Interview Rais Samia na Azam TV, azungumzia safari, Urais, Mikopo ya Miradi ya Magufuli, Ripoti ya CAG

Interview Rais Samia na Azam TV, azungumzia safari, Urais, Mikopo ya Miradi ya Magufuli, Ripoti ya CAG

Kuwa na staha kwa mama zetu mkuu.
kata kama mama yako kama ataongoza familia yenu huo ni msiba.

hata katika Mitume wote waliotumwa na Mungu hakuna mwanamke.

Mungu sio mjinga
 
Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje?
[emoji15][emoji15][emoji848] Tuachane na hilo la pili kwamba itaendeleaje.. Maana hata yeye hapa anatia shaka..! Sasa tuje kwenye tafsiri ya 'fedha zetu Lakini tulikopeshwa'[emoji848]... Kikiwa chako ni chako huwezi ukakopeshwa na yoyote yule bali unaweza kukopesha.. PERIOD!
Peas iliyojenga miradi mikubwa ilikuwa ni ya MIKOPO MIKUBWA YA SIRI isiyojulikana masharti yake

Wabongo wengi mna upumbavu mobu , sasa wewe shida yako kama mwananchi ni nini? ni masharti au unataka miradi ifanyike? Hayo masharti umewahi wekewa hadharani tangu awamu ya kwanza ya fisiemu ?
 
Sijui iwapo cognitive competence ya Sasha iko sahihi. Miradi iligarimiwa na fedha za mikopo. Sawa! Lakini miradi haijakamilika na inaonekana serikali imeishiwa fedha za kukamilisha miradi hiyo wakati mikataba ya mikopo ya kugharimia miradi husika bado ni hai!

Sasa kwa nini miradi imesimama, haiendelei kutekelezwa wakati mikataba ya project funding (construction phase) bado iko hai? Je, mikataba ya mikopo husika iliandaliwa kutegemea uhai wa mwendazake? Kwamba project funding phase inge-cease immediately baada ya Magufuli kufaariki dunia!? Inakuwaje baada ya kifo cha mwendazake mikopo ya miradi imedorora kiasi cha serikali kushindwa kuhitimisha miradi kama ilivyokuwa imepangwa?
 
Ni kwasababu sisi raia , tunatafuta mlinganyo , huku tukishambulia kila anachokifanya Mama, tukisema hakikufanyika awamu iliyopita na maisha yalikuwa poa.

Na kwakua Mama nae sio mkaa kimya sana, anaamua kuumwaga ukweli, ili tusikie , ingawa haisaidii.
Sawa Ila Unaemsema Hana Uwezo Wa Kujitetea Tena Je Tuta Amini Vipi Kama Ni Kweli Anayosema Kwamba Awamu Ya 5 Ilikopa Kwa Siri, Hayo Ni Maneno Ya Kufurahisha Jamii Wakati Kuna Mambo Mengi Ya Kufanya Kama Nchi.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
kata kama mama yako kama ataongoza familia yenu huo ni msiba.

hata katika Mitume wote waliotumwa na Mungu hakuna mwanamke.

Mungu sio mjinga
Jamhuri haina dini. Mambo ya kiimani haiyafuati.
 
Yeye yuko wazi tunatekeleza kwa mikopo full stop.. Sio tulidanganywa tutembee kifua mbele eti tunajenga kwa pesa zetu z a ndani kumbe ni mikopo.. Je umeelewa sasa?
Basi mikumi tena kwake...
 
Sijui iwapo cognitive competence ya Sasha iko sahihi. Miradi iligarimiwa na fedha za mikopo. Sawa! Lakini miradi haijakamilika na inaonekana serikali imeishiwa fedha za kukamilisha miradi hiyo wakati mikataba ya mikopo ya kugharimia miradi husika bado ni hai!

Sasa kwa nini miradi imesimama, haiendelei kutekelezwa wakati mikataba ya project funding (construction phase) bado iko hai? Je, mikataba ya mikopo husika iliandaliwa kutegemea uhai wa mwendazake? Kwamba project funding phase inge-cease immediately baada ya Magufuli kufaariki dunia!? Inakuwaje baada ya kifo cha mwendazake mikopo ya miradi imedorora kiasi cha serikali kushindwa kuhitimisha miradi kama ilivyokuwa imepangwa?
Tunaenda Kuijenga ZENJI..

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mawee kwahiyo huko marekani wamesaini mikataba ambayo utekelezaji wake ni wa mashaka.

Aisee. Duuh.
 
Yeye yuko wazi tunatekeleza kwa mikopo full stop.. Sio tulidanganywa tutembee kifua mbele eti tunajenga kwa pesa zetu z a ndani kumbe ni mikopo.. Je umeelewa sasa?
Huo uwazi mpaka sasa haujafanikisha kutekeleza mradi wowote ulioanzishwa.

Zinahitajika fedha na sio maswala ya kuambiana uwazi.

Kama wamekwama pia wawe wawazi tujue kama Taifa kuwa hiyo miradi haitakaa ikamilike.

Wasiendelee kutuficha wakidai kuwa wapo wawazi.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza na Tido Mhando wa Azam TV, leo Mei 4, 2022

RAIS SAMIA: HAKUNA FUNDI WA URAIS, HAUZOELEKI
Rais Samia Suluhu Hassan amesema nafasi ya Urais haizoeleki kwa kuwa kuna mambo mengi.

“Sidhani kama kuna mtu anaweza kusema ni fundi katika nafasi ya Urais, labda kama mimi ni mgeni kwa kuwa nina mwaka mmoja.

“Nilipoteuliwa kuwa Rais mshtuko ulikuwa tukiola msiba haikuwa Urais kwa kuwa nilikuwa Makamu Rais kuna mambo nilikuwa nayajua,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.

SAMIA: TULIKOPESHWA FEDHA ZA MIRADI MIKUBWA
Rais Samia amezungumzia miradi mikubwa ambayo ilikuwa ikitekelezwa wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli kwa kueleza kuwa alikuwa akiijua lakini changamoto ni kwa kuwa ilikuwa ikiendeshwa kwa fedha za mikopo.

“Miradi ilikuwa ya kwetu kwa kuwa nilikuwepo katika Awamu ya Tano na nilikuwemo katika mipango na utekelezaji, changamoto ni ukubwa wa miradi na uwezo wetu wa ndani.

“Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje? Lakini ni miradi yenye tija,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.

SAMIA: SAFARI ZINA FAIDA, LAZIMA TUTOKE TUKATAFUTE
Rais Samia amezungumzia kuhusu safari zake za nje ya nchi kwa kusema kuwa anatoka kwa kuwa safari zina faida nyingi kwa nchi ikiwemo kufungua biashara.

“Wanataka tujifungie hapa afu walie ukata mifuko ipo mitupu, sina miujiza ya kujaza mifuko yao, lazima tutoke tukatafute.

Wafanye tathmini za safari zenyewe, kila ninapoenda ninakuwa na wafanyabiashara, mfano nilikuta vikwazo 64 Kenya na vyote tulitatua baada ya kuzungumza,” Rais Samia akizungumza na Azam TV.

Ameongeza kuwa safari zake za Marekani amesaini mikataba ambayo kama itatekelezwa Tanzania itaingiza Tsh. trilioni 11.

RAIS SAMIA: NITAWATAJA WALIOCHANGIA BILIONI 7 ZA ROYAL TOUR
Rais Samia Suluhu amesema kupitia vipande vya kuitangaza Filamu ya Royal Tour ambavyo vimekuwa vikirushwa kwa miezi mitatu sasa zimeleta faida kubwa ambayo ni zaidi ya kiasi kilichotumika kuandaa filamu hiyo.

Tsh. Bilioni 7 zilitumika kuandaa filamu huku Serikali ikisema zilitokana na michango ya wadau mbalimbali

“Ni fedha nyingi lakini faida zake zikianza kuingia wataona, kuhusu waliochangia juzi Arusha niliwashukuru kwa ujumla lakini nitawataja tu,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.

RAIS SAMIA: TUTAFUTA KODI YA MAFUTA YA KULA
Baada ya mafuta ya kula kupanda bei Rais Samia Suluhu ameelezea kilichotokea na njia inayofuata ni kuondoa kodi ya mafuta ghafi yanayotoka nje.

“Mwaka 2020 mabadiliko ya tabia nchi hatukufanya kilimo vizuri, bajeti ya 2019/20 tulipandisha kodi ya mafuta yanayoitwa crude ambayo hayakuwa na kodi.

“Mafuta yakawa hayaingizwi, nazi na chikichi hazikutosheleza soko, hivyo bajeti inayokuja tunaenda kupitia mfumo wote wa kodi, tutaondoa kodi ya mafuta ya kula ili walete crude oil tuichakate tupate mafuta tuyasambaze ndani,” Rais Samia akizungumza na Azam TV.

04 May 2022

KWA UREFU : Maongezi ya ana kwa ana kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando.

Source : Azam TV
 
Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje?
[emoji15][emoji15][emoji848] Tuachane na hilo la pili kwamba itaendeleaje.. Maana hata yeye hapa anatia shaka..! Sasa tuje kwenye tafsiri ya 'fedha zetu Lakini tulikopeshwa'[emoji848]... Kikiwa chako ni chako huwezi ukakopeshwa na yoyote yule bali unaweza kukopesha.. PERIOD!
Peas iliyojenga miradi mikubwa ilikuwa ni ya MIKOPO MIKUBWA YA SIRI isiyojulikana masharti yake
Utatumia Fedha zako za ndani halafu unadai umekopa?? Hapo ndiko Kwene shida!!!
Fedha ndani akizikuwa akitumia Mwendazake ilikuwa ni DHULUMA KWA WAFANYI BIASHARA. WANASIASA WA UPINZANI NA MIFUKO YA PENSHENI. Ndiyo maanacreport ya CAG imesema MIFUKO ya PSSSF na NSSSF iko mashakani!! MIFUKO hii inaidai SERIKALI Trillions of Tshillings.
Mama aseme ukwelu tu!!
 
Sijui iwapo cognitive competence ya Sasha iko sahihi. Miradi iligarimiwa na fedha za mikopo. Sawa! Lakini miradi haijakamilika na inaonekana serikali imeishiwa fedha za kukamilisha miradi hiyo wakati mikataba ya mikopo ya kugharimia miradi husika bado ni hai!

Sasa kwa nini miradi imesimama, haiendelei kutekelezwa wakati mikataba ya project funding (construction phase) bado iko hai? Je, mikataba ya mikopo husika iliandaliwa kutegemea uhai wa mwendazake? Kwamba project funding phase inge-cease immediately baada ya Magufuli kufaariki dunia!? Inakuwaje baada ya kifo cha mwendazake mikopo ya miradi imedorora kiasi cha serikali kushindwa kuhitimisha miradi kama ilivyokuwa imepangwa?
Mradi gani hauendelei? Umelewa chimpumu nini?
 
Ninachomkubali huyu mama ni msema kweli, kuna jitu liongo eti lenyewe likawa linajiita ati msema kweli mpenzi Mungu, kumbe ni liongo namba moja.
 
hivi kweli mijianaume na midevu yetu tumekaa mwanamke ndiye anaenda kututafutia ?

vya kutafuta ni vingi na mama hajaweka wazi anaenda kutafuta nini sisi tukae tukenue meno tu ataleta
Hata kama unamchukuia huyo ndio Command in Chief, pimbi wewe.

FB_IMG_1636980250441.jpg
 
Back
Top Bottom