Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

Tatizo lenu ni kuto kuset simu vizuri vpn ipo kama 2g tu hakuna uhusiano wowote na kuchemka simu wala kufa betri na sababu tunazijua
 
Soma alicho sema ...kasema kazima data voda maana yake raini yake ya voda ndiyo ilikuwa na data...hivyo akazima data voda na kuwasha halotel data ka hivo vpn ndiyo ikakubali
Ntaijaribia kwa simu ya mama watoto nikirudi jioni, mi sina halotel kwa sasa.
 
Tafuta lain ya TTCL, ingia playstore, download Wire Tun, baada ya hapo, hakikisha laini yako imeisha bando au haina bando kabisa, washa data hivyo hivyo! kisha fungua app ya wire turn, chini ya app kuna bar imeandikwa server list, bofya hapo, chagua moja kati ya server hizi Canada2, US 4, UK2, France2 lakini hiyo server ya kwanza na ya pili ni nzuri zaidi! Ikiwa inafika mida ya saa 10 jioni hadi saa 4 usiku utaingia YouTube, tiktok, likee, tsapp na instagram! Muda mwingine tumia kwenye facebook, tsapp, jamiiforums, Quora na chrome!

Ili kuongezewa muda uwe unawatch ads kwenye app yao, kila ad utapewa 30 min za kuperuzi! Tumia uwezavyo!

Baada ya wiki mbili urudi hapa tusaidizane kukuza huu uzi, lakini kwa msaada zaidi, wakati unafanya huu ujinga, hakikisha unaandaa na powerbank kwa ajili ya dharura siku kadhaa zijazo, pia hakikisha unatembea na USB Cable kwenye wallet yako!
 
Kwangu haikubali bila kuwasha data
Sasa itakubali vipi bila ya kuwasha data [emoji856][emoji856][emoji856][emoji856]data ni tofauti na bando ...washa data bila ya bando kisha washa vpn ..ngoma inakonecti
 
Mnapenda vya bure nyie watu!
 
Niliwahi ku comment humu! Simu inachemka balaa ukitumia VPN , halafu chaji inaisha fasta.sasa hiyo hali ikiwa kila siku lazima betri libabuke.

Ngoja aje chief mkwawa atupe maarifa zaidi.
 
Mkuu, jaribu kuwauliza google kuwa infinix hot 10i zina uwezo upi kwenye battery, ukikuta ni 6000 mAh rudi hapa uweke like, kisha upita kimyakimya wanaozijua simu wasije kukucheka!
 
Nimetumia hizo wire turn, thor etc lakini nilikuja kuona naichosha tu simu yangu maana zina run background, network bandwidth ndogo, slow internet connection mwishowe simu ina struggle sana ku access internet inaishia kupata moto kuliko kawaida yake. Kwanini maisha ya betri yasipungue!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…