Ipi top 3 yako ya nyama tamu?

Nyama ya kiboko hapa kitimoto utaona takataka.

Nyama ya Ngiri

Pweza

Ngisi

Nyama ya pofu, we sikia tu ana mafuta kitimoto akasome.

Halafu namalizia na bata, utagundua kuku anapewa sifa sio za kwake
 
Mimi nikishaacha kutumia muda sana na sitokaa nitumie tena ila kitimoto anashina moja /mbili na tatu peke yake
Choma
Roast
Kavu
 
Kuna siku kiboko kafariki huku kwetu,nasikia alipigwa na ndugu zake wakimfukuza kwenye ukoo,ile nyama tuliigawana karibia kijiji kizima na vitongoji vyake kama 10 na zaidi,kwenye familia yangu tulichelewa kuipata hii nyama tulipewa kidogo tu lakin cha kushangaza ikipikwa inaongezeka ni tamu balaa tuliitumia karibia siku tatu na list yangu itakuwa hivi
1.Nyama ya kiboko
2.kuku
3.Ng'ombe ikipata fundi unaweza hisi ina sukari
 
Labda kuku wa kienyeji..lakini wale wa kizungu hawafai kwa mchemsho au hata rosti
 
Ukitaka kujua kama nyama ya Mbuzi,Sungura ,Bata na Kondoo ni balaa..nenda pale darajani kigamboni siku za Jumamosi vuka daraja kidogo tu kushoto.
1. Sungura
2.Bata
3.Kondoo
4.Mbuzi
 
No1. NGISI
No2. PWEZA
No3. Dagaa na samaki wote WA MAJI CHUMVI
No4. KUKU
No5. NG'OMBE nyekundu tu sio mafuta wala mifupa tofauti na hapo sili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…