Manuell
New Member
- Aug 26, 2022
- 3
- 1
UTANGULIZI
Hivi karibuni tumeshuhudia kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mwanasiasa na mwanasheria kijana akihoji juu ya sheria inayotaka mgombea Wa nafasi za ubunge awe na umri wa zaidi ya miaka ishirini na moja, huku haki ya kikatiba ikimtaka kijana mwenye umri wa miaka 18-19 na 20 kupiga kura, hii imeinua hisia kali juu ya NAFASI YA VIJANA KWENYE SIASA NA UONGOZI.(UTAWALA)
Kabla ya kusonga mbele ni vema kujiuliza JE VIJANA WANAUELEWA GANI JUU YA MAMBO YA UTAWALA(SIASA,) vijana wengi wanauelewa finyu juu ya siasa, na vijana wachache wamejitoa kimasomaso kuingia katika uwanja wa siasa. Mara nyingi vijana hujushughulisha na mambo ya siasa pale uchaguzi unapokarribia na kwa nafasi kubwa wao hubaki kuwa wapambe wa viongozi tu na kutojaribu kuingia katika tasnia hio ya siasa hata pale uchaguzi unapoisha hii imeleta wasiwasi mkubwa juu ya nafasi ya vijana katika siasa. Wanasisa wakubwa na wakitambo wamekuwa wakiwatumia vijana kupiga kampeni zao, kuhamasisha upigaji kura lakini pindi tu viongozi wanapopata madaraka ushirikishwaji wa vijana huwa ni mddogo sana na hata wakishirikishwa basi viongozi hupendelea zaidi wale waliopo kwenye vyama vyao vya siasa huku kuacha kundi kubwa la vijana nyuma na kuona siasa kama mchezo mchafu tu au wakupena ndugu kwa ndugu na kupoteza hata hamu ya kuingia kwenye siasa.
Nini kifanyike hilo bado ni swali kwa vijana ulimwenguni kote, ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, matatizo ya afya ya akili na uzazi hayo ni baahi ya changamoto zinazo wakumba vijana na hupoteza muda mwingi kukaa vijiweni na kusahau kuhusu umuhimu wa wao kujikita katika siasa kwani kwao ni kupoteza muda.
JE HUU NI MUDA SAHIHI, kweli kabisa huu ndio muda muafaka kwa vijana kuingia katika siasa kwani nguvu wanayo, uwezo wanao lakini kuna mambo mengi yanayoruisha nyuma jitihada hizi za vijana wachache ikiwemo upatikanaji wa nafasi katika vyama vya siasa kukosekana kwa mfuko maalumu kwa ajili ya ku gharamia gharama za uchaguzi
Pia viongozi wenye uchu wa madaraka kung’ang’ania nafasi zao, lakini siasa si kugombea tu, bali kujishughulisha na mambo kemkem yanayo husu siasa na, muda ni mali husema na mwishowe hubaki lawama, hasira n ahata vita kwa baadhi yan chi maana nafasi zipo ila wachache bado wamezishika na hawataki kuziachia na jambo lingine la kujiuliza je sheria zetu zinatoa fursa hio?, ni kweli sheria inatoa fursa hio kwa vijana kuwania nafasi mbalimbali kwa vigezo vya umri akili timamu na kusoma na kuandika tuna je unadhani ni wakati pia wa sheria kuweka umri wa kustaafu uongozi?
Kabla huya kusonga mbele ni muda wa kujiuliza,
JE HUU NI MUDA MUAFAKA KWA VIONGOZI WA WALIOKO KWENYE UONGOZI KWA MUDA MREFU KUSTAAFU?
Hivi karibuni kumekuwa na uchaguzi mkuu nchini Kenya uliogusa hisia za Afrika na dunia kwa ujumla na kati ya maswali walioulizwa wananchi juu ya viongozi wao ni je mitano yatosha na wengi walijibu yatosha hii ni kwa wale walioko madarakani na kushindwa kufanya chochote kwa kipindi cha uongozi wao ni swala la kuhoji pia kwa Tanzania je inatosha kwa muda walitumikia, Na waachie nafasi zao?
Kuwa kiongozi ni jambo moja na kuwa kwenye siasa ni jambo lingine, vijana wengi wapo kwenye siasa na kwenye uongozi ni wachache, tatizo moja tu vijana wengi huangalia pale tu ambapo pana maslahi kama hakuna basi hawajishughulishi nalo kabisa hadi itakapofikia siku za uchaguzi ndio utaona kundi kubwa la vijana wakijishughulisha na siasa, tukirudi katika swali hapo juu, ni kweli kuna viongozi wapo mda mrefu kwenye siasa na uongoziwakishika nyazifa mbalimbali kwa miaka nenda rudi wengine wamefanya maendeleo katika maeneo wanayo ongoza kushinda wengine.
Nadhani si vema tukisema wastaafu siasa na uongozi lakini wawe wakufunzi bora kwa vijana wanaoingia kwenye siasa na uongozi lakini pia ni muda sasa wapumzike na kuwaachia vijana, pia serikali ishirikishe Zaidi vijana, katika kufanya maamuzi yake kwani ni kweli wakati wa kale si sasa na nafasi ya vijana katika dira ya siasa na uongozi ni kubwa sana kwa ulimwengu wa sasa hii inaweza chochea ari mpya kwa vijana kuingia ulingoni mwa siasa
Umri pia usiwe kigezo cha kuweka zuio kwa vijana kuwania nafasi mbalimbali kama kijana mwenye miaka 18 anauwezo wa kupiga kura kwanini asigombee nafasi kama za ubunge na nafasi nyingine kwenye utawala?, pia swala la elimu lizingatiwe kwa jamii juu ya nafasi waliyonayo katika siasa na wajibu wao kwa ujumla.
HITIMISHO
WITO KWA VIJANA
Kama vijana tuna wajibu mkubwa wa kujenga taifa letu, tuwe wabunifu, wepesi na wenye morali hasa katika dira ya siasa na uongozi, tujitokeze kwa wingi kuchangia katika Nyanja hii adhimu ya siasa, watu wa sasa husema JIONGEZE n ani mud awa vijana kujiongeza, maana kama nguvu na uwezo wanao nini sasa kiwazuie. Muda ni sasa kuachana kukaa vijiweni kulalamika na kuongea maamuzi yafanywe sasa na taifa letu litakuwa na viongozi wengi vijana walio na uzalendo kwa nchi yao, wasio na woga na walio tayari kufanya mabadiliko, maana nchi ya Tanzania ina asilimia kubwa ya vijana, na huu sio wakati wa kusubiri kuitwa ni wakati wa kuvaa silaha za amani, uzalendo na umoja kujenga Taifa, vijana na siasa ni pande mbili za sarafu moja huwezi tenganisha kamwe.

Upvote
1