iPhone 18 Pro Max na Ultra Yaja! Kaa tayari kwa Sept 9

iPhone 18 Pro Max na Ultra Yaja! Kaa tayari kwa Sept 9

Sahihi mkuu, nilitaka kuvuta s24 ultra ila mtu akaniambia kuchukua 14 pro max, hatimae nikaichukua. Aisee jamaa wapo vizuri sema tu upande wa multitasking ndo wamefeli kwa sehemu. Pia apps ni chache sana ukicompare na Android.
Mkuu app gani umeitafuta app store ukaikosa?
 
iPhone user ni wakuonewa huruma kabisa kiukweli sioni kama wanatendewa haki na kampuni lao ukilinganisha na pesa wanayolipia hizo bidhaa.

Imagine juzi hapo Apple wameachia iOS 27 na moja ya feature waliyosema ni mpya ni hii.

"iOS 27 imekuja na features mpya ya volume control kuifanya simu iwe na uwezo wa kutenganisha na kudhibiti sauti ya alarm tofauti na media au ringtone."

Before iOS 27 ilikuwa kama mchana ulipunguza sauti ya simu kwa kutumia vidude vya pembeni ili usisumbue watu ofisini, hukujua kuwa umepunguza na sauti ya alarm.

Ukifika usiku unalala ukiamini alarm uliyo set ipo sawa, kumbe ipo kimya kama bismini.

Matokeo yake unakuja kushtuka asubuhi tayari umechelewa kazini au umepishana na mchongo wa maana.
Kwakweli hiki kichekesho na unakuta watu wanashangilia wakiwa kwenye foleni wakisubiri kujipatia aiphoni mpya 😁😁😁
 
Sahihi mkuu, nilitaka kuvuta s24 ultra ila mtu akaniambia kuchukua 14 pro max, hatimae nikaichukua. Aisee jamaa wapo vizuri sema tu upande wa multitasking ndo wamefeli kwa sehemu. Pia apps ni chache sana ukicompare na Android.
App nyingi za ios zimenyoka mkuu hazina ma adds ya kijinga zikiwepo ni kidogo tu hawa jamaa wametulia sana,picha ndiyo usiseme nachopenda zaidi iphone ni kama dhahabu ni rahisi kuibadili kwenda pesa yani ni dakika tu unaweza iuza pasipo usumbufu naukitaka kupanda toleo la juu yake ni rahisi maana uhakika nikuongezea tu pesa
 
Ila kununua iPhone kila mwaka ni upumbavu aisee.

Halafu wala huwa hazina tofauti kubwa.

Utumwa wa kisaikolojia.

Apple ingekuwa ni kampuni ya Kitanzania, watu wangekuwa washadai inatumia waganga kupata wateja 😀.
Uko sahihi kabisa! Mimi sijui kwanini sijawahi kuwa addicted na kubadili badili simu, naona bora pesa yangu nikaiweke shamba sijui ndio ushamba au kukoswa pesa! Siku tukikutana na marafiki, simu yangu inabaki kwenye mkoba, maana wengi wao hawapitwi na trend wakiona hujabadili wanaanza kukusakama ubadili simu unakaaje na simu ya zamani🤦🏽‍♀️
 
Awali nilikua nazichukua sana simu za iphone na kuwaona watu wanaozishobokea kama hamnazo,ila banah nilipoanza kuitumia aiseh zina mvuto wa kipekee ,umasikini ni mbaya kila kitu utakosoa na kuchukia chanzo ni uhaba wa fedha
Si kweli mkuu, kwasasa kuna simu nyingi bei ghali kuliko hata Iphone, kaangalie bei ya vivo x300 ultra na Oppo find x9 pro bei zake mkasi kinoma ndio maana bongo huzioni ovyo

Hizo mashine ukiona bongo ujue mshkaji ni tech enthusiast kweli kweli
 
Back
Top Bottom