Interview Rais Samia na Azam TV, azungumzia safari, Urais, Mikopo ya Miradi ya Magufuli, Ripoti ya CAG

Interview Rais Samia na Azam TV, azungumzia safari, Urais, Mikopo ya Miradi ya Magufuli, Ripoti ya CAG

Kwani kila pesa ya mkopo ni pesa ya nje, kama tulikopeshwa na Makampuni ya ndani je? Kwani lile daraja pale Kigamboni si limetumia pesa za ndani ambazo ni mkopo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii? Huenda wewe ndiye unayekaza fuvu kuliko huyo unayemshutumu.
Umeona lkn Rais alichozungumza kuhusu miradi na fedha zake? Point ndio hiyo amesema ni mikopo kutoka nje ya wafadhil!! Basi tufanye hivi... Awamu ya tano miradi yote mikubwa iliendeshwa kwa fedha za ndani!! Over!!
 
Mbona tulisikia yule bwana alikua katili na dikteta jumuiya za kimataifa ya nje walimchukia na kusababisha nchi kutofunguka, iweje sasa awe amekopa pesa nyingi hivyo za miradi mikubwa. Ni kina nani walimkopesha ikiwa alikua dikteta? Nawazaga sana...
Nchi ngumu sana hii, walisema aliifunga Nchi tukakosa Mikopo na Misaada kutoka nje, Wao wameifungua Nchi na fedha zinaanza kumiminika! Unajua kuna wakati wanaona aibu kusema ukweli, wanaangalia upepo wa wakati huo ndiyo maana hizi contradiction zinatokea.
 
Nchi ngumu sana hii, walisema aliifunga Nchi tukakosa Mikopo na Misaada kutoka nje, Wao wameifungua Nchi na fedha zinaanza kumiminika! Unajua kuna wakati wanaona aibu kusema ukweli, wanaangalia upepo wa wakati huo ndiyo maana hizi contradiction zinatokea.
Waongo

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Umeona lkn Rais alichozungumza kuhusu miradi na fedha zake? Point ndio hiyo amesema ni mikopo kutoka nje ya wafadhil!! Basi tufanye hivi... Awamu ya tano miradi yote mikubwa iliendeshwa kwa fedha za ndani!! Over!!
Mbona kama unatumia hasira Mkuu? Hapa tunaelimishana, kama ulikuwa unafuatilia hotuba za Mwendazake kuna wakati alisema walipotaka kuanzisha Mradi wa Reli "SGR" waliomba fedha za mkopo ili kuanzisha na wakapewa Masharti magumu, ikabidi watumie fedha za ndani kuanzisha Mradi huo ndipo baadae wakajitokeza kutoa Mikopo yenye Masharti nafuu.

Kusema kwamba tuliaminishwa kuwa Miradi yote inatumia fedha za ndani hizi ni propaganda, lakini ni kweli pia ipo Miradi mingi ambayo ilitumia fedha za ndani kama ule mfano niliokupa awali.

Ipo Miradi ambayo ilifanyika kwa kuahirishwa shughuli fulani za Serikali na fedha kupelekwa kwenye Miradi ya kimaendeleo, ipo Hospitali pale Dodoma, barabara ya Moroco Dar es salaam n.k.
 
Si tulikuwa tunaambiwa tunajenga kwa fedha za ndani?
Kwani hakuna Miradi iliyofanyika kwa fedha za ndani? Lile daraja pale Kigamboni ni mkopo wa nje? Hata Mradi wa Reli ulianza kutekelezwa kwa fedha za ndani, uwe unafuatilia mambo si kuwasikiliza tu Wanasiasa, kama uliambiwa tunajenga kwa fedha za ndani na Mwanasiasa ukaamini leo unaambiwa na Mwanasiasa tulikopeshwa unaamini, yupi yupo sahihi kwako hapo, do you have any evidence?
 
Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje?
[emoji15][emoji15][emoji848] Tuachane na hilo la pili kwamba itaendeleaje.. Maana hata yeye hapa anatia shaka..! Sasa tuje kwenye tafsiri ya 'fedha zetu Lakini tulikopeshwa'[emoji848]... Kikiwa chako ni chako huwezi ukakopeshwa na yoyote yule bali unaweza kukopesha.. PERIOD!
Peas iliyojenga miradi mikubwa ilikuwa ni ya MIKOPO MIKUBWA YA SIRI isiyojulikana masharti yake

ukikopa maana yake umefanya matumizi ya pesa zako unazotarajia kupata mbelen mda huu, katafute kitabu cha ray del rio anazungumzia the economic time machine utaelewa
 
Statement hii INAELEZEA VITU VINGI SANA vilivyo nje ya upeo wa macho YETU...
Opera Snapshot_2022-05-05_104949_www.jamiiforums.com.png
 
Inawezekana ni fedha za mkopo kutoka ndani ya Nchi, sijaona mahali aliposema vinginevyo, yeye kasema tulijenga kwa fedha zetu lakini za mkopo, kwani lazima kila mkopo uwe wa fedha za nje?
Sawa. PSSSF wanahusika hapa. Wapo Hoi bin taaban.
 
Mradi gani hauendelei? Umelewa chimpumu nini?
  1. Njia za DART (Morocco/Mwenge DSM) kimya.
  2. Mradi wa JNHPP (2025 badala ya June 2022).
  3. SGR serikali iko kimya.
  4. Barabara ya Kimara Kibaha 8 lanes kimya.
  5. Daraja la Kigongo kimya.
 
Back
Top Bottom