Internship (Manamba) mashambani Israel?

Internship (Manamba) mashambani Israel?

Intership na nafasi nyingi nazo ni connection labda kama wanafanyisha interview wenyewe ila kama wasimamizi ni wabongo hamna kitu ..

Ishu ipo wazi kila kona huo ujinga upo usije na ujinga wa ukanda wako ,chuo kina watu mchanganyiko sasa elimu kila acheni ubaguzi wa kijinga mtu akifa mnataka huruma ya watanzania wote ,pelekeni huo msib huko kwenu kama mnaleta ubaguzi.
Watu wanalipa pesa wapate nafasi na kwenda israeli,kikubwa pesa tu.
Hata vyeti havitumiki pale kwenye usaili wala popote.

Utakuta mtu hata kilimo hakijui wala hajasomea mambo hayo amehonga pesa aende na anaenda kuogesha mbuzi wa kiyahudi.

Sugeco waje hapa wakatae rushwa iliyoko hapo.
 
Dogo hiyo programme ipo zaidi ya miaka minne. Uliishasikia Kila wakienda wanakufa? Imetokea mara moja, tena kitendo cha kigaidi unaleta ngonjera humu? Kwahiyo hutaki waende? Ushamba wa wapi huu!?
Program ina miaka 9 kama sio kumi ukakae ughaibuni mwaka urudi na milioni 4 hivi hamna huruma na vijana wetu kabisa jamani embu tumieni komoni sensi
 
Get rich or die trying. Kama zipo za kwenda kubeba tofari mnishtue hata ikiwa Iraq nakwenda mradi salio liwe zuri.
 
Kule wanajifunza kufanya kilimo Kwa vitendo ndio maana wanapewa diploma. Israel ipo advanced kwenye masuala ya kilimo. Wanazalisha chakula kingi na kusambaza duniani. Halafu wanaoenda kule sio watanzania tuu hata watu kutoka mataifa mengine wanaoenda. Kuna jamaa mmoja tulikuepo shortcourse Thailand anatokea Timor Leste alienda israel kwenye mafunzo. Halafu kule wanapokea mkwanja mrefu Sana . Wanarudi na chochote kile Tanzania

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
mkwanja mrefu my foot kama kijana katokea familia maskini akituma pesa nyumbani mara kadhaa tu harudi na kitu acheni upotoshaje anayepata pesa kwenye hii program Mama Temu acheni upotoahaji
 
Ivi wewe unawajua wachanga wewe, hawawezi kuunganika ni wabinafsi sana
Tukiwaangalia wachaga kwa mtazamo chanya, ndiyo watu wanaoweza kuungana na yeyote, mradi tu kuwe na faida. Huu ubinafsi tunauona kinyume kwa sababu ya fikra hasi.
Mchaga ametawanyika nchi nzima na sasa anaelekea dunia nzima.
Kwa hali hiyo kweli utaona kuwa hawezi kuungana na wengine?
 
Hii suala watu wa sua waulizwe,wanaujua ukweli kuwa wale vijana wanaenda kukamua maziwa ng'ombe,mbuzi, wala si intership.

Mtu ana degree anaenda huko eti kutawaza mbuzi,kubeba kuku,kufagia mabanda ua wanyama.

Hiyo sugeco kwa sasa ni hadi watu wanalipia kwenda israeli.

Sua hapa wawajibike.
Hapa changamoto ni tafsiri ya elimu.
Sasa degree zinatumikaje au wanasoma ili wafanye nini?
Wanatakiwa wajue practically ili wasaidie wakulima na wafugaji wetu.
Zile fikra za kwamba ukisoma chuo bila kuelewa halafu uajiriwe ule pesa za serikali tena kwa hasara bila tija yoyote zimepitwa na wakati.
Graduate lazima Uwe field practically upate experience. Hizi fursa hapa nchini ni change au hazipo na badala yake wachache watawekwa ofisini wakiandika ripoti za kipuuzi tu kwa kukariri.
Tunataka graduate akawe mkulima na mfugaji binafsi (serikali image mitaji/mikopo) na siyo huu ujinga wa ekari mbili ambao ni matumizi mabaya ya fedha za Uma bila tija na ripoti zitakuwa nyingi zisizo na faida yoyote.
 
Huu utaratibu wa kupeleka vijana Israel;

1. Nani anaratibu?

2. Sifa za kujiunga Ni zipi? Maana naona wanufaika wanatokea Kanda ya Kaskazini zaidi, Kuna nn hapo? Ukute Coordinator Mangi anapata Dola zake kimyaa huku vijana wanafuata kifo.

3. Usalama wao upoje? Shambani/vitani.

4. Je, ipo MoU au makubaliano yoyote? Au ndo modern slave trade/human trafficking?
We acha tu! Mengi yatajulikana. Eti wanasema tusichimbe, kwani hilo ni suala la Serikali.

Mitandao raha, Inachimbua mpaka habari za mafichoni.
Degree ya Kilimo- kwenda mashambani kuvuna mazao. Pazuri hapo! Mi sisemi.
 
Watu wanalipa pesa wapate nafasi na kwenda israeli,kikubwa pesa tu.
Hata vyeti havitumiki pale kwenye usaili wala popote.

Utakuta mtu hata kilimo hakijui wala hajasomea mambo hayo amehonga pesa aende na anaenda kuogesha mbuzi wa kiyahudi.

Sugeco waje hapa wakatae rushwa iliyoko hapo.
Connection na pesa tu
 
Labda Kilimanjaro tu, Arusha wamasai na shule wapi na wapi?
Ongea unayoyajua mzee Arusha ina wamasai tu? WaPo watu lukuki hapo me siangaliii kabila me naangalia ukimuuliza mtu unaishii wapi anajibu, Arusha na moshi kuna wanafunzi wengi vyuo vikuu kutokea pande hizo
 
Intership na nafasi nyingi nazo ni connection labda kama wanafanyisha interview wenyewe ila kama wasimamizi ni wabongo hamna kitu ..

Ishu ipo wazi kila kona huo ujinga upo usije na ujinga wa ukanda wako ,chuo kina watu mchanganyiko sasa elimu kila acheni ubaguzi wa kijinga mtu akifa mnataka huruma ya watanzania wote ,pelekeni huo msib huko kwenu kama mnaleta ubaguzi.
Unaongea hata usiyo yajua nikuache tu
 
Hii suala watu wa sua waulizwe,wanaujua ukweli kuwa wale vijana wanaenda kukamua maziwa ng'ombe,mbuzi, wala si intership.

Mtu ana degree anaenda huko eti kutawaza mbuzi,kubeba kuku,kufagia mabanda ua wanyama.

Hiyo sugeco kwa sasa ni hadi watu wanalipia kwenda israeli.

Sua hapa wawajibike.
Bila picha huu ni uongo, ukiwa na degree ndo unachagua kazi! Degree ni nini kwa unexperienced personel?
 
Dalali wao anaitwa Dr Temu pande za Sua wanakulipia nauli Na Visa ukilipwa wanakukata cost zao
Wanawahadaa vijana wenye Degree ukienda shambani unalipwa na unatoka na Cheti cha Diploma ya Agriculture hivi uwe na Degree then utunukiwe Diploma 😆😆

Kuna kijana mmoja nilimskitikia sana mzazi wake baada ya kuniambia Kijana wake kafanikiwa kwenda Israel kujifunza masuala ya Intelijensia kwa udhamini wa Serikali
Ahsante kwa Taarifa.

TAKUKURU...!???😞😞
 
Kila kitu kitajulikana yule wa Urusi kafikaje pale mpaka kupigana vita vita ?Ni wa huko kaskazini..

Serikali ikae chin ifuatilie tangu yule wa kwanza...Kuna kitu hapa .

Unafikria kutoka nchi fulani kwenda nyingine kupata kazi kama jeshini ni rahisi tena sehemu nyeti kweny usalama wa taifa.

..hata aliyeshiriki ktk shambulizi la kigaidi Kenya alikuwa Mtanzania toka Kaskazini. Tena anatokea familia ya wafanyabiashara matajiri.
 
Maisha ya bongo kwa vijana jehanamu tosha Bora ukafie vitani Israel au Urusi watoe TU connection kwa vijana.
Hata ukifa familia yko ipate mafao iukimbie umasikini,ukipona utambe mjini.
Umasikini sio poa.
Posta mbezi kwa mguu kukosa buku ya daladala sio poa.
Kifo kipo tu kama kimefika
 
Bila picha huu ni uongo, ukiwa na degree ndo unachagua kazi! Degree ni nini kwa unexperienced personel?
Nipinge kwa hoja za msingi,sio kusema uongo.

Hivi tanzania hapahapa wameshindwa kujifunza kilimo?

Je yale mashamba sua yana kazi gani kama si kujifunza kwa vitendo?

Mtu mzima anasafiri kwenda kuogesha mbuzi na wanyama israeli mnadanganya anajifunza kwa vitendo wakati hao wengi wao huonga pesa kupata nafasi husika.

Kwani jambo hili halijulikani?,kuwa hata mtu hajasomea kilimo anapata connection anaenda utumwani israeli?

Sugeco waache uhuni.
 
Back
Top Bottom