Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Mimi nina mwanangu ana miaka 4 alikuwa hajaanza shule kwa kweli maana nilikuwa namuona kama ni mdogo sana bado.
Sasa, sasahivi ndo naona angalau kamekua kidogo, hivo nimeona ni busara aanze rasmi shule.
Ila juzi kati hapa kuna shule ya Nusery ipo karibu na ninapoishi, so nilienda kwa lengo la kumtafutia nafasi ili aanze shule.
Kinyume na fikra zangu kwamba mambo yatakuwa straight forward, ila nimeshangazwa sana baada ya kuambiwa hapa hawapokei mtoto asiyejua kusoma na kuandika, na kwamba eti kabla ya kuingia huwa wanatakiwa wafaulu interview.
Akaendelea kuniambia kwamba, hata kama ni mtoto wa miaka 3. Lazima ajue kusoma na kuandika ndo aingie hapo.
Kwa kweli hapa nimejikuta nipo kwenye hali ya kushangazwa sana na hichi kitu. Yaani naona kabisa hizi ni complication ambazo hazina msingi.
Halafu naona kabisa hawa watoto wadogo wa miaka mitatu wanaolazimishwa kujua kusoma na kuandika, hichi kitu kitakuja kuwaathiri sana miaka ya baadae. Sijui huu utamaduni wa kishenzi umetoka wapi, yaani mtoto wa miaka mitatu au minne, eti humtaki kisa hajui kusoma na kuandika.
Hivi no halali kweli hii issue? Au ni jamii yetu inazidi kupotoka