Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

VPN kuharibu betri nakubaliana nalo hilo,,,ishawahi nitokea,,,simu ilikua inachemka kichiz mwisho ikazima,,,ikabidi nibadilishe tu betri!
 
Kwa tunatakiwa tuset vp boss
Tatizo lenu ni kuto kuset simu vizuri vpn ipo kama 2g tu hakuna uhusiano wowote na kuchemka simu wala kufa betri na sababu tunazijua
 
Nimezima data voda nimetest thunder vpn now ngoma imekubali kuanzia sasa nikiweka bando bila sababu za msingi mniite paka.
Mimi inaniletea hivi
Kwahiyo lazima niconnect data ndio nitumie??
Nashindwa kuelewa mana nna bundle hivo nikiwasha data sielewi inayotumika ni hivo vpn au ni bundle langu
Screenshot_20220821-093129.jpg
 
Mbona mimi ninatoa maelezo kila siku hata hapa nipo JF BILA YA BANDO ...TUMIA "THUNDER VPN" ila uwe na raini ya halotel basi utapata intanet bure utatumia ...mimi natumia JF ,TWEET, FACEBOOK, ISTAGRAMU, WHATSAPP, YOUTUBE , GOOGLE BURE SIKU ZOTE ..ILA INAKUWA SLOW KIDOGO
Nq sisi wa tigo na airtel tusaidie mkuu
 
Hello wanajamii forums,

Ni wiki kama mbili sasa tokea kutumia zile apps za wire tun, Thor VPN na HA Tunnel zinazotoa huduma ya free internet kutoka servers za mbali kama vile UK, US, German e.t.c

Simu yangu iliyotoka kiwandani ikiwa na 6000 mAh, ambayo ilimaliza siku 3 pasipo kuchajiwa kwa matumizi ya kawaida pasi na kuwasha data, au masaa 40 kama nitaacha data on! Sasa imegeuka nahisi si zaidi ya 1400 mAh.

Mwanzoni wakati naanza kutumia hizo huduma, simu ilichemka kuliko kawaida, kuna wakati niliiweka kwenye friji ili ipunguze joto, maake nilihisi ingelilipuka. Nimetumia kwa muda sasa kiasi kwamba simu ilichukua masaa sita tu kuwa na chaji. Ndipo nilipoamua kufuta app hizo!

Mbali na kuchukua hatua hiyo, simu yangu inatunza chaji kwa muda wa masaa nane tu, niwashe data, nisiwashe data, niitumie, iwe screen off, niizime, nisiizime! Haya yote yamekuwa bure! Masaa nane tu ndio yaliyobaki kuniweka hewani! Vya bure vimeniponza!

😂 😂 😂 😂 hakunaga vpn ya free internet, acha kupiga watu
 
Tafuta lain ya TTCL, ingia playstore, download Wire Tun, baada ya hapo, hakikisha laini yako imeisha bando au haina bando kabisa, washa data hivyo hivyo! kisha fungua app ya wire turn, chini ya app kuna bar imeandikwa server list, bofya hapo, chagua moja kati ya server hizi Canada2, US 4, UK2, France2 lakini hiyo server ya kwanza na ya pili ni nzuri zaidi! Ikiwa inafika mida ya saa 10 jioni hadi saa 4 usiku utaingia YouTube, tiktok, likee, tsapp na instagram! Muda mwingine tumia kwenye facebook, tsapp, jamiiforums, Quora na chrome!

Ili kuongezewa muda uwe unawatch ads kwenye app yao, kila ad utapewa 30 min za kuperuzi! Tumia uwezavyo!

Baada ya wiki mbili urudi hapa tusaidizane kukuza huu uzi, lakini kwa msaada zaidi, wakati unafanya huu ujinga, hakikisha unaandaa na powerbank kwa ajili ya dharura siku kadhaa zijazo, pia hakikisha unatembea na USB Cable kwenye wallet yako!
[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwahiyo tujiandae kabisa kisaikolojia
 
We ni mgonjwa kumbe sasa infinix ni simu? Brand zote kali nazijua ndo mana nikamalizia mwishoni kwa kuandika bila shaka ni wanzuu nikimaanisha tecno, itel, infinix..ndo watumiaji wake wanapenda mserereko sababu sio rahisi ukute mtu ana macho matatu anahangaika na Free internet
Mkuu hii comment yako umeuwa kabisa, na sisi wenye Oppo tuna simu au ni calculator tu?
 
Back
Top Bottom