iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

Mmiliki wa cloud ni nani? Upige zako picha halafu mweingine akakutunzie? Na ili uzi access ukanunue bando kwanza.
 
Mmiliki wa cloud ni nani? Upige zako picha halafu mweingine akakutunzie? Na ili uzi access ukanunue bando kwanza.
ni apple mwenyewe na amekupa storage ya bure, dunia inahamia huko ata adobe naye na watengeneza software wengi wanahamia kwenye cloud, juzi windows katoa os inafanana kama chrome nayo ina work based on cloud, siyo jambo la kuepukika tunaelekea huko ndiyo maana hata google documents imeshika kasi now.
Its all about cloud. uzuri wake ni kwamba hutopoteza vitu vyake kirahisi mimi nina vitu vya 2015 kisa nlivisave google drive na kwenye icloud kupitia iphone. Huwezi kimbia technology waliojaribu walikufa kama blackberry alivyodhani iPhone haitofanya kazi kwasababu ina demand data sana ita crash mtandao kilichomkuta mpaka leo kabaki jina tu..
 
Aisee nilijua niko peke yangu! Mimi bora nitumie hata itel kuliko iphone!
 
Aisee nilijua niko peke yangu! Mimi bora nitumie hata itel kuliko iphone!
Naona tu watu wanavyohangaika nazo huku
Hela hawana,mabando shida,mambo ya notes na mambo mengine ni kasheshe.
 
Naona tu watu wanavyohangaika nazo huku
Hela hawana,mabando shida,mambo ga notes na mambo mengine ni kasheshe.

Yaani wanajitutumua tu ila hakuna kitu! Mimi sijawahi kuzielewa iphone kwa kweli!
 
Yaani wanajitutumua tu ila hakuna kitu! Mimi sijawahi kuzielewa iphone kwa kweli!
Ni show off tu hakuna lolote.
Hasa Hawa walionazo huku ndo kabisa,wanazo tu ili wazionyeshe na wengi wanafata tu mkumbo.
 
Huawei no..sipendi zilivyo.
iPhone na huawei ndio dimu sizipendi ajili ya muonekano wake...
Samsung nimeitumia toka naanza kutumia smartphone nishaichoka sasa kampuni hii. Nimetumia Grand prime,s4,s5,76 A10
£918
 
Mmiliki wa cloud ni nani? Upige zako picha halafu mweingine akakutunzie? Na ili uzi access ukanunue bando kwanza.
Nadhani hii point ya memory card inahitaji uafafanuzi zaidi.

Mempry card unaweza kufanya back up kwenye sehemu ambazo hazina internet, Android inaweza kufanya back ups kwenye mitandao inayotunza data kama inavyoweza iphone lakini i phone haiwezi ku back up kwa memory card.

Pia cloud storage si ya kuaminika sana, kuna kipindi i cloud ilidukuliwa picha za uchi za mastaa zilivuja na hili shambulio linaweza kutokea tena
 
Povu la omo hili [emoji16][emoji16]

Umekuja kutetea iphone wakati hata huna, Au ili tu uonekane una uchungu nayo watu wajue unayo[emoji16][emoji16]

Wenye i phone wamekaa kimya.
You sound childish.
 
Hakuna kisicho dukuliwa hata simu bila icloud bado inadukuliwa, na icloud storage as far as i remmeber imedukuliw mara moja nadhani ilikuw 2016. Lakini ndiyo maana kila mara tunapokea updates na patches kuimarisha system.
iPhone ina mambo mengi inayokosa lakini still hoja nyingi kwangu ninaona hazina maana maana haikulengwa kufanya hayo, so kosa siyo la iPhone kosa la yule anayelalamika kwa kununua kitu ambacho hakukifanyia utafiti maana ukweli ni kwamba kama mtengenezaji angekuwa kamlenga yeye angeyaweka hayo yote mbona rahisi tu.
 
Android gani hiyo ya siku hizi unayoweza kufungua na kutoa battery??
 
Mtu anahangaika na kuhamisha miziki wakati siku hizi watu wana stream apple music au spotify.

Dunia inabadilika sana. Hata sasa sioni haja ya kuning'iniza mawaya masikioni wakati kuna wireless headphones.

Na hata android za sasa kuna vingi vinaondolewa. Ikiwemo headphone jack.
 
Ip 5,6,6+ Zina sehemu ya kuchomeka earphone.
Nyimbo unadowload fresh Tuu Kwenye kila iPhone(audiomack, Spotify)
Ukinunua kitu piru unapewa na bt earbuds
I11
Kuhusu gharama NI kwako ...watu tunaaford.
Sd card slot ya Nini simu ina storage kubwa nyooooookooooooooh
Acha umama mtoa mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…