iPhone 18 Pro Max na Ultra Yaja! Kaa tayari kwa Sept 9

iPhone 18 Pro Max na Ultra Yaja! Kaa tayari kwa Sept 9

Siyo mbaya maana maisha ni kuchagua utumie pesa kwa ajili ya Experience na Convenience au Basic Utility..

Na kila mtu ana level yake ya Basic Utilization, hatufanani aisee usiige Tembo kunya dafu......

ila shida ni wewe mwenzangu na miye mwenye Status Anxiety unaogopa kuonekana na TECNO SPARK kama miye, unayapitia mateso kumiliki vitu kwa ajili ya Prestige huku usiku unakosa usingizi kwa Financial Stress..
 
Zamani nilijua ni watu Wana wivu au Chuki za kijinga kwa Watz kuona mtu ana kitu kizuri, My friends nimeshuhudia 100%

Baadhi ya Wadada wanaopenda/ wenye addiction ya iPhone 0712 wanatoa vizuri kabisa tena wao ndio wanakushawishi kabisa
Mkuu ulishawahi kushawishiwa nini
 
Hizo labda 2030 ndio nitazifikiria..
Kwa ratiba zangu.. 2030 ndio nitanunu s26
 
iPhone user ni wakuonewa huruma kabisa kiukweli sioni kama wanatendewa haki na kampuni lao ukilinganisha na pesa wanayolipia hizo bidhaa.

Imagine juzi hapo Apple wameachia iOS 27 na moja ya feature waliyosema ni mpya ni hii.

"iOS 27 imekuja na features mpya ya volume control kuifanya simu iwe na uwezo wa kutenganisha na kudhibiti sauti ya alarm tofauti na media au ringtone."

Before iOS 27 ilikuwa kama mchana ulipunguza sauti ya simu kwa kutumia vidude vya pembeni ili usisumbue watu ofisini, hukujua kuwa umepunguza na sauti ya alarm.

Ukifika usiku unalala ukiamini alarm uliyo set ipo sawa, kumbe ipo kimya kama bismini.

Matokeo yake unakuja kushtuka asubuhi tayari umechelewa kazini au umepishana na mchongo wa maana.
Dah!yaani nakumbuka hadi samsung S6 yangu niliyotumia 2017 ilikuwa na feature hii lakini Iphone wamekuja kuitoa kwenye latest phone yao
 
Back
Top Bottom