba dola bilioni moja
Jenerali katili kuwahi kutokea Sani Abacha,alituma makachero,wakamteka wakamtia katika sanduku ,wakaandika kuwa ni mzigo wa kidiplomasia
Kilichomuokoa airport alipiga chafya kama tatu mfululizo kwa jili ya dawa za usingizi zilikua zinaisha nguvu,wazungu wakasema fungua mzigo msitutanie!
Dah! Kumbe ilikua ni wakati wa Abacha The Butcher!? Ila Wanigeria tangia enzi hizo wanaiibia nchi yao hatariiii
 
1. Kwa taarifa za sasa, alikuwa safarini, 27 Agosti alikuwa Dubai na aliwasiliana na familia yake.

2. Alipanda ndege binafsi "private jet" iliyokuwa inaelekea mojawapo ya nchi iliyopo Afrika ya Kati. (Hapa ndio kwenye utata)

3. Ndege ilitua Kigali na akawekwa chini ya ulinzi.
Mkuu, kwa maelezo hayo basi akili kubwa sana ilitumika
 
Hii Serikali ya Rwanda ni tata sana. Jamaa yangu mmoja (Mnyarwanda) anaiponda sana, lakini ukichat naye WhatsApp au fb utashangaa anavyoitetea. Kama utataka muongee akiwa huru inabidi utumie mitandao mingine ya kijamii kama WeChat (ambayo ni less popular).
Jamaa wangu mmoja tulikua nae kule neng'ung aliniambia pia hili swala

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
1. Kwa taarifa za sasa, alikuwa safarini, 27 Agosti alikuwa Dubai na aliwasiliana na familia yake.

2. Alipanda ndege binafsi "private jet" iliyokuwa inaelekea mojawapo ya nchi iliyopo Afrika ya Kati. (Hapa ndio kwenye utata)

3. Ndege ilitua Kigali na akawekwa chini ya ulinzi.
Huyo jamaa atakuwa na pesa nying kukodi private jet sio mchezo
 
Umaru Diko,alikua waziri wa mafuta na usafirishaji,aliiba dola bilioni moja
Jenerali katili kuwahi kutokea Sani Abacha,alituma makachero,wakamteka wakamtia katika sanduku ,wakaandika kuwa ni mzigo wa kidiplomasia
Kilichomuokoa airport alipiga chafya kama tatu mfululizo kwa jili ya dawa za usingizi zilikua zinaisha nguvu,wazungu wakasema fungua mzigo msitutanie!

Rais wa kipindi hicho wkt Dikko anatekwa huko uingereza alikua ni huyu huyu wa sasa Gen. Buhari aliyeitawala Nigeria kuanzia 1983-85 na sio Sani Abacha.
 
Huyo kagame mna mu overate tu, siku akileta upuuzi wake bongoland aka Mongolia hakuna rangi wataacha kuiona ndani ya dk kadhaa kigali itakuwa haina mtu

Labda panya na paka tu watakao kuwa wanaranda randa mitaani na masokoni
Inawezekana militarily Tanzania is far superior to Rwanda lakini vita siku hizi ipo katika fronts nyingi sana mfano kiuchumi, biashara, ki intelijensia, sayansi na teknolojia n.k
 
1. Kwa taarifa za sasa, alikuwa safarini, 27 Agosti alikuwa Dubai na aliwasiliana na familia yake.

2. Alipanda ndege binafsi "private jet" iliyokuwa inaelekea mojawapo ya nchi iliyopo Afrika ya Kati. (Hapa ndio kwenye utata)

3. Ndege ilitua Kigali na akawekwa chini ya ulinzi.
Asante sana mkuu,Lkn mzee baba hapo hapo Private Jet iliyombeba huyo jamaa inamilikiwa na serikali ya PK.

Sasa hapo sijui aliingiaje humo.
 
Na mim
Rais wa kipindi hicho wkt Dikko anatekwa huko uingereza alikua ni huyu huyu wa sasa Gen. Buhari aliyeitawala Nigeria kuanzia 1983-85 na sio Sani Abacha.
Namimi nahisi kumbukumbu zangu zinaniambia ilikua ni kwenye 80s. Huyu Buhari anawafuatilia sana Wanigeria walioweka pesa za kifisadi nje ya nchi yao. Hata kipindi alivyorudi tena madarakani kaenda kuomba Wazungu warudishe Nigeria mabilioni ya dola yaliyopo kwe ye ma bank ya Ulaya. Sijui kama kafanikiwa
 
Kivyovyote vile wakitia pua tu wanapotea
Niliwahi kusikia umbeya na naomba radhi in advance kuuweka hapa maana siwezi kuthibitisha, kwamba kuna nchi fulani iliyopo Afrika Mashariki na Kati eti kikosi cha kumlinda Kiongozi wa nchi hiyo kimetoka Rwanda. Wenyewe wanakiita Presidential Security Unit.....narudia tena haya ni maneno ya kuambiwa na siwezi kuthibitisha popote
 
Wazungu wakampa uraia, akapewa tuzo nyingi kama shujaa kumbe naye ailikuwa "mdhamini" wa mauaji na msaliti wa nchi yake! (Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu jamaa hasa pale unapoona kiongozi anapewa support kubwa na mataifa ya magharibi na Marekani) Ingekuwa Tanzania Paul Rusesabagina angekuwa kiongozi wa chama cha siasa au NGO ya kutetea Haki za raia, na hata urais angegombea tu, ila kwa Rwanda ukiisaliti nchi na kuwatumikia "mabeberu" lazima wakuwinde tu!
View attachment 1568411
Ninadhani kuna kitu haukielewi sawasawa kuhusu siasa za ndani ya Rwanda.

Mtu yeyote anayempinga ama kumkosoa rais Paulo Kagame hubatizwa jina la 'adui wa taifa' awe ndani ama nje ya nchi.

Unapompinga Kagame hata kwa mfano wa upinzani wa kisiasa unaofanywa nchini kwetu, elewa unarisk maisha na mustakabali wako wa uraia kwa ujumla.

Uchaguzi uliopita Rwanda, kuna mama mmoja chama cha upinzani, ile kuonesha nia ya kugombea urais tu, kazushiwa kesi nzito nzito zisizoisha, mpaka leo sijui aliyamalizaje!

Kwa hiyo huyo mtu, usiamini moja kwa moja kwamba ni 'haini' ama muuaji wa kimbari, hizo bado ni tuhuma tu.

Tusubiri tuone kwanza udadavuzi wa kisheria utakavyokuwa mahakamani, maana kashitakiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very true.
Mauaji ya watusi yalifanywa out of panick, frustration and anger. Ni reaction baada ya Rais wao kuuliwa tena na kikundi kidogo cha kina Kagame wakisaidiwa na Marekani. Kwa hiyo ni sahihi kusema Kagame ndiyo chanzo cha genocide baada ya kumuua Rais.
Mjomba hapo umechemka katafute vitabu Kama vitano vya waandishi tofauti ndipo uje kuongea source ya mauaji ya Rwanda sio rahisi Kama ULIVYO koment
 
Back
Top Bottom