Ipi tathmini yako kuhusu siku 100 za Rais Samia madarakani?

Mama katuletea matumaini tulikuwa jangwani!
Hakika tulikuwa njia panda yenye miba na upupu mwingi!
Matumaini yalitoweka kiza kilitanda kila mahali!
Dua njema kwa Mama wajameni
 
Mwigulu yupo mtegoni, akifanya mambo ya ajabu anaweza kupotea kwenye anga za kisiasa mazima.
 
Uhuru wa watu hasa kwenye kutoa maoni.
Anapaswa kubadilisha baraza la mawaziri
Kukubali na kutangaza kwamba kuna covid 19 sawa kabisa.
Hahutubii kila mara
Good start
 
Jifunze kusoma historia za mataifa mbalimbali ya namna wanavyoendesha siasa zao.
Ulichoandika hapa kinaonesha uwezo mdogo kabisa wa kujenga hoja.
Kwamba raisi hapaswi kusifiwa na wapinzani!? Ati akisifiwa hajui majukumu yake??? Lumumba mnajuana na shida zenu
 
Katika siku zake 100 amepindua meza kisomi. Ghafla bin vuu kutoka kwenye wa chuma mpaka kwenye uhuru wa kila kitu.
.
.
Akifufuka ghafla mtu aliyefariki kabla ya 17 March,2021 hawezi kuamini kama yupo Tanzania.
 
Lakini si unaambiwa alitaka kujiuzulu akanasihiwa akomae tu. Sasa kama angejiuzulu kama mnavyofikiria je leo angekuwa raisi na kufanya anavyofanya? Pengine hata alilazimishwa kutojiuzulu na boss wake. Hayo yote tuyaache tumpe ushirikiano kwani nyota njema huonekana asubuhi, akiiendesha nje vyema wanufaika ni mimi na wewe na vizazi vyetu kwani sisi sote ni watanzania hata wapinzani ni watanzania pia.
 
Mama anaupiga mwingi yaani anakabia chini kabisa.
Ombi langu kwa kile ambacho Taifa limepitia hyo miaka mi 5 nyuma ni muda wa kushughulikia katiba ambayo itakuwana checks and balance kwa nchi.Hii iliyopo akikaa kichaa anaweza haribu nchi kabisa.
Namuombea kila la kheri Rais wetu Samia Suluhu Hassan.
Kazi iendelee kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
mpaka Sasa bado hakuna alichokifanya.mradi upi amekamilisha au hata kafika 10% tangu pale alipoanzia Hadi Sasa, almost nothing.labda tumpe muda zaidi tuone.
 
mpaka Sasa bado hakuna alichokifanya.mradi upi amekamilisha au hata kafika 10% tangu pale alipoanzia Hadi Sasa, almost nothing.labda tumpe muda zaidi tuone.
Jiwe aliwakamata vizuri sana na kuwapiga vya kutosha kwenye hiyo mnayoiita miradi. Jamaa alikuwa anauma yaani hajui hata kupuliza. Hiyo SGR ikianza kufanya kazi chini ya 2024 nikumbushe nikulipe $100.
 
Mama yuko vizuri. Itoshe tu kusema hivyo.

Kama taifa likienda hivi natumai mpaka miaka 10 tutakuwa mbali sana
Utakuwa mbali eh? Utakuwa umefika wapi? Kwa hiyo, Kwa Maoni yako tulichelewa kumpata huyu mama? Na Kwa Maoni yako Ni Mzuri kuliko Mwalimu Nyerere na Kikwete?
 
Sijui kwanini wanazi na vijana wa chama chake wamemnunia na wanamsimnga kila kona
Mshana hebu acha masihara kwenye mambo ya msingi. Hivi kweli unaongea kutoka kwenye Utosi wa akili yako kuwa huyu ni Kiongozi wa Nchi au yupo kuziba pengo la kikatiba?
 
Jiwe aliwakamata vizuri sana na kuwapiga vya kutosha kwenye hiyo mnayoiita miradi. Jamaa alikuwa anauma yaani hajui hata kupuliza. Hiyo SGR ikianza kufanya kazi chini ya 2024 nikumbushe nikulipe $100.
itafanyaje kazi chini ya 2024yr,wakati aliyeachiwa majukumu,yuko bize kupotosha wananchi na corona.badala ya kusimama na watu,yuko bize na matangazo ya korona,na mbarakoa usoni utadhani ninja.
 
Maisha ni yale yale tu na watawala ni wale wale tu, sioni jipya sana.......anayenufaika na system mpya ndiye atakayesema safi as well as waliokuwa wananufaika na Magu wataponda Utawala wa Sa100.Binafsi naona ni story zile zile tu za watawala wetu.
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…