Interview za Lissu zinaacha maswali mengi kuliko majibu

Mfukuzeni basi Lissu kama mnaweza muone. Mbowe apumzike kwa heshina na Lissu aambiwe arudishe fomu ya makamu acnukue ya m/kiti. Makamu achukue Heche au Lema. Mnyika amsusa ukatibu kwa sababu Mbowe anafuja pesa za jana huku anaona, Mnyika ni smart hataki kusema tu. Mrema aondoke pale kama anaweza agombee na yeye vyeo ndani ya chama vya kupigiwa kura. Mkimfukuza Lissu atawataja washenga wa Abdul ndani ya chama Kwa umma.
 
anajitahidi sana kujitenga na uovu, udhaifu na rushwa iliyokithiri anayo ilalamikia sana ndani ya uongozi wa chadema huku akijua fika na yeye ni miongoni mwa viongoz waandamizi muhimu ndani ya Chama hicho...

ama kweli nyani haoni kundule 🐒
 
Ukifahamu kwamba Lissu ni mwanasheria Nguli hutokuwa na shaka kuhusu chochote anachozungumza.
 
Lissu anaonekana amekosea kujibu kwasababu amejitofautisha na mazoea yetu, Msigwa kuhamia CCM ni maamuzi yake, na lazima yaheshimiwe.

Kumponda Msigwa ni kwa wale wasiojiamini, siasa za kizamani, sio lazima kufanana na Msigwa anaemponda Mbowe kila siku, cheap politics.

Kama unajiamini, utamsifia ukijua fika bado una silaha za kutosha kumpiga mpinzani wako.

Maswali mengine kuhusu matumizi ya pesa naona ni kujichanganya tu, na kumuingiza Mbowe personally kwenye hilo suala ni udhaifu na unathibitisha mambo kadhaa;

- Viongozi wengine wote wa CDM na KK wanamuogopa Mbowe.

- Wote wanalinda uozo wa Mbowe kama upo. Hawa kwa mtazamo wangu wote ni dhaifu.

So, niwakumbushe wale wenye mahaba kwa Lissu, hamuwezi kumpamba Lissu wakati huu kwa kumponda Mbowe, hao wote wapo kwenye chungu kimoja, kama mnamuona Lissu clean sana, ashauriwe aondoke CDM kwa wachafu.

Lakini sio aendelee kubaki Chadema huku mkihangaika kumponda Mbowe, wakati Lissu mwenyewe yupo kimya kumhusu Mbowe!.

- Mahaba yenu kwa Lissu yamepitiliza mpaka mmeamua kuwa wasemaji wake, tena kwa mambo ambayo hajawatuma!, very funny!.

Kama Lissu anajua mabaya ya Mbowe kama wafuasi wake mnavyoyajua {sijui mmeyajulia wapi anyway}, na hafanyi chochote, basi kwangu Lissu ni muoga na dhaifu, tofauti na mnavyompamba.
 
Unataka ajibu kitu kisichomuhusu?
Alishasema yeye sio mmoja wa watia saini wala hahusiki na kamati ya fedha
Makamu mwenyekiti ni mwenyekiti wakati mwenyekiti hayupo. Mwenyekiti lazima awe na taarifa zote za chama.
 
Ni Maswali mengi kwa wale tu wasio na uelewa wa majibu yake au kama kuna namna ambayo mwenye kujifikirisha hayo maswali anataka kuyatafuta maswali hayo kichwani mwake... binafsi sijayaona hayo maswali...
 
katika watu ninaowakubali ni Lissu. tuwe wakweli Lissu akiingia CCM atakua ahajimaliza kisiasa na kiakili. CCM atachie sisi
 
Lissu ni kiongozi mkubwa ndani ya Chadema baada ya Mbowe anafuata yeye.

Ungefuatilia mahojiano baina ya John Mrema na Kikeke haya mswali ya fedha yaliulizwa na kujibiwa vizuri sana.Inashangaza Makamu Mwenyekiti hawezi kujibu anamsukumizia Katibu Mkuu ?.

Tatizo la Lissu anataka kujibrand tofauti na chama chake,lakini wakati huo huo anataka chama hicho hicho kimpatie nafasi ya kugombea uRais !.
 
Watu waliokuwa organised kila mtu ana mamlaka yake. Siyo ya tawala za kidikiteita kama samia anaingilia kila muhimili wa dola. Mnyika ndiye mtunza nyaraka za chama, ripoti zote ziko kwa Mnyika. Ukitaka nyaraka yoyote lazima upate kibali cha Mnyika. So it is right kumuuliza Mnyika!
 
Ni mimi nimeona hivyo kwamba anataka kujiinua zaidi yeye kuliko chama anasahau kwamba chama ndiyo kimejenga mizizi mpaka ngazi ya msingi na kwamba bila chama yeye si kitu. Asipochukulia tahadhari jambo hili litamshinda kwani anawakwaza watu wengi sana (wafuasi, wanachama na wapenda mabadiliko) halafu baadaye wataanza kumsingizia M/kiti Mbowe.
 
Na inaonekana yeye na Msigwa lao moja. Ana kigugumizi sana kumzungumzia Msigwa tofauti na wengine wengi waliohama kama akina Dr Slaa n.k.....

Hata ule mgogoro wa Iringa aliuingilia kumuokoa rafikiye Msigwa. Kuna mengi nyuma ya pazia na muda ni mwalimu mzuri.
 
Ukweli daima ni muhimu na ukweli Watanzania wengi hawapendi wanapenda usanii katika masuala ya msingi.
 
Ndg.Lissu atuwekee CCTV FOOTAGE ya tuhuma zake za kutaka kuhongwa....pale nyumbani kwake ana CCTV CAMERA...
Hivi unafikiri anatoa tuhuma hizi bila ushahidi usiotia shaka? Wakati ufaao kila kitu kitawekwa hadharani. Huwezi ukaweka silaha zako hadharani.
 
Nikuweke sawa kuwa alisema alikuwa muhimu kipindi yupo CDM ila si kwa sasa. Kuhusu matumizi mabaya ya fedha za chama amesema yakuwa anaehusika kujibia hayo ni katibu kutokana na kanuni za chama
Nakubaliana na wewe mkuu nami nimesikia hivyo
 
Kuhusu masuala ya fedha Lissu yuko sahihi kabisa,tuhumu za matumizi mabaya ya fedha ni tuhuma nzito sana hazitakiwi kujibiwa kwa maneno matupu bali kwa vielelezo vya nyaraka ambazo Lissu anasema zipo lakini kikanuni za chama mwenye kuweza kuzitoa ni Katibu Mkuu. Na mara nyingi Lissu amesema ni vema hizi tuhuma zijibiwe tena kwa vielelezo ili kukisafisha chama. Ni wakati sasa Katibu Mkuu akisafishe chama kwa nyaraka na vielelezo ili haya maswali yasiendelee kuulizwa. Ukimlaumu Lissu kwa kutotoa maelezo ya tuhuma za fedha ni kumuonea,kumbuka Lissu ni mwanasheria ndiyo maana anasisitiza suala hili lijibiwe kwa vielelezo.
 
Nikuweke sawa kuwa alisema alikuwa muhimu kipindi yupo CDM ila si kwa sasa. Kuhusu matumizi mabaya ya fedha za chama amesema yakuwa anaehusika kujibia hayo ni katibu kutokana na kanuni za chama
Asante kwa kuliweka hili vizuri..nami nilisikia na kulielewa hivyo..ila nami niseme siku hizi kama simuelewi elewi mkuu sana Ngongo ..upo hasi kidogo na Mh Lissu, ..jaribu kurejea michango yako humu
 
Mimi naona amejibu maswali vizuri kabisa na siyo ya kukibagaza Chadema.
 
Mleta mada alitamani Lissu amsafishe mwenyekiti au apige propganda za kudai kuwa ndani ya CHADEMA kuko safi.

Akifanya hivyo itakuwa ni kuwasafisha wapiga dili na mafisadi waliomo ndani ya CHADEMA kwa sabuni nzuri ya bure!.

Wacha aongee hivihivi ili chama kipigwe pressure ili kichukue hatua, na kikichukua hatua kitapata baraka za umma.

Lakini hii ya kutaka kuisema CCM huku ukifumbia macho ufisadi ulio katika chama chako mwenyewe umma hauwezi kukuchukulia serious
 
Tukubali tukatae mkiti wetu si salama kivile upande wa pesa ya chama, mengine tunafunika kombe
Hizi fikra zinasababishwa na wanaohusika kutotoka na kujibu maswali haya kwa ufasaha na kuweka hesabu zilizoandaliwa kitaalamu na kukaguliwa kwa uwazi ..

Inawezekana mwenyekiti Freeman Mbowe hana shida yoyote. Lakini kitendo cha ubaridi na ubabaishaji wa kukalia taarifa na kuacha mambo kusemwasemwa tu bila ukomo, kinaharibu sifa ya chama..

Kama ziliibwa au zimetumiwa vibaya na watu fulani, ni kwanini hao watu walindwe? CHADEMA inapaswa kuonesha mfano kwa vyama vingine kama CCM kwa kutowavumilia wanaotumia pesa vibaya kwa kuchukua hatua stahiki na za wazi dhidi ya watu hao..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…