Lissu anaonekana amekosea kujibu kwasababu amejitofautisha na mazoea yetu, Msigwa kuhamia CCM ni maamuzi yake, na lazima yaheshimiwe.
Kumponda Msigwa ni kwa wale wasiojiamini, siasa za kizamani, sio lazima kufanana na Msigwa anaemponda Mbowe kila siku, cheap politics.
Kama unajiamini, utamsifia ukijua fika bado una silaha za kutosha kumpiga mpinzani wako.
Maswali mengine kuhusu matumizi ya pesa naona ni kujichanganya tu, na kumuingiza Mbowe personally kwenye hilo suala ni udhaifu na unathibitisha mambo kadhaa;
- Viongozi wengine wote wa CDM na KK wanamuogopa Mbowe.
- Wote wanalinda uozo wa Mbowe kama upo. Hawa kwa mtazamo wangu wote ni dhaifu.
So, niwakumbushe wale wenye mahaba kwa Lissu, hamuwezi kumpamba Lissu wakati huu kwa kumponda Mbowe, hao wote wapo kwenye chungu kimoja, kama mnamuona Lissu clean sana, ashauriwe aondoke CDM kwa wachafu.
Lakini sio aendelee kubaki Chadema huku mkihangaika kumponda Mbowe, wakati Lissu mwenyewe yupo kimya kumhusu Mbowe!.
- Mahaba yenu kwa Lissu yamepitiliza mpaka mmeamua kuwa wasemaji wake, tena kwa mambo ambayo hajawatuma!, very funny!.
Kama Lissu anajua mabaya ya Mbowe kama wafuasi wake mnavyoyajua {sijui mmeyajulia wapi anyway}, na hafanyi chochote, basi kwangu Lissu ni muoga na dhaifu, tofauti na mnavyompamba.