Kuna mambo ambayo wazazi na walimu huwa hawazingatii kutoka kwa watoto hasa katika mchakato mzima wa mtoto kupata elimu.
Pasipo kufahamu haya madogo ndio makubwa zaidi katika kumjenga mtoto kiuelewa ambapo itakuwa ni msaada mkubwa sana kwake katika maisha yake yote yaliyobaki kitaaluma, kazini na hata katika utu uzima wake baadae.
International schools ni zaidi ya english na masomo haya ya kawaida wanayosoma English Medium na kayumba.
Mambo madogo madogo ambayo hizi shule za kawaida hawazingatii kule international schools wanazingatia.
Katika kitu ambacho nili notice binafsi.
Uwezo tu wa kujiamini wa mtoto anayesoma International school ni next level, mtoto anafundishwa confidence ya hali ya juu anaweza kusimama mbele ya watu 1000 na akazungumza kwa kujiamini sana, na sio hawa watoto wa kayumba akiona mwalimu ni mbio na hajui hata anakimbia nini, ye anawaza fimbo tu, hio ni mbaya, mwalimu na mtoto ni maadui hapo saa 4 wapo wanapiga maembe na mawe kazi kweli kweli.
usizungumzie ubora wa elimu ya michezo na viwanja vya michezo, ubora wa maabara, computer room, maktaba hadi madarasa, vyakula n.k. plus watoto wanapewa care ya hali ya juu mfano uende 5 star hotel na kwa mama ntilie mtaani, mtoto anajiona special na wa thamani, haya ni mambo yanamjenga sana mtoto kisaikolojia.
Ukweli ni kwamba kila mmoja anatamani mwanae asome international ni ile tu uchumi hauruhusu.
Nadhani umaskini hasa wa fikra unaleta makasiriko sana kwenye maisha , maana mleta mada hata kwa swali lake tayari ameshaonyesha bias . Anyways - hakuna formula kuwa aliyesoma NECTA Vs aliyesoma International schools ni lazima mmoja awe bora au asiwe bora. Kuna factora nyingi sana - na tumeona wengi wamesoma NECTA na wamefanya vyema , HOWEVER tunajua mazingira wezeshi na mtaala na walimu na walezi wana mchango mkubwa sana katika kutengeneza fikra za mwanafunzi akawa tayari kupambana na maisha , soko la ajira, misukosuko ya biashara nk. Kwanza tuelewe shule za kimataifa ni zipi? na shule zinazofundisha kwa Kiingereza ni zipi , na swali lake ni lipi? Nadhani anamaanisha
Shule ya kimataifa ni taasisi za elimu zinazotoa mtaala ulioundwa na kuidhinishwa kwa kiwango cha kimataifa, mara nyingi kwa lengo la kuwafundisha wanafunzi kutoka nchi mbalimbali na kuwaandaa kwa maisha ya kidunia. Shule hizi zinaweza kufuata programu za kielimu kama vile International Baccalaureate (IB), Cambridge International Examinations, au American Advanced Placement (AP), ambazo zinatambulika na kuheshimika kote duniani.
Shule za kimataifa zina manufaa mengi ambayo yanazidi yale ya vifaa vya kawaida vya darasani. Zinawaandaa wanafunzi kwa masoko ya kimataifa kwa kusisitiza kufikiri kwa kina, ujuzi wa kutatua matatizo, na uelewa wa tamaduni tofauti- mwanafunzi hafungwi katika mtazamo wa jamii yake pekee , kusoma na kuishi na tamaduni nyingi kunampanua mawazo.
Mitaala ya kimataifa: Shule nyingi za kimataifa hufuata mitaala inayotambulika kimataifa kama vile International Baccalaureate (IB) au Cambridge International Examinations, ambayo ni ngumu na inaheshimika duniani kote. Basi patatokea wabishi ooh wanafundishwa kuwa vibaraka wa wazungu, labda ndio labda sio ila kwa waliosoma hesabu kuna somo la probability- kuwa aliyekuwa na mtaala wa kimataifa ana nafasi kubwa sana ya kupambana na vijana wengi soko la kimataifa, ana nafasi kubwa kupata scholarship nk .
Uwezo wa Lugha: Ingawa kujifunza lugha ni sehemu ya uzoefu, lengo kuu ni ujuzi wa mawasiliano wa lugha nyingi, ambao ni muhimu sana katika dunia iliyo na muingiliano mkubwa. Bado watatokea wabishi na kukataa (wanaruhusiwa), binafsi nilikuwa na ubishi huu huu , nimesoma NECTA ila naona tabu katika matumizi la lugha nikilinganisha na wengine waliweza kuwa na lugha nyingi- kumbuka hata wengi wetu Kiswahili fasaha kujieleza na kukitumia pia ni changamoto.
Kufikiri kwa Kina na Kutatua Matatizo: Mbinu ya kielimu katika shule za kimataifa mara nyingi husisitiza kujifunza kwa kuuliza maswali, hivyo kuwahamasisha wanafunzi kufikiri kwa kina na kutatua matatizo kwa ubunifu. Tunaona leo , wengi tumekuzwa kwa hofu kuuliza maswali hata kwa walezi, jamii tunaona ni dhambi tumeondolewa kujiamini inapekea kuonewa , kunyanyaswa na kupata misongo ya akili - root cause ni malezi, elimu , dini , mitazamo nk , keyword mojawapo hapa ELIMU
Uwezo wa Kitamaduni: Wanafunzi wanajifunza jinsi ya kuelewa na kuheshimu kanuni na desturi tofauti za kitamaduni, jambo ambalo ni muhimu kwa mafanikio katika jamii iliyo na mchanganyiko wa watu kutoka tamaduni mbalimbali. Watu wameelezea kuwa shule za kimataifa zina mashoga wengi , pengine sina takwimu ila fuatilia vyombo vya habari na chunguza idadi ya shule zetu za kayumba nini kinaendelea , sikiliza vyombo vya habari idadi ya ulawiti , unyanyasaji wa kingono kwa ngazi za familia, jamii, ndugu nk- fuatilia idadi ya mashoga na matumizi ya bangi shule za kata ni hali mbaya . Kubwa ni je elimu imewatengeneza kuchambua lipi bora na lipi si bora katika tamaduni mbalimbali?
Michezo na ujuzi wa maisha: Kuna mengi kama muziki, kuogelea , michezo ambayo bahati mbaya shule zetu hazina miundo mbinu yetu haijawa nazo- siku hizi elimu pekee haitoshi , michezo hujenga uwezo wa kufikiri, na shule hizi humfunza mtoto mengi. Huendi camp wanajifunza hata kujenga vifaa kwa vitendo . Bado utasema mbona hawajui kufua - si dunia inaenda kwenye automation pana mashine, pana vifaa vya kutendea kazi kwa hiyo tujikite mtoto afue au mtoto ajue skills zote
Fursa za Zaidi ya Masomo: Shughuli nyingi za ziada zinawaruhusu wanafunzi kuchunguza maslahi na vipaji vyao, hivyo kukuza elimu iliyo kamili. Msomi wetu nguli Professor Mhongo ametuletea takwimu za kazi na masomo yanayohitakija duniani kwa sasa kama artifical intelligence, machine learning, data science, automation , blockchain technologies - swali ni je vijana wetu wako tayari kwa elimu yetu kupata fursa zaidi kwa hali hii?
Kuwa na mawazo wazi ni muhimu. Badala ya kuwa na hasi dhidi ya wale wanaohudhuria shule za kimataifa, tunapaswa kukubali uzoefu wao wa kipekee na akili kubwa wanazozikuza. Wanafunzi hawa mara nyingi wako tayari zaidi kukabiliana na changamoto za kimataifa na kuchangia kwa maana katika jamii. Bei ni kubwa ila tuwa celebrate wanaoweza - nilikuwa kama wewe mdau nikiona mtu anasomesha watoto wake shule bora naona anaringa, anawaharibu , anachezea pesa , ni kibaraka - ila nilipokutana na hawa watoto kazini nikaanza kubadili mtazamo na wengi hawana makasiriko kama sisi - wako open sana kutusaidia wakati sisi tumejikita kuhukumu, kusikitika na kuhuzunika mafanikio ya wengine. Yani njoo na hoja na mihemuko lakini ukweli utabaki pale pale . Haitoi hoja kuwa wengi wa NECTA wanafanikiwa pia , ila ni kwa msuli sana. Una ruksa kuchukia ila tujenge tabia ya kufuatilia kwa undani na kunchunguza kabla ya kulaumu maana tunaonekana hata hatuelewi nini kinaendelea huko duniani.
Blessings !!