Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Kanisa Katoliki kwa miaka nenda rudi wamekuwa na utamaduni wa kujilimbikizia maeneo makubwa ya ardhi nchi mbalimbali, na ardhi hiyo huwa inasauiliwa Vatican kama milki yao halali.
Kanisa limekuwa likifundisha kwamba tusijiwekee akiba duniani, lakini lenyewe ndio kinara wa kujilimbikizia ardhi.
Haya mafundisho naona yanakinzana na kile ambacho kanisa linakifanya. Sasa ningependa kujua nini dhamira ya kanisa kumiliki haya maeneo makubwa? Kijijini ni mfano tu, kanisa linamiliki zaidi ya heka mia mbili, za nini zote hizi kama sio ulafi tu na ubinafsi?
Hebu tujulishane nyuma ya mpango huu kuna nini kilichojificha?
Kwanini ardhi isajiliwe kama ni mali ya Serikali ya Vatican?
Kanisa limekuwa likifundisha kwamba tusijiwekee akiba duniani, lakini lenyewe ndio kinara wa kujilimbikizia ardhi.
Mathayo 6:19-20
“Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba."Haya mafundisho naona yanakinzana na kile ambacho kanisa linakifanya. Sasa ningependa kujua nini dhamira ya kanisa kumiliki haya maeneo makubwa? Kijijini ni mfano tu, kanisa linamiliki zaidi ya heka mia mbili, za nini zote hizi kama sio ulafi tu na ubinafsi?
Hebu tujulishane nyuma ya mpango huu kuna nini kilichojificha?
Kwanini ardhi isajiliwe kama ni mali ya Serikali ya Vatican?