Ipi rahisi, nafuu na salama zaidi kati ya kununua gari showrooms na kuagiza kutoka ng'ambo?

Ipi rahisi, nafuu na salama zaidi kati ya kununua gari showrooms na kuagiza kutoka ng'ambo?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Hebu mshauri mTanzania huyu anaekusudia kununua usafiri wake wa gari dogo sasa hivi. Ipi njia rahisi kwake kununua gari kwa urahisi, kwa unafuu wa fedha na muda na kwa usalama zaidi kati ya kuagiza kutoka ng'ambo na kwenda kuchagua tu sehemu mbalimbali yanapuuzwa magari nchini?

Kwa niaba ya mstaafu moja na wadau wengine wenye nia na malengo ya kununua magari hapo mbeleni 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Aagize gari kutoka nnje anapata faida ya waranti ya kimataifa.

 
Kuna faida na hasara za kila njia.
Faida za kununua showroom
1. Ni haraka na unapata gari yako kwa haraka zaidi bila kuwa na wasiwasi mkubwa
2. Unaiona na kukagua muonekano wa gari kwa uhakika zaidi
Hasara zake au mabaya yake
1. Kwa Tz, uaminifu wa dealers wengi unatia mashaka hasa kwenye mileage ya gari
2. Bei huwa juu zaidi ya kama ungeagiza mwenyewe.
Vice versa ni faida na hasara za kuagiza.

Siwezi kusema moja kwa moja ipi ni bora zaidi, kwani inategemea sana uwezo wako kifedha, umakini wako na aina ya gari unayotaka kwa wakati huo
 
Back
Top Bottom