Ipi faida ya Mzee Alli Hassan Mwinyi kuwepo Dodoma kama Baba wa Taifa aliyebakia?

Wewe Mwanao angepewa Urais pengine ungeenda mbali zaid

Mwacheni Mzee wa watu akili zimruke, Jpm angeamka vibaya si angelifyeka tu jina la mwanae
Tatizo mwinyi hatakiwi kuwa mshamba wa madaraka, yeye teyari ameshakuwa rais kwa hataki kuwa na kimuyemuye na mambo madogo.
 
Kama ni mzee anafuata nini kwenye majukwaa ya siasa hadi anaongea ujinga
 
Hata alipokuwa akiongoza alikuwa anaongoza kwa mawazo ya walio nyuma ya pazia. Nyerere alimuweka maana ilikuwa rahisi kwake kumuagiza afanye atakalo.
Ni kweli, alianza kumsikiliza mkewe Mama Sitti Mwinyi zaidi ya Mwalimu. Ndipo wakati ule ambapo Mwalimu alisema “Ikulu imegeuka Pango la wanyang’anyi”, Pia “Rais Mwinyi anamsikiza mkewe usiku ndipo anafanya maamuzi asubuhi”

Wakati Mrema alipokamata dhahabu ya mama Sitti pale Airport nk
 
Mzee Mwinyi aliwahi kupigwa kofi na mwanafunzi wa madarasa way back 2012.

Sasa naanza kuelewa yule dogo alikuwa sahihi kumtandika Kofi huyu mzee.
 
“Nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba na lazima tuienzi, lakini twaweza tukitaka kuiahirisha kwa muda mfupi ili kumpa Rais Magufuli kipindi kingine kimoja cha Asante kisha baadaye tuendelee vilevile mpaka Dunia iishe, kwasababu kuna mengi aliyonayo na Nchi itayakosa” -MSTAAFU MWINYI
 
Sasa mtu anayeongea PUMBA kiasi hiki eti KATIBA IAHIRISHWE kwa kipindi kifupi anastahili kweli kupewa UBABA WA TAIFA? Mwalimu angekuwa hai asingeweza kuongea UJINGA kama huu kuhusiana na dikteta.


 
Huyu mzee ni bora hata asiwe anaongea hadharani.
 

Miaka yote hii Mwinyi amekua mbinafsi akiimba sifa ili mwanawe apitishwe na Tanganyika kuwa Rais wa Zanzibar’
Ashapata ugombea Sasa ni Bora apunguze
 
Mzee kachoka mwili mpaka akili anachoongea ni kama mtoto mdogo ambaye hajaanza shule
 
Faida yake ni mwanaye anapendelewa kwa mambo mengi, lakini hata yeye anajua ukweli kwamba huyu jamaa hakuna la maana analofanya
 
Kila mtu anao uhuru wa kufikiri na kusema atakavyo. Iwe ni mgambo, mama ntilie au rais mstaafu. Kama maoni ya mtu yakikukera unatulia unapiga malimao unatulia. Katiba hurekebishwa na bunge hivyo anachosema Mwinyi ni maoni yake tu.
 
Kila mtu anao uhuru wa kufikiri na kusema atakavyo. Iwe ni mgambo, mama ntilie au rais mstaafu. Kama maoni ya mtu yakikukera unatulia unapiga malimao unatulia. Katiba hurekebishwa na bunge hivyo anachosema Mwinyi ni maoni yake tu.
Sasa ndiyo aongee upoyoyo huku akijua influence yake kwa jamii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…