iPhone 12 haitokubali spare hata kutoka kwa iPhone nyingine

iPhone 12 haitokubali spare hata kutoka kwa iPhone nyingine

Haya mzee umeshinda.

Turudi kwenye jukwaa la Manchester United. Tueleze kwanini Ole bado anatakiwa andelee kuaminiwa.
Mkuu mbona umekubali kirahisi hivi hahahah,tuendeleze kushusha nondo...Tunaofaidika ni sisi
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] kwahiyo unanunua simu unaenda kutunza halafu unasubiri chaja? Au mimi ndio sielewi

hapana utatumia hii ya kawaida lightening au ya mwaka uliopita kama uko nayo.

ila ukitaka ya mwaka huu ujue utatoa pesa baki.
 
Aisee huu mjadala unapendeza sana. Watu wanashusha data tu na wengine tunafaidi. Hii ndio jf sasa, sio ile ya kina wasafi na kiba.

Swali nalojiuliza mpaka sasa ni kuwa, iwapo simu inakuja bila chaja wala earphone hivo vitu unavipataje na kwa gharama ya nani na kiasi gani?

Nina swali lingine kutegemea na jibu la kwanza
ndiyo. zinakuja na usb tu
Na kuongezea usb inayokuja na iphone 12 ni type C wakati charger za zamani za Iphone ni Type A (unless ulinunua pro charger zamani) hivyo hutaweza kutumia huo waya wako kwenye chaja ya zamani unless ununue dongle ama ununue charger mpya.
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Mkuu mbona umekubali kirahisi hivi hahahah,tuendeleze kushusha nondo...Tunaofaidika ni sisi
Nimechoka ku debate.

Hakuna atakachoelewa.

Hadi mabosi wa nokia walishanyoosha mikono 2009 manake walikuwa wanapokea kipigo toka 2007.
 
Nimechoka ku debate.

Hakuna atakachoelewa.

Hadi mabosi wa nokia walishanyoosha mikono 2009 manake walikuwa wanapokea kipigo toka 2007.

mkuu hapa ndipo unafeli nawewe.

nokia imekufa kwa ujinga wa viongozi wake wala sio ushindani.alieuwawa na ushindani bila kupepesa macho ni blackberry.kwa wakati ule hakuna kampuni iliyokuwa kubwa kama nokia. alikuwa na uwezo wa kufanya kila analotaka ili andelee kuwa juu,ila hakuwa tayari.
 
Nimeona review simu hizi mpya za iPhone 12 kuwa hata ukichukua kioo ukakibadiisha ukakiweka kwenye simu nyingine kama hiyo hiyo, kwanza ukiiwasha haitowaka unless uiwashe kwa kuplug in charger.

Ikishawaka itakuletea msg kuwa umeweka kifaa ambacho siyo cha simu hiyo, face id haitofanya kazi na mambo mengine.

Mfano ukibadilisha betry utakumbana na dhahama kama hiyo. Vifaa kama logic board au cameera, camera itakuwa na mawenge wenge, haitopiga picha ikifunguka itaganda yani naona ile mambo ya kununua simu zenye iCloud kwa ajii ya spare wanataka kuziondoa.

Ila hawa jamaa nahisi kifo chao kiko kwenye kona, yani unaship vipi simu haina charger wala earphone eti unapunguza uchafuzi wa mazingira.
Tatizo hilo lipo hata kwa Samsung galaxy note 20 upande wa battery na vitu vingine vichache
 
Wakuu iPhone 11 Kwa sasa Dukani mpya bei gani...?

Maana Wife kanikalia kooni hatarii
 
Asantee Kaka Mkwawa sema Je...?
Nawezaje kutambua Original na Fake asee...?
Ukinunua kwa wakala ama duka kubwa hutokuwa na hofu ya kuuziwa fake.

Pia iphone ambayo ni fake haiwezi kuwa na service yoyote ya Apple, haitakuwa na icloud, Itunes, App store, Appke tv, arcade etc. Jaribu kulogin kwenye service yoyote kati ya hizo kuverify kama itakukubali.
 
Sawa mkuu nimekupata.
Hii kitu effect yake tutakuja kuiona miaka kama mitatu mbele baada ya simu zinazotoka leo kuanza kuharibika haribika na pia baada ya refurbrished zake kutapakaa sana Tanzania. Wasiwasi wangu ni wabongo wangapi wataweza kufunga only genuine spare parts za iphone mfano ikiharibika??
Anyways lets pray and hope China people will find a way around this as they always do
Kwaio kuweka spare parts zingine inawezekana sema tu ndo vile inabidi hicho kifaa kiwe OG kisowe cha replacement toka kwenye simu ingine?
 
mkuu hapa ndipo unafeli nawewe.

nokia imekufa kwa ujinga wa viongozi wake wala sio ushindani.alieuwawa na ushindani bila kupepesa macho ni blackberry.kwa wakati ule hakuna kampuni iliyokuwa kubwa kama nokia. alikuwa na uwezo wa kufanya kila analotaka ili andelee kuwa juu,ila hakuwa tayari.
Kuna article nimeweka link huko mwanzo inasema managemeng ya Nokia walikuwa wanafikiria kusimamisha utengenezaji wa simu kwasababu ya ushindani kuwa mkali.

Na suala la kuwa na management mbovu halikuanza hiyo 2007. Ni tatizo la makampuni mengi makubwa ya wakati huo. Na nokia wamekuwa nalo toka miaka ya 2000 mwanzoni.

Walishindwa ku adopt na ushindani wa ghafla ambao hawakujiandaa.
 
ni kwa gharama zako,zitauzwa kwa ingizo baadae sokoni.

ni zaidi ya $100.

yaani apple kwa sasa wanafanya utapeli wakijua kabisa hamna mteja wa kuhoji.walitoa eaphone wakaanza kuziuza peke yake wakapiga hela,saaa wako kwenye charger.watahamia kwenye betry muda sio mrefu.
Apple hawafanyi utapeli ni matakwa ya mazingira ya soko lao, Hakuna mteja wa iphone ambaye anapeleka simu ku repair kwa fundi. Apple customers wanapeleka simu iliyoharibika kwa dealers, dealer hAwana fake parts. Najua hii imetuuma sana wabongo, tunanunua refurbs phone, spare parts za china. Yaani ukibadilisha screen inagoma fingerptint. Ukibadilisha betery simu inakuwa ya moto. Lazima tukubali kuwa sisi sio dedicated market ya apple ptoducts.
 
siku zote mchina ataendelea kuwa upande wetu.

na hatutajihangaisha na wafamyabiashara wasiotujali,ila biashara zao tu.
 
Kuna article nimeweka link huko mwanzo inasema managemeng ya Nokia walikuwa wanafikiria kusimamisha utengenezaji wa simu kwasababu ya ushindani kuwa mkali.

Na suala la kuwa na management mbovu halikuanza hiyo 2007. Ni tatizo la makampuni mengi makubwa ya wakati huo. Na nokia wamekuwa nalo toka miaka ya 2000 mwanzoni.

Walishindwa ku adopt na ushindani wa ghafla ambao hawakujiandaa.

leo hii apple wana mafanikio sababu ya viongozi wenye maono,tokea muasisi wa hiyo kampuni.

kama uongozi mbovu umeanza kuwala nokia 2000,unakujaje kusema apple ndio aliiua nokia!!!!!
ndio sababu tunasema matatizo yao wenyewe ndio yalifanya wakapoteza ushindani,sio ujio wa apple na iphone.maana apple yupo na kampuni kibao bado zinazaliwa na kukua.
 
Na mimi nimejiuliza swali kama lako. Iwapo matatizo yalianza kabla ya ujio wa iphone, iweje sababu iwe iphone. Ni sawa na mtu kushindwa kutafuta pesa kabla hajaoa kisha akioa tuseme mkewe ndio amechangia anguko
 
Back
Top Bottom