Ridomil gold
JF-Expert Member
- Aug 22, 2020
- 2,790
- 2,232
Wakimaliza kusoma watakujibu ahsante
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nafikiri wewe akili yako Kama ya panya! Una imani?????????????????!Mama anaupiga mwingi kama Ronaldinho Gaucho...
Watu flani wanateseka sana...
Chapa kazi mama... tuna imani kubwa sana na wewe
Really? Unaota weweHakuna tena anaeogopa kukosoa.
Iwe Jf au hata ma group ya watsap.
Hakuna anaeogopa kutekwa wala kufatiliwa na Nissan nyeupe.
Kila mtu anajiona Yuko huru kutoa mawazo yake.
Wabunge wa CCM sasa wanaikosoa serikali.
Upinzan wanatembea nchi nzima kufanya siasa.
Mahakama zinafanya kazi bila maagizo ya wanasiasa.
Wanamuziki wanaimba bila kuogopa.
Asasi za kiraia zimeanza kufufuka.
Tra imeacha kenyanganya hela kibabe.
Siku 100 za neema tupu kwa waungwana na wenye akili...
Hapa ndipo mnapokera watu, kama kweli Samia alikuwa opposite na mkuu wake, the best decision kwake ingekuwa kujiuzulu na tungeona ukomavu wake kisiasa, angekuwa kinyume na mkuu wake angekataa kuongeza mda katika kipindi cha pili cha utawala wa JPM.RAIS MAGUFULI ALIMWEKA "JELA" MAKAMU WAKE SAMIA SULUHU HASSAN
Na Bollen Ngetti
MWANAMUZIKI Ndanda Kosovo aliwahi kuimba, "Jela..jela ni mbaya, jela..jela ni mateso". Ndanda hakukosea. Aliimba uzoefu alioupata jela hapo Ukonga. Ninamuunga mkono Ndanda kwa uzoefu nilioupata nikiwa jela Keko na Segerea. Jela ni mbaya. Ukiwa jela umezungukwa kuta nene ndefu huwezi kuona nje kwa kifupi unakuwa umenyimwa uhuru wako.
Hata hivyo hakuna jela mbaya duniani kuliko hata Gwantanamo kama jela ya fikra. Yani jela ambapo huwezi kutoa mawazo yako hadharani. Hii ni jela mbaya inayojengwa na shetani tu.
Niliwahi kudokezwa huko nyuma lakini sikuandika maana nilikosa ushahidi kwamba kuna wakati Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitaka kujiuzulu nafasi ya Umakamu kujiondoa kwenye gereza la fikra lakini wenye hekma na busara walimshauri asifanye hivyo.
Kwa namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyoongoza nchi hii kwa siku 100 ni dhahiri alikuwa jela la fikra. Ni ukweli kwamba hakukubaliana na mambo mengi ya Rais Magufuli hata kama leo anasema "Mimi na Magufuli ni kitu kimoja" lakini matendo ni tofauti.
Mama Samia hakukubaliana na uendeshaji wa demokrasia nchini. Alikuwa jela na ilimtesa ndio maana amechukua njia tofauti kuendesha dhana nzima ya demokrasia. Hakuwa na jinsi wala namna. Bila shaka alilia kimya kimya gerezani.
Mama yetu Samia hakupenda uminyaji wa Uhuru wa Habari. Ilimtesa ndio maana "Fundi" alipomwondoa duniani Pombe naye kuchukua hatamu waandishi wa habari wakashangweka. Akaruhusu Uhuru wa Habari na dunia imeshuhudia maana enzi hizo za jela hata andiko hili lisingetoka maana ningekwenda jela la majengo.
Mama Samia hakufurahishwa na kesi za kubumba. Ilimtesa, ilikuwa ni jela kwake ndio maana alipoingia madarakani akafyatua kesi 147 zilizobumbwa na TAKUKURU. Hali hii ilimtesa. Lakini kuachiwa kwa viongozi wa dini wa Uamsho waliosota kwa miaka 9 jela nayo ilimweka jela kisaikolojia Samia. Hakupenda uonevu.
Huyu mama ni swala 5. Ni Muislamu Safi. Hapendi mali za dhulma iwe ni kwa mtu binafsi au Serikali. Hakupenda fedha za dhulma zilizotokana na kesi za kubumba za uhujumu uchumi na ML ndio maana tunaendelea kushuhudia watuhumiwa wakichomolewa magerezani kwa makundi. Lilimuumiza lakini hakuwa na lakufanya maana hakuwa Mkuu wa Maamuzi, Rais. Kitendo cha Mahakama Kuu kuamuru Serikali kurudisha fedha za dhulma kwa kina Mbowe ni ishara nyingine ya kuwa mama yetu aliumia sana kwa matendo hayo. Alikuwa jela.
Makamu wa Rais Samia (sasa Rais) hakupenda watu kuishi kwa hofu na woga. Alitamani watu wawe huru ndani ya nchi yao ila waheshimu Sheria za nchi. Ndio maana leo hata mama lishe, bodaboda nakadhalika wanakwambia, "nchi inafunguka". Wanahisi uhuru walioukosa miaka 5 tuliyoipa kisogo.
Kumbe hata mradi wa Bandari ya Bagamoyo (BEZ) iliyopigwa vita na Pombe ilimkera. Ilimweka jela la kifikra. Hakupenda lakini leo ameamua tufanye mazungumzo mradi ufanyike.
Ndugu zangu, tumuunge mkono Samia kuondokana na gereza la kifikra ili tulisongeshe mbele gurudumu la maendeleo ya nchi.
Binafsi nimejitoa sadaka kumlinda na kumtetea Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan. Mniunge mkono.
Bollen@2021
#MguseMamaNinuke
Ni mtazamo wa Bollen NgetiHapa ndipo mnapokera watu, kama kweli Samia alikuwa opposite na mkuu wake, the best decision kwake ingekuwa kujiuzulu na tungeona ukomavu wake kisiasa, angekuwa kinyume na mkuu wake angekataa kuongeza mda katika kipindi cha pili cha utawala wa JPM.
Msitake kumfanya Samia malaika kwamba hakupenda the way JPM anatawala wakati she was part of his "dictatorial regime" kama mnavumyosema.
Kama angekuwa mtu wa haki, angekataa utawala wa JPM na angejuondoa, ref. Lowassa in 2007. Otherwise tuendelee kuimba mapambio ya CCM coz wametukamata masikio bila kujielewa.
Na wala hatugombani.Yule dingi alikuwa anakula ganja.😝😝😝😝Hakuna tena anaeogopa kukosoa.
Iwe Jf au hata ma group ya watsap.
Hakuna anaeogopa kutekwa wala kufatiliwa na Nissan nyeupe.
Kila mtu anajiona Yuko huru kutoa mawazo yake.
Wabunge wa CCM sasa wanaikosoa serikali.
Upinzan wanatembea nchi nzima kufanya siasa.
Mahakama zinafanya kazi bila maagizo ya wanasiasa.
Wanamuziki wanaimba bila kuogopa.
Asasi za kiraia zimeanza kufufuka.
Tra imeacha kenyanganya hela kibabe.
Siku 100 za neema tupu kwa waungwana na wenye akili...
Mjinga weye.Kama mtu anafanya jambo jema ataachaje kusifiwa?Wote ni Watanzania.Usiwe unakariri visentensi vya lipuuzi.😝😝😝😝😝Ogopa sana kuwa na Rais ambaye hata wapinzani kama CHADEMA na ACT wanamsifia kila kukicha kwenye mitandao.
Rais anayesifiwa na kupongezwa na "wapinzani" ni Rais asiyejua majukumu yake.
Mfano, akitokea Rais Marekani akiwa ni kutoka Republican halafu Democrats wakawa wanamsifia kila siku na kumpongeza basi huo utakuwa ndiyo mwisho au kifo cha siasa Marekani.
Hilo linatokea Tanzania, siasa ndiyo zinakufa sasa. Wapinzani wote wana mahaba na mama.
Akiamka Leo bwana yule atajishangaa sana sana atajua watu walikuwa wana mpuuza tuuOgopa sana kuwa na Rais ambaye hata wapinzani kama CHADEMA na ACT wanamsifia kila kukicha kwenye mitandao.
Rais anayesifiwa na kupongezwa na "wapinzani" ni Rais asiyejua majukumu yake.
Mfano, akitokea Rais Marekani akiwa ni kutoka Republican halafu Democrats wakawa wanamsifia kila siku na kumpongeza basi huo utakuwa ndiyo mwisho au kifo cha siasa Marekani.
Hilo linatokea Tanzania, siasa ndiyo zinakufa sasa. Wapinzani wote wana mahaba na mama.
Wamekosa teuziSijui kwanini wanazi na vijana wa chama chake wamemnunia na wanamsimnga kila kona
Mimi nimejifunza kitu tusichague mgombea alietokea katika umasikin ukampa uongozi ni hatari sanaNdani ya muda mfupi wa utawala wa Mama yetu kipenzi SSH tumeshuhudia yafuatayo;
Mama SSH ni chaguo la Mungu, huyu ni 'Easter' ktk Biblia takatifu.
- Ushetani unatoweka
- Uonevu, uharamia na ujambazi wa kisiasa unakosa nguvu.
- Demokrasia inaanza kutamalaki.
- Ukabila na ukanda unakwenda kupungua.
- Sifa, majigambo, umimi umetoweka
- Ubinafsi nao unakosa nguvu
- Kupotea na kuuawa nako kunakuwa historia.