Interview Rais Samia na Azam TV, azungumzia safari, Urais, Mikopo ya Miradi ya Magufuli, Ripoti ya CAG

Interview Rais Samia na Azam TV, azungumzia safari, Urais, Mikopo ya Miradi ya Magufuli, Ripoti ya CAG

Shida ya mama, usishangae kesho akisema tofauti. Siku chache zilizopita alisema tumeondolewa uchumi wa Kati, Leo anasema bado tupo.
Memory jamming maybe due to royal tour fatique
 
Wabongo wengi mna upumbavu mobu , sasa wewe shida yako kama mwananchi ni nini? ni masharti au unataka miradi ifanyike? Hayo masharti umewahi wekewa hadharani tangu awamu ya kwanza ya fisiemu ?
Asante kwa kutusifu na kututukuza .. Tumeyapokea maoni yako kwa roho nyeupe
 
Sijui iwapo cognitive competence ya Sasha iko sahihi. Miradi iligarimiwa na fedha za mikopo. Sawa! Lakini miradi haijakamilika na inaonekana serikali imeishiwa fedha za kukamilisha miradi hiyo wakati mikataba ya mikopo ya kugharimia miradi husika bado ni hai!

Sasa kwa nini miradi imesimama, haiendelei kutekelezwa wakati mikataba ya project funding (construction phase) bado iko hai? Je, mikataba ya mikopo husika iliandaliwa kutegemea uhai wa mwendazake? Kwamba project funding phase inge-cease immediately baada ya Magufuli kufaariki dunia!? Inakuwaje baada ya kifo cha mwendazake mikopo ya miradi imedorora kiasi cha serikali kushindwa kuhitimisha miradi kama ilivyokuwa imepangwa?
Mama hataki sera ya kupora pesa matajili kufadhili hiyo miradi. Au kuwateka kina Mo Dewji ili warudishwe kwa mabillioni.


Kimsingi mama hataki Gangster Government.
 
Mbona tulisikia yule bwana alikua katili na dikteta jumuiya za kimataifa ya nje walimchukia na kusababisha nchi kutofunguka, iweje sasa awe amekopa pesa nyingi hivyo za miradi mikubwa. Ni kina nani walimkopesha ikiwa alikua dikteta? Nawazaga sana...
 
Sijui iwapo cognitive competence ya Sasha iko sahihi. Miradi iligarimiwa na fedha za mikopo. Sawa! Lakini miradi haijakamilika na inaonekana serikali imeishiwa fedha za kukamilisha miradi hiyo wakati mikataba ya mikopo ya kugharimia miradi husika bado ni hai!

Sasa kwa nini miradi imesimama, haiendelei kutekelezwa wakati mikataba ya project funding (construction phase) bado iko hai? Je, mikataba ya mikopo husika iliandaliwa kutegemea uhai wa mwendazake? Kwamba project funding phase inge-cease immediately baada ya Magufuli kufaariki dunia!? Inakuwaje baada ya kifo cha mwendazake mikopo ya miradi imedorora kiasi cha serikali kushindwa kuhitimisha miradi kama ilivyokuwa imepangwa?


Labda jamaa wameona wa-cease baada ya jamaa kuchomoka sababu walimuamini sana jiwe kuliko mtu mwingine…

 
Sawa, umeongea vyema kabisa.
Sisi tunataka kuambiwa ukweli huku haki, katiba na maendeleo ya kweli ya watu vikiheshimiwa.
Pia tunataka katiba mpya iliyobora
 
Mama hataki sera ya kupora pesa matajili kufadhili hiyo miradi. Au kuwateka kina Mo Dewji ili warudishwe kwa mabillioni.


Kimsingi mama hataki Gangster Government.

 
Ninachomkubali huyu mama ni msema kweli, kuna jitu liongo eti lenyewe likawa linajiita ati msema kweli mpenzi Mungu, kumbe ni liongo namba moja.
Kama ni msema ukweli mbona hatuambii walichangia loyal tour?
 
Yeye yuko wazi tunatekeleza kwa mikopo full stop.. Sio tulidanganywa tutembee kifua mbele eti tunajenga kwa pesa zetu z a ndani kumbe ni mikopo.. Je umeelewa sasa?
Ebu weka hapa mikataba aliosaini huko marekani mimi sijaiona usisahau na ule wa World Bank
 
Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza na Tido Mhando wa Azam TV, leo Mei 4, 2022


RAIS SAMIA: HAKUNA FUNDI WA URAIS, HAUZOELEKI
Rais Samia Suluhu Hassan amesema nafasi ya Urais haizoeleki kwa kuwa kuna mambo mengi.

“Sidhani kama kuna mtu anaweza kusema ni fundi katika nafasi ya Urais, labda kama mimi ni mgeni kwa kuwa nina mwaka mmoja.

“Nilipoteuliwa kuwa Rais mshtuko ulikuwa tukiola msiba haikuwa Urais kwa kuwa nilikuwa Makamu Rais kuna mambo nilikuwa nayajua,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.


SAMIA: TULIKOPESHWA FEDHA ZA MIRADI MIKUBWA
Rais Samia amezungumzia miradi mikubwa ambayo ilikuwa ikitekelezwa wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli kwa kueleza kuwa alikuwa akiijua lakini changamoto ni kwa kuwa ilikuwa ikiendeshwa kwa fedha za mikopo.

“Miradi ilikuwa ya kwetu kwa kuwa nilikuwepo katika Awamu ya Tano na nilikuwemo katika mipango na utekelezaji, changamoto ni ukubwa wa miradi na uwezo wetu wa ndani.

“Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje? Lakini ni miradi yenye tija,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.


SAMIA: SAFARI ZINA FAIDA, LAZIMA TUTOKE TUKATAFUTE
Rais Samia amezungumzia kuhusu safari zake za nje ya nchi kwa kusema kuwa anatoka kwa kuwa safari zina faida nyingi kwa nchi ikiwemo kufungua biashara.

“Wanataka tujifungie hapa afu walie ukata mifuko ipo mitupu, sina miujiza ya kujaza mifuko yao, lazima tutoke tukatafute.

Wafanye tathmini za safari zenyewe, kila ninapoenda ninakuwa na wafanyabiashara, mfano nilikuta vikwazo 64 Kenya na vyote tulitatua baada ya kuzungumza,” Rais Samia akizungumza na Azam TV.

Ameongeza kuwa safari zake za Marekani amesaini mikataba ambayo kama itatekelezwa Tanzania itaingiza Tsh. trilioni 11.

RAIS SAMIA: NITAWATAJA WALIOCHANGIA BILIONI 7 ZA ROYAL TOUR
Rais Samia Suluhu amesema kupitia vipande vya kuitangaza Filamu ya Royal Tour ambavyo vimekuwa vikirushwa kwa miezi mitatu sasa zimeleta faida kubwa ambayo ni zaidi ya kiasi kilichotumika kuandaa filamu hiyo.

Tsh. Bilioni 7 zilitumika kuandaa filamu huku Serikali ikisema zilitokana na michango ya wadau mbalimbali

“Ni fedha nyingi lakini faida zake zikianza kuingia wataona, kuhusu waliochangia juzi Arusha niliwashukuru kwa ujumla lakini nitawataja tu,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.


RAIS SAMIA: TUTAFUTA KODI YA MAFUTA YA KULA
Baada ya mafuta ya kula kupanda bei Rais Samia Suluhu ameelezea kilichotokea na njia inayofuata ni kuondoa kodi ya mafuta ghafi yanayotoka nje.

“Mwaka 2020 mabadiliko ya tabia nchi hatukufanya kilimo vizuri, bajeti ya 2019/20 tulipandisha kodi ya mafuta yanayoitwa crude ambayo hayakuwa na kodi.

“Mafuta yakawa hayaingizwi, nazi na chikichi hazikutosheleza soko, hivyo bajeti inayokuja tunaenda kupitia mfumo wote wa kodi, tutaondoa kodi ya mafuta ya kula ili walete crude oil tuichakate tupate mafuta tuyasambaze ndani,” Rais Samia akizungumza na Azam TV.


RAIS SAMIA: BEI YA MAFUTA TANZANIA NI NZURI KULIKO ILIVYO MAREKANI
Kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta miezi ya hivi karibuni, Rais Samia Suluhu amesema pamoja na hali hiyo bado bei ya mafuta kwa Tanzania ni nzuri ukilinganisha na yanavyouzwa Marekani.

“Kwa Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki, Tanzania tupo pazuri, hata kwa Afrika Mashariki sisi hali ya maisha ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.

"Kwetu bei za mafuta ni nzuri zaidi kuliko mafuta yanavyouzwa Marekani, lakini watu hawataki kutafuta ukweli, wanapiga kelele za kienyeji. Tanzania hatuagizi chakula, kipo cha kutosha,” - Rais Samia alipozungumza na Azam TV, leo Mei 4, 2022.
Hayo mazungumzo au hotuba?Aliulizwa hayo aliyoelezea au aliandaa majibu baada ya kupewa maswali kabla?
Siamini kama hayo ndiyo aliyoyanena,mbona mambo mengi Rais wetu anatulinganisha na yanayotokea Marekani?Je,ni kweli kwamba mafuta yanauzwa nafuu hapa kwetu kuliko Marekani,Kenya,Zambia au nchi zingine?Hii bei ya 3,200+ ndiyo anayolinganisha?Hii bei mpya kwa Dollar ni kiasi gani vile?
 
Kwenye mafuta ya kula, Rais anasema wanafuta kodi kwa mafuta yanayotoka nje. Hapo naona akina Mo Dewji wamerudi upya, kodi itafutwa na bei itabakia pale pale. Au Rais ni mgeni Tanzania?
 
Kumbe Bi Tozo nae analijua neno chawa, anatakiwa awaambie chawa wake waache uzushi kwa JPM.

Leo yeye mwenyewe amekiri uwezo wa serikali kulipa madeni umepungua, nchi imetolewa kutoka low risk kwenda kwenye moderate risks; mambo ambayo yanawapa wakati mgumu kukopesheka na mabank kwenye miradi ya kimkakati.

Hizo ni habari kwake lakini, sio JF alishaonywa baada ya muda mfupi atakuwa huko asibadili aliyoyakuta ni foundation ya kuelekea uchumi usiotegemea misaada na masharti.

Haya kiko wapi tumerudi kulekule halafu chawa wake kutwa kuongopa makusanyo ya kodi yamepanda. Unadhani ukusanyaji wa kodi unataka mambo ya kurembuliana macho.

Ni hivi harudi nyuma na kuangalia alikosea wapi, personal naweza sema nilitabiri mwaka jana ikifika mwaka huu mwezi wa sita kwa hatua zake watu wengi watakuwa wamechoka.

Kilichobaki sasa nifungue kibanda changu cha biashara ya utabiri na ushauri.
 
Back
Top Bottom