Interview kwa watoto wanaoingia Nusery School ni haki kweli?

maskini...kg 3 alikua anaumwa?.
Alichoka shule maana route nlokua nakaa wao ndo wa kwanza kufwatwa na wa mwisho kuletwa sasa naona ule uchovu akaona awe anaumwa kila siku asubuhi, yani analegea kabisa mpka unaahirisha kwenda kazini umpeleke hsptl, ila kwa sasa nimeamia oengin walau wapo karibu na shule hawachoki sana
 
Kama ulikubali mwanao afanye mtihani, wewe na wao hamna tofauti ni pipa na mfuniko
 
Na ukakubali afanye interview? Kwamba shule ipo moja tu? Ni lazima asome hapo?
 
Afadhali ni kazi sana...mimi kuna huyu wa 3yrs nikiona amechelwa kulala kesho haendi shule ni mm mwenyewe naamua tuu namwacha alale sitaki kumtesa mtoto...kuna kipindi niliona ameenza kudorora afya yake nikamwacha siku 3 nyumbani nikampiga menu nzuri angalau...mimi si take serious sana shule ya hawa kindergaten..aende haya siku asipoenda haya..
 
Mtoto anatakiwa aanze nursery na huo umri, ndio aanze baby class
 
Akaendelea kuniambia kwamba, hata kama ni mtoto wa miaka 3. Lazima ajue kusoma na kuandika ndo aingie hapo.[emoji23] hakuna shule hapo
 
Mie wa kwangu mpka above 5+yrs kabisa.kusoma sio uhai kikubwa koneksheni. Kuna watu Wana vyeti feki ama chawa wanaongoza wilaya na wenye PhD zao na mpaka maprofesa wanaishi kwa shida.

Ama sure isn't everything,yaani asome kisela tu. Diploma ukijumlisha akiwa na akili ya kitaa ama emotional intelligence nadhani ata survive vizuri hapa duniani. Pia na English amwage Kama cherehani ya kudarizi , financial literacy awe nayo ya kutosha na hii anaipata home.
Unamnunulia share za stocks za Tesla,Amazon,apple ,usa30, dax40 nadhani Ni elimu tosha. Yaani elimu watu wanayoipata mtandaoni inazidi ya darasani .yaani kikubwa ajue uwekezaji ama Kama ana kipaji akiendeleze na sio kukomalia apate mavyeti utadhani ndio Kinga ya maisha.

Kuna watu wanamaliza havard school of business wanakuja kujifunza biashara YouTube na vitabu vya akina Graham of value investor na masela wengine ambao Ni ma hasla kitaa so Wana knowledge kubwa sema kisa haipo formally Kama ya maprofesa Basi wanakuwa wanaonekana Kama hawana la ajabu Sana.

Kuna profesa anafundisha trading ana investment Ila ukimwambia trade ama invest hii $100000 tafuta 20% annually hawezi kazi kuongea na maneno hayana gharama kuyaongea .


Ndio akili yangu Karibuni wenye matusi,kupinga,kuunga juhudi mkono
 
Ujinga tu kwanza lengo la mzazi kumuanzisha mtoto wa miaka 4 shule sio kusoma ni kupata exposure tu na kutengeneza marafiki may be
 
Mkuu ungewauliza hiyo Nursery wao wanawafundishanini watoto incase wanaanza tayari wakiwa wanajua kusoma na kuandika??
 
Yeah, binafsi hadi 4yrs ndio madogo wanaenda shule. Hizi mambo za kupeleka watoto shule wakiwa na miaka miwili sio hata kidogo.
Kama wa kwangu 4yrs.
Nawahurumia wale wa 2 yes kupelekwa shule
Na 4yrs ni kwa sababu mtoto anapaswa apitie nursery
 
Mie naomba tu ufafanuzi wa hizo stock

Ukitaka wapongaji wasubiri wale wa kataa ndoa[emoji1][emoji16][emoji16]
 
Hukumpeleka baby class mkuu. Kuna nyingine hawapokei kama kavuka miaka 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…