International School, watoto hutafuta vitu vitatu tu

Hawa Leopard Tours huwa wana adopt watoto? Inaruhusiwa makampuni ku-adopt kumbe!
 
Ukweli ni huu alioandika huyu bwana aliueleta huu Uzi.

Mie nimesoma shule za kawaida za serikali nimeona kweli kabisa connection uliyonayo ni Ile ya wasongolist yaani unasoma ndio upate maksi za juu ili uendelee na chuo.

Unaingia chuo kikuu upo serious na masomo yani hata mademu unaona wanakupotezea muda.

Haupati muda wa kusocialize kama kwenda club, kukaa na jinsia tofauti just kupiga mastori tu, kupata exposure na watu tofauti unaona Kama inapoteza muda na unahisi ukifeli ndio life imeisha.

Unakuja kumaliza chuo hapo ndio kuja kuelewa nilipaswa pia kusocialize maana unakutana na wenzio wameanza kazi nzuri Wana magari nk halafu haikuwa karibu nao inakuwa ngumu kuanza kujipendekeza mtu anakusalimia kama schoolmate Ila sio Kama a friend.

Hii niliikataa na nikajisemea nitasomesha watoto wangu kwenye shule zenye watoto wa mataniri hata kama ni middle class lakini iwe nzuri.

What I can say, uliza shule inaitwa ROYAL ELITE SCHOOLS ipo mbezi beach nimeweka wanangu watatu pale mmoja last born ameanza mwaka huu Ada ni kubwa kiasi Ila naona watoto wanaosoma pale ni tofauti wandugu.

Kuanzia chakula Hadi elimu ni Safi kabisa na siku ya wazazi ukienda unaona kabisa parking imejaa gari za aina gani unajikuta unapaki Rav 4 yako pembeni unajisemea mwanangu aoe hawahawa.

Mnachotaka kusema kampani aliyonayo pale nina uhakika tukichanganya na malezi mazuri ya home basi vijana watapata malezi, kampani na marafiki Bora sana na hii huchangia kwa asilimia kubwa mafanikio kwenye maisha.
 
Ada bei gani Mkuu?
 
Umenichekesha Sana Mkuu, eti unasema mtu anakusalimia Kama schoolmate na sio Kama rafikiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ halafu Sasa unatamani ujenge urafiki halafu it's too late.
 
Hakuna kanuni katika maisha ndugu
 
Umenichekesha Sana Mkuu, eti unasema mtu anakusalimia Kama schoolmate na sio Kama rafikiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ halafu Sasa unatamani ujenge urafiki halafu it's too late.
Too late braza πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ Yani anakupa Hi halafu hakuulizi unafanya kazi wapi au kama ni ofisini kwao hata hakuulizi una ishu gani akusevu πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Utasikia aisee long time, halafu anatamasamu then anakuambia aisee tupo tunapambana huku anasepa πŸ˜ƒ
 
Kwa kifupi ni kwamba jamaa amekudharau.
 
Kwa kifupi ni kwamba jamaa amekudharau.
Anaona huyu wakumwitu hata akisema akuite Havoc utaanza kushangaa bia efu sita wakati labda yeye ndio Amelia akinywa mitaa hiyo.

Kimsingi hamuendani. We unapiga story ya kufuga mbuzi yeye anapiga story ya kununua nyumba aiweke kwenye BnB renting na masuala ya kununua gari ya watalii.
 
ume overate sana hizi shule... Kubwa katika shule hizi ni ile IB... Kutumia mtaala wa kimataifa na hata mtoto wa international professional akihama nchi moja hana shida kupata shule anakoenda .. Mfano anatoka Tanzania anahamia Indonesia ipo tena shule kama hii.

Asilimia kubwa wanaosoma hapa ni watoto wa international NGO/ Embassies/ Bank and other international jobs... Si watoto wa wafanya biashara .. Ingawa watoto wa wafanya biashara wapo...

Hivyo swala la networking halipo pale. Kwanza wote ni wanafunzi ... Halafu hawakutani tena maishani .. Ile ni shule kwa mtaala wa kimataifa .... Sio networking school.

Hayo mengine ya exposure na confidence ipo mahali popote kwenye mazingira mazuri ...Hata kupitia makanisa na platform mbalimbali
 
Tutafute mpunga ikiwezekana vitukuu zetu waje kuskonga kwenye hizo shule...
 
Haya maisha haya nyie yaoneni tu Yana mengi sana!!!kikubwa juhudi tu mkuu!!unaodhani wenye Maisha mazuri wote Wana hayo???bahatihupata yeyote Yule!!
 
Tafuta pia Shule inaitwa SUN RAY ni ya Wazungu flan Ipo ADA ESTATE mtaala ni NECTA lakini wanachanganya na Cambridge hasa kwa masomo ya Lugha na Hesabu,wao darasa moja halizidi watoto 30,ina competition kali sana lakini mtoto akipata pale hizo Connection unazozitaka mbona utazipata tu,hasa kwenye hiyo mikutano ya Wazazi,utakutana na wanaokula keki ya Taifa wa kutosha.Lakini ada yao ipo juu kidogo ya ROYAL ELITE.
 
Hiz
Hao 2 kwa 10 lakini wengi awatupani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…