Sio majivuno ya kishamba.
Ally ana limited exposure kwenye mambo mengi ukijumlisha na shule ndogo unaona kabisa tatizo alilonalo.
Mtu anaweza kua na shule ndogo ila akawa na expisure kubwa kama Diamond, lazima atabadilika na uwezo wake wa kuelewa mambo utapanuka. Hata waswahili husema kuzaliwa mjini ni sawa na kusoma form six, sio kwamba mjini kuna elimu ya bure, hapana, exposure inayotokana na mazingira ya mjini sio sawa na bush.
Ally ni mswahili na hataki uswahili umuache, hakuna tofauti kati ya Ally na Hamorapa, wote wana majina makubwa ila limited exposure.
Sio kwamba Ally anaringa, hapana, ni ushamba ukijumlishwa na uelewa mdogo wa mambo kuhusiana na hadhi yake.
Ushamba ni mzigo.