Interview kwa watoto wanaoingia Nusery School ni haki kweli?

Nikamuambia sasa kama hajui kusoma na kuandika si ndo mumfundishe? Eti hooh, hiyo haiwezekani kabisa....
Sasa kama anajua kusoma na kuandika, hapo nursery wao watamfundisha nn?

Dogo apigwe interview, hiyo hali iliyokukuta unaweza baki hauna majibu, unatoa tu macho au ukaanguka na vichekoo

Ni kama comedy flan hiyo nursery
 
Imebidi niondoke tu kwa upole maana hata hao walimu wenyewe niliona hawana logic....
 
Mdogo wangu anasoma shule Moja basi la njano anarudi amechoka sana😬 home work kibao aise
Aisee pole kwake. yani sema wabongo kwa kuvamia vitu vya wazungu tupo vizuri sana. hadi homework kibao. maskini kawaida wanapaswa one homework. yani napata hasira nikisia wanawachosha watoto wadogo. yani kwa uzoefu wangu sio hivyo. halafu watoto hawaenjoy nursery sana.
 
Ni tatizo kubwa... inaonesha kabisa kwamba bado hata walimu wa hizi shule hawajui dunia inapokwenda.... yaani kabisa unaweka interview kwa mtoto wa miaka 3.... huu ni upumbavu
 
Mimi nilidhani kipindi wanasema interview lengo ni kula zile 30000
 
Sahizi shule itageuka terrible Kwa watoto dogo apa namuona kabisa hataki shule kuamka saa 6:10 am gari linapita😬 kurudi saa 5pm apo akutane na homework za kutosha kesho tena msoto ule ule mpaka jumamosi
 
Sahizi shule itageuka terrible Kwa watoto dogo apa namuona kabisa hataki shule kuamka saa 6:10 am gari linapita😬 kurudi saa 5pm apo akutane na homework za kutosha kesho tena msoto ule ule mpaka jumamosi
Kuna mwanangu mmoja akiwa sijui kg 3 ilikua kila siku anaumwa asubuhi mara kidole mara tumbo yani hoi kabisa kumbe shida na mzunguko wa school bus
 
Kama wazazi tuna wakati mgumu sana katika malezi, kila mtu anaongea lake, walimu huko mashuleni wanakuja na yao mengine hata hayaeleweki yani.
 
Yaani hao wanatakiwa kufutiwa usajili shule ya vidudu mara moja. Shule ya vidudu kazi yao ni kulea tu watoto umri huo na kuanza kuwafundisha a,b,c na 1,2,3. Hii tabia ya uroho na ubabaishaji umerudi kwa nguvu sana tangu samia kua rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…