Habari wakuu.
Lalamiko nilaloleta mahali hapa ni kwanini TRA iitishe interview, iruhusu watu wafanye alafu mtu unafaulu kwa marks zaidi ya tisini unaambiwa una irrelevant qualification za kuendelea na mchakato wa kufanya oral interview.
Ina maana hadi wanakuita uje ufanye interview hawakujua kwamba una irrelevant qualifications?
Mtu unakopa pesa ili uweze kufika mkoa ambao umeitwa kwenda kufanya Interview maana interview inakukuta kwenye vibarua vya watu unapambana kujitolea alafu unafika unapambana kusoma usiku na mchana unajiandaa vizuri unaingia kwenye mtihani unafanya vizuri unafaulu kwa marks za juu kabisa alafu unakuja kuambiwa umefaulu lakini hujachaguliwa kwakua una irrelevant qualifications? Kwanini mliita mtu in the first place?
INTERVIEW IRUDIWE ILI HAKI IWEPO. MCHAKATO MZIMA WA
INTERVIEW URUDIWE, WATANGAZE UPYA ILI WATU WAOMBE UPYA NA WENYE QUALIFICATIONS HUSIKA WAOMBE NA MUWACHAGUE KWA HAKI NA USAWA. WAHANGA NI WENGI SANA NA INAUMIZA.
NAOMBA TRA WARUDIE MCHAKATO WA INTERVIEW ILI WALIOKOSESHWA KWENDA KWENYE ORAL KWA KIGEZO CHA IRRELEVANT QUALIFICATIONS HATA KAMA WANA MARKS KUBWA NAO WAITWE WAFANYE TENA INTERVIEW.
Haki itendeke watoto wa maskini tunaendelea kusota.
Nimeambatanisha na mfano wa uonevu huo uliotendeka.
Na TRA mlipotaka kufanyisha interview nyinyi wenyewe hiki ndo mlitaka kufanya? Haki itendeke mchakato urudiwe
Ndugu inaonekana uliweka matumaini makubwa mnoo kwenye hizi post.(wenzako hatufanyi hivyo)Alafu kusoma chuo cha kodi haina maana waliosoma vyuo vyengine unawazidi academically kwenye hio kodi na pia haina maana lazima uajiriwe TRA relax.
Hii ndio maana ya interview Kuna watakaopita na watakaodondoka, ukidondoka unasimama tena unaendelea na mapambano ndivyo tufanyavyo wenzako.
Ngoja nijaribu kukujibu japo najua unaweza usinielewe maana inaonekana una hasira.
Kwanza elewa TRA hawawezi kukutema tu hata kama wanataka kukuonea bila kukutaftia sababu(tukipata chance nyingine tusiwape sababu).Watu kama watatu waliotemwa na nawajua na wamepata marks za kuitwa, wote wamesoma Banking finance ambao hawa hawajasoma kabisa tax kipindi chote cha masomo!!!na wote kwenye kujaza ile form wakati wa maombi waliandika wamesoma finance wakaishia hapo na ndio maana system ikawapitisha.
Lakini siku ya paper ya written wasimamizi wakati wanawakagua vyeti wakaona ni banking finance wakawaletea noma maana hawa watu hawajasoma tax,lakini wakawaruhusu wakafanya Pepa nadhani kwa ajili ya kufatilia zaidi maana waliambiwa waandike majina yao pembeni.
Sasa mtu hajasoma tax kabisa na kaongopea mfumo umemuita na pepa akafanya fresh unamuita aje afanye nini?? Unadhani kama wangekua na nia ya kuwatema kwa kuwaonea si wasingemundikia 90% wangemwandikia tu 32% wakaachana nae.!!!!kuandika exactly marks tu hapa inaonyesha jinsi gani waliosahihisha na wasimamizi wa mchakato mzima wako makini na fair.
Kama unaona umeonewa na hakuna sababu ya kuonewa, nenda kwenye office zao kawasilishe hayo malalamiko direct mda bado upo, hata utumishi huwa wanakosea na watu wanaenda na wanatoa majina ya nyongeza,kulia lia hapa HAITAKUSAIDIA CHOCHOTE.
Nadhani tulioshindwa kupita kwa next stage tujifunze kuheshimu waliofaulu zaidi yetu na kubwa zaidi tujifunze wakati wa Mungu ni wakati sahihi zaidi.