Interview za TRA hazijatenda haki

"Haki itendeke watoto wa maskini tunaendelea kusota"..

Mkuu pamoja na kuwa na kibarua ila bado una victim mentality. Unachokisema kina ukweli ila usipende kujitilisha huruma "kimaskini" kwa sababu in reality, nobody cares
In reality.. it hurts. Kwasababu wanatuambia kabisa mi dad wangu yuko huko so either way ntapita tu. Kongole kwao ila tusio na dads huko nani anatusemea. So tusiseme kwasababu it sounds like a victim mentality? Isn’t it a reality thou? It being worthy of being an issue or not is not my case to solve but the truth has to be spoken
 
I'm telling you this as a person who passed through a lot of shi*t kutengeneza hata vissibility niliyonayo sasa kwa watu. Hakuna aliyejali maumivu au mental damage niliyoipata. That's how the world operates

Kama unaona wivu kwa hao watu, make sure wewe unakuwa the next "Dad" Na kama unataka haki. Unaweza kuidai pasipo kujidogosha ili kupata public approval or sympathy.
 
Nimekuelewa ila tujikite kwenye mada husika mkuu. Sasa wivu ntamuoneaje mtu ambae siwezi kua nae sawa. I wasn’t asking for sympathy natetea haki. Ndo maana sijaonba kuonewa huruma nimeomba haki itendeke.

Hope hilo limekaa sawa
 
Hili la TRA ni Moja ya matatizo makubwa kwenye mfumo wa ajira yanayopuuzwa.

Tumuombe Rais Samia arudishie michakato ya ajira sekretarieti ya ajira, bila hivyo mengine yatakuwa simulizi ya kutisha sana mbeleni
Acha mkwara pasua paper wewe pata 100% then uwekewe sifuri tuone.
 
"Haki itendeke watoto wa maskini tunaendelea kusota"..

Mkuu pamoja na kuwa na kibarua ila bado una victim mentality. Unachokisema kina ukweli ila usipende kujitilisha huruma "kimaskini" kwa sababu in reality, nobody cares
Hii slogan ya watoto wa maskini ni ya kipuuzi sana kaza msuli mtoto wa maskini ndiye anayetakiwa kupasua kweli kweli.
 
ingekuwa halmashauri usingeomba irudiwe
 
Umesoma ulichoandika hapa?? Unaweza muajiri mtu wa Phd kwenye office yako,?, Ila umemuajiri kwa qualification yake ya ordinary diploma? Basi utakuwa zuzu
 
Umesoma ulichoandika hapa?? Unaweza muajiri mtu wa Phd kwenye office yako,?, Ila umemuajiri kwa qualification yake ya ordinary diploma? Basi utakuwa zuzu
Inawezekana kabisa kama degree ....sasa kama kaapply kwa kutumia cheti cha chini!?

Tofautisha overqualified and irrelevant qualifications....Wapo watu wa masters wameomba nafasi za degree na wameanza kama officer II maana wao ndio wameapply hawakulamishwa , makubaliano watalipwa kulingana na level yao ya degree hiyo Masters ni added advantage kweny kupata daraja huko mble.



Nafanya kazi na madogo wamesoma Masters weng waliunga ila wameapply kazi za degree na wanapiga mzigo kama officer II kama makubaliano ya Tangazo la kazi.
 
Mkuu, qualification si ni kuwa na sifa za chini zilizotangazwa? Huyu mwenye masters kama ana diploma na ameombea kazi kwa diploma bado anakua na qualification, na hata angeombea kwa cheti cha masters kama inahusiana na kazi hiyo, bado anastahili kupata kazi hiyo.

Sanasana, mwajiri unaweza kutompa nafasi mtu huyo kwa mtazamo wa kuwa hatafanya kazi kwa kuridhika na kwa ufanisi kwa sababu mshahara atakaoupata ni chini ya kiwango cha elimu yake, sio kuwa unamkosesha kazi kwa kutokuwa na qualification - wakati ameshapita kiwango cha chini (minimum) ulichokisema.

Kwa fikra zako mkuu, unamaanisha kama kazi hiyohiyo ya Diploma wakasema ufaulu ni kuanzia GPA ya 3.0 mfano, wakaomba 5 wote wenye diploma ila wawili wakawa na GPA ya 3.5 na waliobaki wana 3.0 basi hawa wenye 3.5 hawatastahili kwa sababu wapo waliogonga mulemule mlimotajwa na mwajiri (3.0)
 
Umesoma ulichoandika hapa?? Unaweza muajiri mtu wa Phd kwenye office yako,?, Ila umemuajiri kwa qualification yake ya ordinary diploma? Basi utakuwa zuzu
Mkuu, hapa wewe ndio unaonekana zuzu. Kwa nini usimuajiri ilhali ameomba kazi kwa kufuata tangazo lako na ametimiza vigezo vya chini vilivyopo kwenye tangazo lako la ajira? Qualification ni kuwa na vigezo au sifa za chini za kazi inayotakiwa, kuwa na zaidi sio tatizo ila kuwa chini ya sifa ya chini iliyotanganzwa, ndio tatizo
 
Mkuu naona unaitamani sana TRA 😊😊😊mkuu nikwambie kitu Bora uwe TRA wa MAISHA yako......
 
Ingawa sheria zetu za kazi zinasema ili mtu ashtaki chini ya sheria za kazi ni lazima kuwe na uhusiano wa mwajiri-mwajiriwa,

Jambo kama hili linafaa kabisa kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kazi. Mwajiriwa mtarajiwa anakua amekosewa kwa kunyimwa fursa, ni kama vile mchezaji wa soka anavyochezewa rafu ndani ya 18, huwa timu inaadhibiwa kwa kumkosesha fursa ya kufunga bila kujali kuwa huenda asingechezewa rafu angekosa kufunga labda kwa kupiga mpira nje au kupaisha nk
 
ukiwa hauna watu,mambo mengi utayaona magumu,,,,
Kazana sana katika sala wakati wako wa kufanikisha ukifika ndio utaelewa
Mama mzazi aliwai nambia hii kauli niliona kama siku zinachelewa sanaa.....hapo madogo form four failure na marafik wa mdogo angu walikua wanakuja home kwetu na ndinga zao Kali....nikawa Ile state ya kupoteza Kila kitu ulicho kipambania maishani...

Nilisoma kitabu Cha zaburi Kuna sura 150 Kwa miezi mi tatu asubh na jion na kutafakari sanaaa Bado sikufanikiwa chochote.... Muda wa MUNGU ni sahihi nilisha sahau yotee wasife moyo vijana...
 
Sanasana, mwajiri unaweza kutompa nafasi mtu huyo kwa mtazamo wa kuwa hatafanya kazi kwa kuridhika na kwa ufanisi kwa sababu mshahara atakaoupata ni chini ya kiwango cha elimu yake
Na hili ndiyo jibu sahihi, kabisa
ila lazima watafute kichaka cha kujifichia ambacho ni over-qualification

mwenye Masters aki-apply nafasi ya Diploma, jua huyo anafanyia shida(njaa) na waajiri wanajua hii vizuri sana, akipata kwengine kwenye kuhitaji Masters anachomoka chap, mwajiri anaingia gharama tena kuita mchakato wa interviews

mimi nigekuwa mwajiri ningekwepa pia, hakuna mwajiri mwenye akili timamu akafanya hivyo
 
naaam mkuu ahsante sana kwa maneno ya kutia moyo kiasi hiki,,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…