Interview kwa watoto wanaoingia Nusery School ni haki kweli?

Interview kwa watoto wanaoingia Nusery School ni haki kweli?

Nakumbuka hili... Wakati mwanangu anaanza Baby Class .... Tulikuwa wazazi zaidi ya 500+.... Walikuwa wanataka wanafunzi 80 pekee. Nilishangaa Sana😅
Haaaah...hao watakuwa vipanga wa seminary
 
Mimi nina mwanangu ana miaka 4 alikuwa hajaanza shule kwa kweli maana nilikuwa namuona kama ni mdogo sana bado.

Sasa, sasahivi ndo naona angalau kamekua kidogo, hivo nimeona ni busara aanze rasmi shule.

Ila juzi kati hapa kuna shule ya Nusery ipo karibu na ninapoishi, so nilienda kwa lengo la kumtafutia nafasi ili aanze shule.

Kinyume na fikra zangu kwamba mambo yatakuwa straight forward, ila nimeshangazwa sana baada ya kuambiwa hapa hawapokei mtoto asiyejua kusoma na kuandika, na kwamba eti kabla ya kuingia huwa wanatakiwa wafaulu interview.

Akaendelea kuniambia kwamba, hata kama ni mtoto wa miaka 3. Lazima ajue kusoma na kuandika ndo aingie hapo.

Kwa kweli hapa nimejikuta nipo kwenye hali ya kushangazwa sana na hichi kitu. Yaani naona kabisa hizi ni complication ambazo hazina msingi.

Halafu naona kabisa hawa watoto wadogo wa miaka mitatu wanaolazimishwa kujua kusoma na kuandika, hichi kitu kitakuja kuwaathiri sana miaka ya baadae. Sijui huu utamaduni wa kishenzi umetoka wapi, yaani mtoto wa miaka mitatu au minne, eti humtaki kisa hajui kusoma na kuandika.

Hivi no halali kweli hii issue? Au ni jamii yetu inazidi kupotoka
Kwahiyo wanamaanisha huyo mtoto alitakiwa ajue kusoma na kuandika akiwa tumboni au? 😅😅😅
 
Siku hizi watoto wanateseka sana twa miezi saba nao wanaanza shule,ka miaka miwili kanaamshwa saa kumi na moja kujiandaa kwenda shule. Sasa huyo wa miaka minne wanamkataa wakati wao ndio wenye jukumu la kumfundisha kusoma na kuandika aiseee.

Bora serikali imepiga marufuku watoto boarding ilikuwa balaa hadi wa miezi wanapelekwa boarding
Aiseee, hii ni kali mkuu.
 
Kiukweli sio haki Sasa miak minne kusoma alijifunzia wapi na yeye kazi yake itakuwa nn km anatak mtoto anaejua kusoma tayari
 
Unaogopa nini? Kama hawezi hata kuongea vizuri? Kama ana matatizo ya kiakili? Nk
 
Kwanini mkuu... mimi wao ndo nawaona wana matatizo.. maana huwez kusema eti unaanza kumpima mtoto akiwa na miaka 4... kuna wengine wetu mpaka darasa la saba tulikuwa hatujielewi, ila baada ya hapo tumesonga kielimu kupita hata wale ambao walikuwa wanaonekana ni ma genius wakiwa wadogo
Mimi nimeanza kujielewa nikiwa darasa la 2.
Kuna njemba ilikua inakimbiza wilaya nzima yenyewe imeanza kushine darasa la 4, huko nyuma alikua hata hajui shule anakuja kufanya nini.

Mwingine huyu ye kaanza kujielewa na kufaulu darasa la 6.
Sometimes watu hubadilika kadri muda unavyokwenda japo wengine ndo hawabadiliki.
 
Na wewe mzazi sio mbaya ukajifunza kuandika Kiswahili fasaha.
Hakuna neno "hichi" kwenye lugha adhimu ya Kiswahili.
Omba nawe nafasi hapo nursery school ufundishwe lugha.

Elimu haina mwisho.
 
Back
Top Bottom