Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

Ngoja nitoe ushuhuda..

Kipindi flani hivi kulikuwa na Vitonga viwili(kabla havijapigwa pini) nilikuwa nakimbiza balaa masaa 24 kama nimeweka bando bila kukwamakwama ila nilichogundua ni kweli Vpn zinaharibu betri kwani betri chaji inaisha chap nikiperuzi kwa Vpn tofauti na Data ya kawaida kama una simu bomu tegemea betri kuisha haraka sana.

Baada ya kupigwa Pin Vpn ninazo tegemea na kurudi uraiani nimeona mabadiliko kidogo kwenye simu kwenye kukaa na chaji tofauti na zamani japo mimi mwenyewe nina matumizi mengi ila Vpn inalichangia kea kiasi fulani japo sio kwa kiwango kama kikubwa kama uzi ulivyoeleza.
Tatizo lenu ni kuto kuset simu vizuri vpn ipo kama 2g tu hakuna uhusiano wowote na kuchemka simu wala kufa betri na sababu tunazijua
 
Soma alicho sema ...kasema kazima data voda maana yake raini yake ya voda ndiyo ilikuwa na data...hivyo akazima data voda na kuwasha halotel data ka hivo vpn ndiyo ikakubali
Ntaijaribia kwa simu ya mama watoto nikirudi jioni, mi sina halotel kwa sasa.
 
Wewe ulicho takiwa kutuambia ni kati ya hizo huduma ulizo tumia ni ipi inafanya vizuri zaidi hapo tungekuona una akili timamu .....pia ulitakiwa kuwajulisha wana JF kuhusu hizo huduma ili nao wazijue na kuzitumia kisha walete mrejesho wa kuchemka simu hapo ungekuwa umepata hakika ya sababu ya simu yako kuchemka na kutokukaa na chaji
Tafuta lain ya TTCL, ingia playstore, download Wire Tun, baada ya hapo, hakikisha laini yako imeisha bando au haina bando kabisa, washa data hivyo hivyo! kisha fungua app ya wire turn, chini ya app kuna bar imeandikwa server list, bofya hapo, chagua moja kati ya server hizi Canada2, US 4, UK2, France2 lakini hiyo server ya kwanza na ya pili ni nzuri zaidi! Ikiwa inafika mida ya saa 10 jioni hadi saa 4 usiku utaingia YouTube, tiktok, likee, tsapp na instagram! Muda mwingine tumia kwenye facebook, tsapp, jamiiforums, Quora na chrome!

Ili kuongezewa muda uwe unawatch ads kwenye app yao, kila ad utapewa 30 min za kuperuzi! Tumia uwezavyo!

Baada ya wiki mbili urudi hapa tusaidizane kukuza huu uzi, lakini kwa msaada zaidi, wakati unafanya huu ujinga, hakikisha unaandaa na powerbank kwa ajili ya dharura siku kadhaa zijazo, pia hakikisha unatembea na USB Cable kwenye wallet yako!
 
Kwangu haikubali bila kuwasha data
Sasa itakubali vipi bila ya kuwasha data [emoji856][emoji856][emoji856][emoji856]data ni tofauti na bando ...washa data bila ya bando kisha washa vpn ..ngoma inakonecti
 
Hello wanajamii forums,

Ni wiki kama mbili sasa tokea kutumia zile apps za wire tun, Thor VPN na HA Tunnel zinazotoa huduma ya free internet kutoka servers za mbali kama vile UK, US, German e.t.c

Simu yangu iliyotoka kiwandani ikiwa na 6000 mAh, ambayo ilimaliza siku 3 pasipo kuchajiwa kwa matumizi ya kawaida pasi na kuwasha data, au masaa 40 kama nitaacha data on! Sasa imegeuka nahisi si zaidi ya 1400 mAh. Mwanzoni wakati naanza kutumia hizo huduma, simu ilichemka kuliko kawaida, kuna wakati niliiweka kwenye friji ili ipunguze joto, maake nilihisi ingelilipuka. Nimetumia kwa muda sasa kiasi kwamba simu ilichukua masaa sita tu kuwa na chaji. Ndipo nilipoamua kufuta app hizo! Mbali na kuchukua hatua hiyo, simu yangu inatunza chaji kwa muda wa masaa nane tu, niwashe data, nisiwashe data, niitumie, iwe screen off, niizime, nisiizime! Haya yote yamekuwa bure! Masaa nane tu ndio yaliyobaki kuniweka hewani! Vya bure vimeniponza!
Mnapenda vya bure nyie watu!
 
Niliwahi ku comment humu! Simu inachemka balaa ukitumia VPN , halafu chaji inaisha fasta.sasa hiyo hali ikiwa kila siku lazima betri libabuke.

Ngoja aje chief mkwawa atupe maarifa zaidi.
Screenshot_20220820-102734.jpg
 
Joto ni adui mkubwa nambari moja wa lithium battery

Kama ilikuwa inachemka sana labda ni tatizo

Na kwann ichemke ikitumia hizo app? Ni simu aina gani hio..yenye 6000mah bila shaka ni kutoka wanzuu

Maana brand nyingi kwa sasa hazina hio zina 4000 to 5000
Mkuu, jaribu kuwauliza google kuwa infinix hot 10i zina uwezo upi kwenye battery, ukikuta ni 6000 mAh rudi hapa uweke like, kisha upita kimyakimya wanaozijua simu wasije kukucheka!
 
Nimetumia hizo wire turn, thor etc lakini nilikuja kuona naichosha tu simu yangu maana zina run background, network bandwidth ndogo, slow internet connection mwishowe simu ina struggle sana ku access internet inaishia kupata moto kuliko kawaida yake. Kwanini maisha ya betri yasipungue!
 
Back
Top Bottom